Tusaidiane kutafakari kauli za mama Diamond

Mzee kaongea kwasababu ya unyonge, hata kidogo ku release maumivu.. Mzee dingi angekuwa na hela anaonekana mtu poa sana.. ukiachana na udhaifu wake mwingine wa kibinadamu
Alipokua nazo pesa hakumthamini mtoto
Nimekutana na kisa cha kumfukuza nasibu harusini ili asile pilau.... kwa kweli usimfanyie mtoto ubaya
 
Wote wamezingua ila huyu mzee nae alizidi....

Yaani kila siku kwenye media kumsema mtoto anayejua sio wake na wala hakumlea! Jina jina tuu, kwani kuna Abdul wangapi buana

Mtoto kutumia jina lake ikageuka fimbo ya kumchapa mama Diamond kila kuchwao! Angekuaga na upendo na nasib yote haya yasingetokea.... Sasa mwenzie nae kachoka kamwaga mboga

Mfanyie ubaya mtu mzima lakini sio mtoto sababu atakua naikumbuka maumivu uliyompa na hujui atakua nani.
Wataalamu wa saikolojia tunaelewa zaidi.. hakunaga vita ya maskini na tajiri..
 
HABARI zilizoshtadi mjini kwa sasa ni kadhia ya mama Diamond kumkana baba Diamond (mzee Abdul) kwa idhlali na taadhira kubwa, kuwa si baba mzazi wa Diamond. Naam hii ni HABARI. Na sisi (kwenye balagha) tunasema hivi:
الخبر هو الكلام الذي يحتمل الصدق والكذب لذاته، اي؛ الكلام المقال نفسه.
Yaani kwa ufupi: HABARI ni maneno yanayopelekea UKWELI na/au UONGO kutokana na uthibitisho wake. Kwahiyo, sifa ya HABARI yoyote ile duniani, ni kubeba taarifa ya KWELI au ya UONGO. Sasa, utajuaje kwamba HABARI flani ni ya KWELI au ya UONGO? Wanazuoni wa Balagha wanafafanua:
ان طابق الكلام الواقع كان صدقا، وان لم يطابق الواقع كان كذبا.
Yaani, ikiwa maneno (habari) yatafungamana na uhalisia/mazingira basi maneno hayo yatachukuliwa ni KWELI. Na ikiwa maneno hayo hayatofungamana na uhalisi/mazingira basi yatachukuliwa ni UONGO.

Mathalani: Ikiwa bado mmelala ndani (kwenye nyumba ya wazi), halafu asubuhi akaingia mtu kukwambia kwamba tayari JUA linawaka nje. Ikiwa kauli yake itafungamana na uhalisia/mazingira (Ukaona mwaga/miale ya jua imeanza kupenya ndani), basi kauli yake itachukuliwa kuwa ni KWELI. Walakini, ikiwa maneno yake hayatoambatana na mazingira/uhalisa (kwamba ndani hakuna miale—na giza bado limetamalaki), basi maneno yake yatachukuliwa kuwa ni UONGO.

Kwa utangulizi huo. Sasa, tunaweza kutumia maneno ya mama Diamond—ambayo yamezua HABARI kubwa—ili kuona kama yamebeba UKWELI au UONGO kutokana na mazingira/uhalisa wake:

1. Mama Diamond anasema kuwa, mzee Abdul hakuwa baba mzazi wa Diamond, inakuaje tena (yeye huyo huyo) aseme kwamba, mzee Abdul aliikataa mimba? Alikataaje kitu (mimba) ambacho si chake? Na kama ni kweli ALIIKATAA, maana yake ni kwamba, basi mama Diamond alitaka kumpa hiyo mimba. Kwanini alitaka kumpa kitu (mimba) ambacho siyo chake? Kwa lugha rahisi alitaka KUMBAMBIKIA). Je, kosa la mzee Abdul ni kukataa kubambikwa?
Hili swali naomba walijibu watoto wa darasa la pili kwa sababu ni jepesi sana. Lakini maswali yanayofuata sasa ndo naomba yajibiwe na watu wazima:

2. Mama Diamond amesema kwamba, mzee Abdul hakuwa baba mzazi wa Diamond—alikuwa ni baba mlezi tu. Pia, yeye huyo huyo akasema tena kuwa, mzee Abdul aliahidi kumlea Diamond lakini HAKUMLEA (rudia hilo neno—HAKUMLEA). Na hata yeye (mama Diamond) hakuwahi kuishi kwa mzee Abdul—na hata picha walizoonekana wakiwa pamoja (kipindi Diamond akiwa mtoto), ilikuwa tu wamepita kumsalimia mzee Abdul hapo Magomeni alipokuwa akiishi.
Swali: Je, mtu ambaye umesema hakuwa baba mzazi wa mtoto, na umesisitiza kuwa HAKUMLEA, hicho cheo cha "BABA MLEZI" kilitoka wapi? Alikuwa analea nini?

3. Mama Diamond amesema, mzee Abdul alikataa mimba (ubaya), lakini pia amesema, hakuwa akihudumia kama alivyoahidi (ubaya), pia amesisitiza kuwa, mimba haikuwa yake (ubaya). Kwa lugha rahisi, mama Diamond ameamua kumpaka UBAYA mzee Abdul. Swali: Kama hayo ni kweli, je, hizo pesa ambazo mama Diamond alikuwa anapewa mara kwa mara na Diamond ili akampatie mzee Abdul zilikuwa zinakwenda kwa mzee Abdul kama nani? (Maana mtoto hakumzaa yeye, na wala hakumlea).

4. Mama Diamond amesema, alimpa Diamond ubini wa Abdul kwa sababu (mzee) Abdul ndiye aliyempeleka hospitali kujifungua. Pamoja na hayo, amesisitiza kuwa bwana Salum Nyange (anayemtaja kuwa ndiye baba mzazi wa Diamond), alikuwa anakwenda Tandale kumangalia mtoto (Diamond) kama kawaida. Maana yake ni kwamba, mzee Salum Nyange hakumkataa mtoto. Swali: Inawezekanaje mtu yule yule (mzee Abdul) aliyetaka kubambikwa mimba akaikataa, ndiye akasimama kidete kumpeleka mama Diamond hospitali? Kama mwenye mimba (Salum Nyange) alikuwepo na hakukataa mimba, ilikuwaje mama Diamond ampe mtoto (Diamond) u-bini wa mtu mwingine (mzee Abdul) kisa tu alimpeleka hospitali kujifungua? Je, ilikuwaje mzee Abdul akaahidi KUMLEA Diamond ilhali baba mzazi wa Diamond (bwana Salum Nyange) alikuwa hai na alikuwa anakwenda kumwangalia mtoto?

Somo la HABARI Kibalagha ni pana sana. Tungeweza kwenda mbali zaidi, kwa kuangalia, je, HABARI iliyoletwa na mama Diamond ilikuwa ni HABARI ya awali yenye kutoa taarifa (الخبر الابتداىي), au ilikuwa ni HABARI ithibitishayo taarifa yenye mashaka (الخبر الطلبي), au ilikuwa ni HABARI yenye kusisitiza jambo lililobishiwa ( الخبر الاءنكاري)?

Ukimsikiliza mama Diamond, anasisitiza kuwa hata mzee Abdul mwenyewe ANAJUA kwamba si baba mzazi wa Diamond. Msisitizo huu unaonesha kwamba habari/maneno hayo yaliwahi KUBISHIWA ( الخبر الاءنكاري). Lakini, ukimsikiliza mzee Abdul, muda mfupi baada ya mahojiano aliyofanya mama Diamond, utamsikia akisema: HABISHI kuwa yeye si baba yake Diamond. AMEKUBALI baada ya kusikia kauli ya mama Diamond. Siku zote hakuwa na YAKINI juu ya hili. Kwa hivyo, hii ni habari mpya kwake (الخبر الابتداىي). Swali: kwanini mama Diamond alitumia MKAZO kana kwamba baba Diamond aliwahi kubishia HABARI hii ( الخبر الاءنكاري)?

Kwa kutumia NYENZO za balagha ili kupambanua habari hii, nadhani kila mmoja anaweza kuja na majibu yake bila kutaghadhabu. Mimi nimechochea TAFAKURI tu—na mpira nimeuacha kwenu.

Maundu Mwingizi (Mwanabalagha).View attachment 1678805
Hii picha huyu mzee alikuwa handsome balaa.akicheka kama akina p square duh
 
Alipokua nazo pesa hakumthamini mtoto
Nimekutana na kisa cha kumfukuza nasibu harusini ili asile pilau.... kwa kweli usimfanyie mtoto ubaya
Hili swala, kila mtu anajivua na kuonekana hana hatia. Ila mwenye matatizo ni mke inavyo onekana na hakuwa muaminifu, we kila mtoto na babake huoni ni shida.. hili jambo lina mzizi .. ila wenye pesa wamezingua kinyama
 
It's true, ndio maana Abdul alipokua tajiri nasib na mamake walikua wanyonge
Dunia duara
Huyo mzee hajawai kuwa tajiri. Tazama picha za zamani kati ya huyo mzee na hiyo mke na diamond.. kama ni mtu unaeweza tafsiri picha utaelewa maisha yao. Ila baraa huenda lilianza mama alipo anza pigwa nje wazi wazi.. ndio ibiri alipo ingia. Na mzee hakuwa na shida, ila baada ya mama kufanya hivyo alianza taka tumia mgongo wa mtoto.. kitu ambacho kimeleta haya yote
 
Hili swala, kila mtu anajivua na kuonekana hana hatia. Ila mwenye matatizo ni mke inavyo onekana na hakuwa muaminifu, we kila mtoto na babake huoni ni shida.. hili jambo lina mzizi .. ila wenye pesa wamezingua kinyama
Nasib angekua teja leo mzee abdul asingejulikana ila mama yake angekua anapambana mwananyamala kumchukulia dose
Sasa kawa maarufu na mwenye kipato mtamu
 
Nasib angekua teja leo mzee abdul asingejulikana ila mama yake angekua anapambana mwananyamala kumchukulia dose
Sasa kawa maarufu na mwenye kipato mtamu
Pesa si maamuzi katika hati ya maisha ya mtu. Hakuna ajue kesho, bado mzee Nasib anabaki kuwa muhimu na mama nasib anabaki kuwa muhimu, wameshindwa tu kusamehana na kuchukuliana katika mapungufu yao. Ndio maana kuna kutupiana mpira
 
Kwahiyo mzee abdul alikua anakula mzigo tu hakubahatika kuzaa nae vi sandra hata mtoto mmoja sio
 
Ndo maana naipenda pombe.... Nkilewa naenda zangu kulala tu, haya mambo ya familia za wengine yatanivuruga akili
 
Diamond ndiye ana- entertain huu utoto labda kwa sababu anafaidika nao kwa namna moja au nyingine.

DNA test itamgharimu 200K tu pale kwa mkemia Mkuu.

Anakata mzizi wa fitna.
 
Kashachanganyikiwa
Labda mimi simfuatilii sana lakini huyu mzee hayupo kwenye kundi la wanaume wanaolazimisha kulelewa na watoto wao kisa wamepata utajiri. Pia sioni inawezekana vipi wewe mwanamke umpe mwanao jina la ukoo wa mwanaume ambaye si baba wa mtoto na ambaye hakumlea huyo mtoto huku oia akiikataa mimba ilhali baba halisi wa mtoto yupo na unamfahamu na amekuwa akimtembelea mtoto. Aliyechanganyikiwa atakuwa huyo mwanamke. Bika shaka.
 
Kbsa lkn huyu mzee hajui kujiongeza
Anawashobokea wakina zamaradi,sjui global tv etc angewakaziaaa

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
Yaani anatakiwa awe na msimamo. Tena anakuwa na account benki wanamuwekea mpunga wake wote kabla ya kuhojiwa. Na anakuwa na stopwatch kabisa na mabodigadi. Muda ukiisha mabodigadi wanawafukuza waandishi na makamera yao mpaka waongeze mpunga benki. Mpaka sasa kwa bei ya laki mbili kwa dakika angeshapata 12m kwa lisaa. Na hizi youtube channel ndogondogo angepata 1m mpaka 3m kwa kuhojiwa tu. Na wale wanaompigia simu kumuhoji kwa dakika tano wangempa 1m. Angepata pesa yake kiurahisi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom