Tusaidiane kutafakari kauli za mama Diamond

Aug 1, 2016
7
17
HABARI zilizoshtadi mjini kwa sasa ni kadhia ya mama Diamond kumkana baba Diamond (mzee Abdul) kwa idhlali na taadhira kubwa, kuwa si baba mzazi wa Diamond. Naam hii ni HABARI. Na sisi (kwenye balagha) tunasema hivi:
الخبر هو الكلام الذي يحتمل الصدق والكذب لذاته، اي؛ الكلام المقال نفسه.
Yaani kwa ufupi: HABARI ni maneno yanayopelekea UKWELI na/au UONGO kutokana na uthibitisho wake. Kwahiyo, sifa ya HABARI yoyote ile duniani, ni kubeba taarifa ya KWELI au ya UONGO. Sasa, utajuaje kwamba HABARI flani ni ya KWELI au ya UONGO? Wanazuoni wa Balagha wanafafanua:
ان طابق الكلام الواقع كان صدقا، وان لم يطابق الواقع كان كذبا.
Yaani, ikiwa maneno (habari) yatafungamana na uhalisia/mazingira basi maneno hayo yatachukuliwa ni KWELI. Na ikiwa maneno hayo hayatofungamana na uhalisi/mazingira basi yatachukuliwa ni UONGO.

Mathalani: Ikiwa bado mmelala ndani (kwenye nyumba ya wazi), halafu asubuhi akaingia mtu kukwambia kwamba tayari JUA linawaka nje. Ikiwa kauli yake itafungamana na uhalisia/mazingira (Ukaona mwaga/miale ya jua imeanza kupenya ndani), basi kauli yake itachukuliwa kuwa ni KWELI. Walakini, ikiwa maneno yake hayatoambatana na mazingira/uhalisa (kwamba ndani hakuna miale—na giza bado limetamalaki), basi maneno yake yatachukuliwa kuwa ni UONGO.

Kwa utangulizi huo. Sasa, tunaweza kutumia maneno ya mama Diamond—ambayo yamezua HABARI kubwa—ili kuona kama yamebeba UKWELI au UONGO kutokana na mazingira/uhalisa wake:

1. Mama Diamond anasema kuwa, mzee Abdul hakuwa baba mzazi wa Diamond, inakuaje tena (yeye huyo huyo) aseme kwamba, mzee Abdul aliikataa mimba? Alikataaje kitu (mimba) ambacho si chake? Na kama ni kweli ALIIKATAA, maana yake ni kwamba, basi mama Diamond alitaka kumpa hiyo mimba. Kwanini alitaka kumpa kitu (mimba) ambacho siyo chake? Kwa lugha rahisi alitaka KUMBAMBIKIA). Je, kosa la mzee Abdul ni kukataa kubambikwa?
Hili swali naomba walijibu watoto wa darasa la pili kwa sababu ni jepesi sana. Lakini maswali yanayofuata sasa ndo naomba yajibiwe na watu wazima:

2. Mama Diamond amesema kwamba, mzee Abdul hakuwa baba mzazi wa Diamond—alikuwa ni baba mlezi tu. Pia, yeye huyo huyo akasema tena kuwa, mzee Abdul aliahidi kumlea Diamond lakini HAKUMLEA (rudia hilo neno—HAKUMLEA). Na hata yeye (mama Diamond) hakuwahi kuishi kwa mzee Abdul—na hata picha walizoonekana wakiwa pamoja (kipindi Diamond akiwa mtoto), ilikuwa tu wamepita kumsalimia mzee Abdul hapo Magomeni alipokuwa akiishi.
Swali: Je, mtu ambaye umesema hakuwa baba mzazi wa mtoto, na umesisitiza kuwa HAKUMLEA, hicho cheo cha "BABA MLEZI" kilitoka wapi? Alikuwa analea nini?

3. Mama Diamond amesema, mzee Abdul alikataa mimba (ubaya), lakini pia amesema, hakuwa akihudumia kama alivyoahidi (ubaya), pia amesisitiza kuwa, mimba haikuwa yake (ubaya). Kwa lugha rahisi, mama Diamond ameamua kumpaka UBAYA mzee Abdul. Swali: Kama hayo ni kweli, je, hizo pesa ambazo mama Diamond alikuwa anapewa mara kwa mara na Diamond ili akampatie mzee Abdul zilikuwa zinakwenda kwa mzee Abdul kama nani? (Maana mtoto hakumzaa yeye, na wala hakumlea).

4. Mama Diamond amesema, alimpa Diamond ubini wa Abdul kwa sababu (mzee) Abdul ndiye aliyempeleka hospitali kujifungua. Pamoja na hayo, amesisitiza kuwa bwana Salum Nyange (anayemtaja kuwa ndiye baba mzazi wa Diamond), alikuwa anakwenda Tandale kumangalia mtoto (Diamond) kama kawaida. Maana yake ni kwamba, mzee Salum Nyange hakumkataa mtoto. Swali: Inawezekanaje mtu yule yule (mzee Abdul) aliyetaka kubambikwa mimba akaikataa, ndiye akasimama kidete kumpeleka mama Diamond hospitali? Kama mwenye mimba (Salum Nyange) alikuwepo na hakukataa mimba, ilikuwaje mama Diamond ampe mtoto (Diamond) u-bini wa mtu mwingine (mzee Abdul) kisa tu alimpeleka hospitali kujifungua? Je, ilikuwaje mzee Abdul akaahidi KUMLEA Diamond ilhali baba mzazi wa Diamond (bwana Salum Nyange) alikuwa hai na alikuwa anakwenda kumwangalia mtoto?

Somo la HABARI Kibalagha ni pana sana. Tungeweza kwenda mbali zaidi, kwa kuangalia, je, HABARI iliyoletwa na mama Diamond ilikuwa ni HABARI ya awali yenye kutoa taarifa (الخبر الابتداىي), au ilikuwa ni HABARI ithibitishayo taarifa yenye mashaka (الخبر الطلبي), au ilikuwa ni HABARI yenye kusisitiza jambo lililobishiwa ( الخبر الاءنكاري)?

Ukimsikiliza mama Diamond, anasisitiza kuwa hata mzee Abdul mwenyewe ANAJUA kwamba si baba mzazi wa Diamond. Msisitizo huu unaonesha kwamba habari/maneno hayo yaliwahi KUBISHIWA ( الخبر الاءنكاري). Lakini, ukimsikiliza mzee Abdul, muda mfupi baada ya mahojiano aliyofanya mama Diamond, utamsikia akisema: HABISHI kuwa yeye si baba yake Diamond. AMEKUBALI baada ya kusikia kauli ya mama Diamond. Siku zote hakuwa na YAKINI juu ya hili. Kwa hivyo, hii ni habari mpya kwake (الخبر الابتداىي). Swali: kwanini mama Diamond alitumia MKAZO kana kwamba baba Diamond aliwahi kubishia HABARI hii ( الخبر الاءنكاري)?

Kwa kutumia NYENZO za balagha ili kupambanua habari hii, nadhani kila mmoja anaweza kuja na majibu yake bila kutaghadhabu. Mimi nimechochea TAFAKURI tu—na mpira nimeuacha kwenu.

Maundu Mwingizi (Mwanabalagha).
FB_IMG_1610711846459.jpg
 
Ila sijui kama ni kutafuta sifa au ni elimu ndogo au ni vyote.

Mmoja aliwahi sema kuwa huyo mama akiwa hai daimond hawezi oa.

Yaani kitendo cha mwanaume wa watu kuomba daimond amkatie bima ya afya ndo mama kapanic,

Anyways ni maisha yao tuwaachie
 
Maundu Mwingizi (Mwanabalagha).View attachment 1678805

huo mkono wa jamaaa naona una fanya Fleming's Left Hand Rule
 
Mod ebu futa hizi habari maana face book na Instagram hatuingii sababu kuna habari za ajabu ajabu kama hizi maana hizi ni personal issues wamalizane wao siye hayatuhusu
 
Jinsi unavyopoteza muda kujaribu kuelewa ndivyo hutoelewa, we wasikilize burudika hata usitafakari wanachokisema maana huwezi kuelewa hata kidogo.
 
Ila sijui kama ni kutafuta sifa au ni elimu ndogo au ni vyote.

Mmoja aliwahi sema kuwa huyo mama akiwa hai daimond hawezi oa.

Yaani kitendo cha mwanaume wa watu kuomba daimond amkatie bima ya afya ndo mama kapanic,

Anyways ni maisha yao tuwaachie
Kuwa mama na kujiita mama siyo kwenda labour tu kna mambo ya ziada pia unahitaji
Maana hata chizi anazaa .....sijui umenielewa?
mama D

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
+mgt pale
Hebu wapitie background ya maisha ya huyu mama majibu watu watapata

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
Huyo mama katembeza mbunye hapo kariako hadi hajielewi watoto aliopata baba zao

Hao kina ESMA dangote ,Queen darlin ,Ricardo mom ,diamond

Ukifuatilia baba zao ni kizungu mkuti ,hawajulikan wametokea wapi

Wote hao ni wanaharamu tu
 
Kuwa mama na kujiita mama siyo kwenda labour tu kna mambo ya ziada pia unahitaji
Maana hata chizi anazaa .....sijui umenielewa?
mama D

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app

Mwanamke anakua mama kwa kuzaa na hata kwa kulea

Haya mambo ya hii familia kila mtu ata judge vile aonavyo yeye na katika level yake ya maisha na kile tunachokiita ustaarabu... bila kujali uhalisia wa maisha ya mama diamond kipindi hicho na changamoto alizopambana nazo

Ila yote kwa yote mvaaji wa kiatu ndio ajuae maumivu yalipo na mbeba mimba, mwenda labor na anayelea ndio anayejua mapito aliyopita kufikisha kijana wake alipo

Tabia nyingi za watu tunazoziona mbovu leo zilitengenezwa na jamii inayowazunguka kwa maumivu waliyopitia na kusurvive hadi kufikia walipo
 
Huyo mama katembeza mbunye hapo kariako hadi hajielewi watoto aliopata baba zao

Hao kina ESMA dangote ,Queen darlin ,Ricardo mom ,diamond

Ukifuatilia baba zao ni kizungu mkuti ,hawajulikan wametokea wapi

Wote hao ni wanaharamu tu
Mbona keshamtaja baba wa mtoto? Hajui nini tena
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom