Turufu ya CCM ni January Makamba

crabat

JF-Expert Member
Dec 28, 2012
4,322
2,000
Katika wagombea wana CCM 40 walio nesha nia ya kutaka kuteuliwa na chama chao kupeperusha bendera ya urai uchaguzi ujao ni January MAkamba pekee ndie mwenye uwezo wa kuijenga CCM mpya kabisa itayopendwa na na wapiga kura wapya miaka 10 ijayo.

Ni kijana mwenye uwezo katika nyanja zote. Ni msomi ambaye ataivusha ccm katika hali ya sasa ya kuanza kukataliwa na miaka 10 ijayo anaweza kabisa kuvunja umaarufu wa vyama vya siasa vilivopo.

Ni pekee asie na majungu wala kashfa ya rushwa.

Hana makundi ndani ya CCM.

Anakubalika kwa kiasi kikubwa na wasomi vijana wasomi.

Hata baadhi ya wapinzania wana muona kama turufu kubwa kwa CCM. Kama CCM inaandaa viongozi basi huyu amekomaa na ni asset kubwa sana kumtumia kukuvusheni.

Vijana wengi sasa wamechoshwa na old guards amabao ukweli hawana jipya.

Janaury anaweza kutuvusha , ni well informed person , ni kwa kiasi mwanadiplomasia makini, msikivu na mpenda watu na maendeo.

Pia ni mzalendo anaeipenda nchi yake na watu wake.

Huu ni wakati mzuri kwa ccm kama chama kikongwe na chenye uzoefu basi kuleta mapinduzi ya uongozi ili kukaribisha fikra mpya ambazo ndio muelekeo ya wapiga kura wengi wajao.

Namfananisha na Barack OBama kijana aliengia kwa gia yake ya change And yes we can.

Leo chini ya Obama kwanza amekijenga chama chake na kuna kila sababu kitarudi tena madarakani.

Pia amejaribu kupunguza uadui katika sera zake za nje.

Iran sasa wanazungumza badala ya vitisho.

Amerudisha uhusiano wa Kibalozi na Cuba baada ya zaidi ya miaka 50.

Ameujenga uchumi wa marekani ilo haribiwa na vita na magomvi na Bush. Hakika namfananisha January na Obama he will bring change to TAnzania, ukweli tunahitaji Dot.Com kutuvusha.

Mungu amsaidie na awape CCM hekima ya kuona mbali na kuachana siasa za makundi.
 

SOGHOO

JF-Expert Member
Mar 25, 2015
1,268
2,000
Makamba yuko team Lowasa. Mlikua hamsomi hotuba zake ? akienguliwa tu anahamia kwa mtarajiwa ndani ya CCM japo nae this taim atawaachia ukawa walipize visasi.
 

wiseboy.

JF-Expert Member
Aug 11, 2014
3,803
2,000
Mtoa mada wewe ni mjinga flani usiye na akili hata kidogo,unathubutu kumfananisha mtu mshenz kama january na obama? Janauary hana ubongo wa kuongoza USA,Hakuna mwana ccm atakayeweza kuitoa Tanzania ktk umaskini,miaka 54 wameshindwa,leo wana mpya gani? Huyu january huyu aliyekomalia cybercrime act ikapita ndo awe rais?

Kama amekununulia bia uje umpe promo rudi kamwambie hatutaki uchafu unaoitwa ccm,go to hell ccm,tumewachoka kabisa,hamna jipya,ubongo wa mmarekani obama unaufananisha na ubongo mbovu wa mtu wa pwani mwana ccm aliyezoea dhiki na joto kali? dead ideas,kweli ccm mmelaaniwa kabisa nyambafu zenu.
 

crabat

JF-Expert Member
Dec 28, 2012
4,322
2,000
mh..!mzee wa cybercrime tanzania itakua kama north korea
Sheria hii ni mbaya na nzuri..lakini cyber crime zipo na wizi wa mtandao upo na mabenki yana fanya hasara kubwa kutokana na wizi wa mtandao kiasi makampuni ya bima ya nje yanakataa kusupport coverage eneo hili kwa mabenki yetu.ama kuhusu habari za mtandao bado wewe na mimi tunatamba ndani ya jamiiforums na kwa uhuru kabisa na hakuna aliefuatiliwa.

Ubaya upo wa sharia hii lakini ndio sharia hata mwizi ukimwekea sharia ya kukata mkono atasema oooh haki za binadamu...lakini anasahau dawa ni kuacha kuiba
 

crabat

JF-Expert Member
Dec 28, 2012
4,322
2,000
Mtoa mada wewe ni mjinga flani usiye na akili hata kidogo,unathubutu kumfananisha mtu mshenz kama january na obama? Janauary hana ubongo wa kuongoza USA,Hakuna mwana ccm atakayeweza kuitoa Tanzania ktk umaskini,miaka 54 wameshindwa,leo wana mpya gani? Huyu january huyu aliyekomalia cybercrime act ikapita ndo awe rais?Kama amekununulia bia uje umpe promo rudi kamwambie hatutaki uchafu unaoitwa ccm,go to hell ccm,tumewachoka kabisa,hamna jipya,ubongo wa mmarekani obama unaufananisha na ubongo mbovu wa mtu wa pwani mwana ccm aliyezoea dhiki na joto kali? dead ideas,kweli ccm mmelaaniwa kabisa nyambafu zenu.

Naheshimu sana mchango na mawazo yako. Lakini na kataa kama mimi ni mjinga.Niko well informed and educated
Na pia situ muwi na mtu yoyote in fact sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa leo wala wakati ule wa chama kimoja japo niliwahi kufanya kazi serikalini lakini sikuwahi kuwa mwana ccm/tanu.Mawazo yangu yapo huru .

Obama ni msomi kama January , wote ni vizazi vya Millenials wote ni wasomi na well informed , tofauti yao ni mazingira tu ya mahala.

Obama anaongoza taifa kubwa lenye nguvu na uchumi mkuu duniani. January anategema kuongoza taifa masikini tegemezi,lenye kila aina ya changamoto .umaskini , elimu duni rushwa nk ...ujana na nguvu yake , elimu yake, muono wake , na upendo wake utalisaidia Taifa hili. Kumfananisha na Obama si kwa maana yakuongoza Marekani...bali vision yake ya change ni sawa na ile ya Obama na anaweza kuisimamia.


Ama kuhusu mtu wa pwani hili nalichukulia ni tatizo laukabila linalo kulabil...sehemu ya mtu anapotoka haina mantiki yoyote kwa vizazi vya sasa. Hata USA walimsema Obama kutoka kisumu , mkenya , muislam aliesoma islamic school lakini ameonesha uwezo mkubwa na kuwa prove wrong wabaguzi wenye chuki za kijinga kama wewe.

Mwisho uwezo wa ccm Tanzania bara bado ni mkubwa,tunakubali CCM inakabiliwa na matatizo ya rushwa ubinafsi na makundi lakini kama Taasisi bado nipekee kinachoweza kuongoza Tanzania Bara.

Nafasi ya vyama vya upinzani kama taasisi bado zina walakini wapo viongozi makini mfano ni Lipumba na Mbatia pekee ndio wenye haiba na uwezo wa kuwa viongozi wa nchi hii lakini tatizo kubwa lipo kwenye vyama vyao , kama taasisi zipo weak sana na mara nyingi vipo kikanda au kikabila zaidi..sio vyama vya kitaifa haswa.

Tusubiri Zitto na chama chake miaka ijayo kinaweza kuwa chama cha kitaifa na mbadala wa CCM.

Upande wa Zanzibar CCM nakubali kimeshindwa na kama taasisi imejengengeka kimapinduzi zaidi hivyo sera zake za kibabe zaidi na kibaguzi hizo zimepitwa na wakati na wao wenyewe ni wagumu kubadilika ndio maana vijana wengi wamewaacha mkono.
 

Ngwananzengo

JF-Expert Member
Jul 28, 2012
1,911
2,000
Duuuhh kumbe siku hizi ukiwa na Cheti wewe ni msomi? Kafanya utafiti upi ambao utamweka kwenye orodha ya wasomi? Hivi anadhani ule udalali aliokuwa anaufanya pale kwenye jengo jeupe anadhani tumeusahau.
 

chakufia nini

JF-Expert Member
Apr 14, 2015
692
170
crabat

Shusha cv ya Makamba hapa tuone ana nini kwenye kapu lake na amejiandaaje kielimu kuiongoza Tanzania.
 
Last edited by a moderator:

crabat

JF-Expert Member
Dec 28, 2012
4,322
2,000
Duuuhh kumbe siku hizi ukiwa na Cheti wewe ni msomi? Kafanya utafiti upi ambao utamweka kwenye orodha ya wasomi? Hivi anadhani ule udalali aliokuwa anaufanya pale kwenye jengo jeupe anadhani tumeusahau.

Kuwa msomi sio lazima kuongea ki English. msomi ni pamoja na mtu mwenye tabia ya kujisomea vitabu tofauti,Mtu anaependa kujiendeleza ili awe up to date...na January ni mtu wa aina hio...hakukoma alipomaliza chuo..bado anasoma.
 

crabat

JF-Expert Member
Dec 28, 2012
4,322
2,000
chakufia nini

Early life and career
Makamba was born in Singida Region and is the eldest of fourchildren. His father, Yusuf Makamba,a stalwart of the country's dominantruling party, the Chama Cha Mapinduzi(CCM) and had served as its Secretary General. His mother, Josephine, is fromMissenyi District in Kagera Region.He spent his early childhood in his ancestral home of Mahezangulu village in Lushoto District and at his maternalgrandmother's village in Kagera Region, which was at the time invaded byUgandan troops during the Uganda–Tanzania War.[SUP][2][/SUP]

He was educated at Handeni and Galanossecondary schools in Tanga Region;and at ForestHill High School. He attended Quincy College in Massachusetts, United States for apreliminary course before transferring to SaintJohn's University in Minnesota, where he majored in PeaceStudies.[SUP][3][/SUP] He thenundertook an internship at the Carter Center,[SUP][4][/SUP] beforeobtaining his MSc in Conflict Analysis and Resolution from the Schoolfor Conflict Analysis and Resolution at George MasonUniversity in 2004.[SUP][5][/SUP]

Upon his return to Tanzania, he joined the Foreign Ministry as a Foreign ServiceOfficer (Grade II). Jakaya Kikwete,the ForeignMinister at the time would later on vie for the presidency in the 2005election. Makamba joined his campaign team and traversed across thecountry visiting all the districts.Following Kikwete's landslide victoryof over 80 percent, he was appointed as an aide tothe President. His formal title was Personal Assistant to the President –Special Duties (PAP-SD); a position that he would serve for five yearsuntil 2010.[SUP][5][/SUP]

Political career
In 2010, he contested in the electionas a Member of Parliament for his home constituencyof Bumbuli and was elected unopposed.[SUP][6][/SUP] In the 10thParliament, he served as the Chairman of the Parliamentary Committeefor Energy and Minerals.

In April 2011, he replaced Bernard Membe as CCM's Political Affairsand International Relations Secretary and served in this post until November2012 when he was succeeded by Asha-Rose Migiro at the 8th NationalCongress of the CCM.[SUP][7][/SUP] Makamba wasalso elected as one of the ten members of the National Executive Committee(NEC) from the mainland part of the country. He received the second highestnumber of votes (2,093).[SUP][8][/SUP]

In May 2012, PresidentKikwete appointed him as the Deputy Minister of Communication, Science andTechnology following a cabinet reshuffle.In July, he launched the Bumbuli Development Corporation, a personal initiativethat would seek to supplement the government's effort in bringing developmentto his constituency.[SUP][9][10][/SUP] In August2014, he was nominated by Vodacom Tanzania CEO to participate in the Ice BucketChallenge in order to raise awareness for obstetric fistula patients in Tanzania; ordonate US$ 100.[SUP][11][/SUP] Makambadecided to donate TSh 1million (US$ 600) instead.[SUP][12][/SUP]

In October 2014, Makamba was quoted advocating dictatorship as a means to end graft in politics.[SUP][13][14][/SUP]

2015 presidential campaign
In February 2014, Makamba along with five other partymembers were warned by the CCM's Central Committee not to engage in prematurecampaigns for the 2015presidential election.[SUP][16][/SUP] On 2 July2014, he announced on BBC Swahili that he was 90% certain that he would contestin his party's primaries for thepresidency.[SUP][17][18][19][/SUP]

On 9 July 2014, President Kikwete whilst on a four dayofficial tour of Tanga Region,addressed Makamba's constituents and praised their MP for his work. On hispresidential ambition, Kikwete advised that he shouldn't 'force things' andthat when the time comes, he would get the presidency.[SUP][20][/SUP] Makambaclarified that Kikwete's remarks were taken out of context by the media and that he wassupportive of his planned bid.[SUP][21][/SUP]

His top priority will be on job creation and if elected, he willintroduce a jobs bill that will need about $2 billion.[SUP][22][/SUP] In January2015, a book authored by Fr. Karugendo was launched titled 40 Questions 40Answers: A Conversation with January Makamba.[SUP][23][/SUP] Its preface was written by retired President Ali Hassan Mwinyi.[SUP][24][/SUP]

Personal life
Makamba is a MuslimHe is marriedto Ramona and is the father of two children. He is an avid football fan andsupports Coastal Union,Chelsea and Real Madrid in the Tanzanian,Englishand Spanishleagues.[SUP][26][27][/SUP]

Honours and awards

 
Last edited by a moderator:

Yegomasika

JF-Expert Member
Mar 21, 2009
13,174
2,000
crabat

Obama na January sidhani kama wapo kwenye hilo kundi la Millennial Generation or Generation Y. Millennial Generation ni waliozaliwa from the early 1980s to the early 2000s.
 
Last edited by a moderator:

bopwe

JF-Expert Member
Oct 1, 2013
1,769
2,000
Hii ni sahihi kabisa...huyu kijana ndie nyota mjema kwa ccm.
Anazo sifa na hana makundi..vision yake tofauti na wazee wa kale ambao hawana jipya kutupatia
 

Macos

JF-Expert Member
May 12, 2008
1,976
2,000
KWANINI TUNAMHITAJI JANUARY ?
Zaidi ya 85% ya wafanyakazi na nguvu kazi Tanzania ni vijana walo zaliwa baada ya Uhuru 1961. Nusu ya vijana hawa ni kizazi cha Millenia walo zaliwa miaka ya 1980’s na wana umri wa wa chini ya miaka 35.Hawa wengi ni dot.com generation hawa kuwepo nchi ilipopata uhuru na hasa ilipitia hatua gani hadi kufika hapa tulipo fikia. Hawajui yalio tokea wakati wa kujaribu sera mbali mbali kuanzia ubepari , Ujamaa , liberised economy , hawa kuwepo nchi..ilipokuwa na raha au shida mbali mbali .Wengi hawajui zaidi ya kusimuliwa nchi wakati wa Ujamaa ilikua na ladha gani.wengi wamekuwa na matarajio na mafanikio makubwa hasa kama yanayotokea katika nchi za wenzetu.Utanda wazi unawafanya wawe na matumaini ya kufika sehemu ya kutia moyo kiuchumi na mandeleo ya nchi yao. Wengi wanapenda kuona wana ondokana na foleni zisizo isha, wangependa uwepo wa train za kasi kutoka Dar es salaam hadi Mwanza. Wanapenda kuona nchii hii inakuwa nashirika lake la ndege..pia wanapenda waone elimu inayotolewa iwe ni elimu bora inayo mjenga kijana kuweza kujitolea.hakika matarajio yao ni makubwa mno..Lakini itabaki kuwa matarajio ya vijana hawa na mafanikio ya kiuchumi kwa ajili ya kizazi hichi si hasa ya kutia moyo..yana katisha tamaa na vijana wana punguza uzalendo,wanaingia katika biashara hasi na wamekataa tamaa.
CHANGE.
Tanzania inahitaji mabadiliko ya uongozi –Inahitaji Kiongozi kijana anaye elewa nini wananchi wa sasa wanahitaji.Tunahitaji kiongozi mwenye wivu wa maendeleo mwenye kuona mbali na kuanzas afari ya kuipeka Tanzania katika maendeleo ya kisasa. Kiongozi atae hakikisha vijana wanapata elimu bora kabisa ambayo itawawezesha wenyewe kujiajiri.Kiongozi mzalendo ataeweka maslahi ya nchi mbele kuliko malsahi ya CorporateEntity za nje ambazo lengo lao ni kuzinyonya nchi hizi.
Tumepita miaka 53 sasa ya uhuru viongozi wengi ni wale wale ambao tumetoka nao tangia uhuru na wengine baada ya uhuru lakini mind zao na uwezo wao bado ni wa60’s na 70’s hawa tunawashukuru , wamefanya mengi lakini sasa Taifa linahitaji CHANGE, linahitaji kijana mkakamavu, mwerevu , mzalendo, mwenye uwezo wa kutuvusha hapa tulipo na kutupeleka kuleeeeee...kama alivosema Kikwete leo bungeni.


Viongozi wetu kisiasa

Hali ya kisasa Tanzania kwa ujumla bado ni mabaki ya wakoloni bado sisi ni memba waCommon wealth Jumuiya ya watawaliwa wa Uingereza na ‘Mkubwa’” wetu ni Malkia wa uingereza na akifa ni yoyote katika watoto wa jumba hilo la mfalme.Nchi kama Marekani na Canada –Quebec , Zimbabwe na Gambia walijitoa kwani waliona kuwepo katika Jumuia hii ni sawa ya kuwa chini ya ukoloni mambo leo wa Kifalme waUingereza.

Mifumo ilio wekwa na wakoloni , elimu iliyotolewa viongozi walo tayarishwa kuongoza nchi hizi huru ‘walitekwa kimawazo’ na bado waliendelea kuwa watiifu kwa wakoloni hao. . Wakati wa uhuru,baadhi ya wasomi walijaribu kubadilisha hali hii lakini hawakufanikiwa ama yalitokea mapinduzi ya kijeshi ( nchi nyengine za Kiafrika) au viongozi walijimilikia madaraka na kuweka maslahi yao hivyo wasomi hawa walipata matatizo na watawala. Bado nchi nyingi za kiafrikana Tanzania ikiwamo inategemea sana wale wale walokuwa wakoloni wa mataifa haya baada ya zaidi ya miaka 50 ya kuwa huru.Tatizo hili lipo zaidi Afrika. Nchi zote nyengine nje ya Afrika mfano Malaysia, Indonesia,Thailand,Philipines,Singapore, India, UAE, Oman, zimepiga hatua kubwa za maendeleo kama nchi huru zilizopata uhuru wao miaka sawa na sisi Tanzania.
Wakati Lee Kuan Yew Waziri mkuu wa kwanza Singapore akiibadilisha nchi hio kutoka kisiwa cha wavuvi hadi kuwa moja ya nchi zilizo endelea na viwanda sisi tulibaki wategemezi na moja ya nchi masikini duniani.
Tujiulize kwa nini ? Nchii yetu ina kila kitu
· Watu
· Rasilimali
· Amani
Jee tumekwama wapi ? bila ya shaka tatizo kubwa lipo kwenye
· Elimu duni
· Uongozi wa kikale
· Umimi
· Uzalendo kubaki ni rangi
· Uoni mfupi
Jee nini cha kufanya...
CCM ni chama pekee ambacho kama Taasisi kime jijenga na kinaweza kuamua kuwa sasa Watanzania wanataka Kiongozi Mpya ,Kijana , Msomi mwenye uwezo wa kutuvusha hapa katika lindi la mkwamo wamaendeleo...lakini lazima CCM ifumbe macho katika kuamua, bado masalia ya za kale wapo na wana nguvu za kifedha na support ya watu ambao wana hakikisha status quo inaendelea ili wafaidi keki ya Taifa pekee yao bila ya kujali maendeleo ya Nchi ..
Jee ni nani katika wagombea wa CCM ambaye ndie atakua Lee Kuan Yew wetu ?Bila ya shaka yoyote..ni JANUARY MAKAMBA
Sifa na uwezo anao.Kama kweli tunataka kuondokana na majungu na siasa za 60 na 70 baso January ndio suluhisho.


 

Utatu

JF-Expert Member
Dec 31, 2008
436
250
Mwizi wa mitihani ya Sekondari anagombea Uraisi, ni CCM tu huko?

Mwizi wa hela za miradi anataka kugombea uraisi. Mnamlinganisha na Obama, si alipigwa marufuku kufika Marekani huyu, kwa sababu hiyo?

toeni njaa zenu, hasafishiki huyu mtu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom