Turudi Kwenye Ujamaa : At least Kwenye Kilimo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Turudi Kwenye Ujamaa : At least Kwenye Kilimo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by VoiceOfReason, Oct 12, 2011.

 1. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Hivi kuna faida gani ya kubinafsisha mahekari na mahekari ya ardhi..? Hivi kwa sasa tatizo ni kwamba hatuwezi kuzalisha (wakulima hawawezi kuzalisha) au hakuna miundo mbinu ya kuweza kufikisha mali sokoni kutoka vijijini.

  Kwanini tulete wawekezaji kutoka India na pengine na kuwapa ardhi yetu yenye rutuba ?, Hivi ni kiasi gani cha kuwekeza kinachotakiwa ambacho serikali inashindwa kukitoa..?

  Nadhani ufike muda tusipende shortcuts…, tutengeneze miundombinu mpaka vijijini, baada ya hapo Tufufue vyama vya USHIRIKA. Ni kweli kabisa corporation kama tano tu zinaweza kulisha Tanzania na Africa Mashariki nzima, hivyo basi kwanini hizo corporations wawe wahindi na wachina na visiwe vyama vya ushirika vya sehemu husika.

  Kuna wazee wengi tu ambao sasa wanamaisha bora sababu ya kusomeshwa na hivi vyama vya ushirika., miji kama Kilimanjaro na Kagera ilistawi sana sababu ya hivi vyama vya ushirika..

  Nadhani ufike wakati kwamba ardhi yote iwe mali ya jamii hekari nyingi na nzuri na zenye rutuba vipewe vyama vya ushirika ambavyo vitafanya mpaka processing kwa faida ya jamii inayozunguka mahali pale na kuongeza ajira kwa sehemu husika…, Individuals wanaweza wakawa na small portions za kulima high value products kama viungo, maua na mboga mboga, lakini mifugo, nafaka na mazao ya biashara yanahitaji high investments (na sababu faida ni kubwa, hii faida iwe shared na jamii husika)

  Tuna Kila Kitu.., Ardhi, Wataalamu (Kutoka SUA), na Rutuba ya Kutosha, Kinachotakiwa ni Mashine za kisasa na vision kuhusu kesho…, tusipoangalia tutakuwa tunarudi kwenye Ubeberu ambapo wananchi wetu watakuwa wanaona mazao mazuri kwa mbali ila uwezo wa kuyapata hawana, na kazi zitakazobakia kwa ndugu zetu ni kufagia ofisi za hizi corporations, kumbuka pia hizi corporations zikija kutoka nje hata mkulima wa kawaida hatashindwa ku-compete.., Njia pekee ya kuwa part ya huu utajiri ni vyama vya Ushirika….(Ardhi yote kwa manufaa ya jamii nzima)
   
 2. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Ili hayo yatendeke lazima uwe na wenye maono hayo na watakaotekeleza hayo na mwisho watakao simamia hayo.Kilimo kwa watawala wetu sio priorty ila ni kivuli kuwa kuwa tuna kilimo.Anyway kuomba Mungu atushushie Wataawala wenye maono [Visioni] ma Mikakati [Mission] ya kukiimarisha kilimo ambapo hata haya kuwa maisha magumu ingekuwa hadithi kwa kuwa Vyakula tungekuwa navyo kwa wingi.
   
 3. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Mkuu vyama vya ushirika vilikuwepo na vilikuwa na nguvu sana watu wakaviua..!!!, Kilimo ambacho maji yenyewe hayapo mbali, na tunaweza kufanya water harvesting na kujenga mabwawa.., kwakweli hatuhitaji mtu mmoja awe kutoka nje au awe kutoka wapi kumiliki hiki kitega uchumi cha taifa...

  Ardhi na kilimo kifanywe kuwa faida ya wananchi wote (tunapoelekea tutakuwa kama Kenya ambapo mjukuu wako hatakuwa hata na ardhi ya kutemea mate...) Ila kama mali itakuwa ni ya ushirika huenda mjuu wako akikosa pesa za kwenda shule chama cha ushirika cha kwenu kikamsomesha
   
 4. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hakika VOR tatizo letu sisi ni uongzoi bora na si vinginevyo,tunaitaji watu [commited] watakawaongoza wananchi kufanya maamuzi magumu ya kukuinua kilimo.Mfano kiongozi au mwananchi atakae hujumu shughuri zozote zile zinazohusu kilimo kama vile wizi wa pembejeo au kubia vyama vya ushirika fedha za miradi yake afungwe serious na kufilisiwa na sio bra bra kama hizi za kuoneana aibu.

  Tufike sehemu tuunde mifumo ya kusimamia haki za mkulima kwa aslimia mia na sio kufurahisha makampuni ya kigeni.Tujitoshereza kwanza kwa kilimo cha mazao ya chakula na kisha toka huko ndio tuangalie uzalishaji wa mazao ya biashara.

  Tuna Ardhi nzuri ya kukisha Africa masharaiki na kati kwa vivyakula vingi tu.Ukianzia Iringa ,Mbeya ,Rukwa, Ruvuma,Shinyanga,Geita,Mwanza,Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Morogoro na mikoa mingineyo.Yote hiyo ni mikoa makini kwa kuzalisha mazo ya chakula kama Mahindi, Maharage, Mtama, Viazi,Mchele, na hata matunda
   
 5. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa mkuu ila naona sasa hivi tatizo haliko kwenye usimamizi peke yake hata hizo plan na core objectives hazifai kabisa...!!

  Ni ukweli usiopingika kwamba kilimo cha kisasa na kilimo kikubwa hata huko marekani ni Makampuni machache ndio yanayolisha watu wote (yaani wanazalisha effectively and cheaply).., hivyo basi utaona kwamba hata huku kumwambia kila mtu alime kidogo kidogo vi-hekari vyake vichache kwa hizo pembejeo zilizopitwa na wakati, na akishalima unamchagulia auze wapi au anashindwa kuuza au wafanyabiashara wanamnyonya kweli hayafai)... Na utaona kwamba kilimo kikubwa kinahitaji investment kubwa ambayo mtu wa kawaida hawezi kufanya peke yake na kusimamia ipasavyo..., Hivyo basi tufanye nini..?

  Badala ya kumuita tajiri mmoja (au wachache kutoka nje ya nchi na kuwapa ardhi yetu safi..) kwanini tusianzishe vyama vya ushirika ambavyo core objectives zake itakuwa sio profit driven bali ni kusaidia jamii ? (kuhakikisha inatoa ajira, mikopo ya elimu hata kujenga shule na kutoa afya..?)

  Kwahiyo hapo utaona kutakuwa na sharing of wealthy kuliko kinachotokea sasa au kitakachotokea ni wananchi kuwa na hasira na wawekezaji na badala ya kuwapa wawekezaji sehemu za mbali ambazo hazina rutuba tunawapa nzuri ili wananchi wazidi kwenda pasipofaa
   
 6. F

  Froida JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Tumeweza kujirisha kwa jembe la mkono mpaka tukawa na the big four ,hakuna sababu hao michwa chama cha magamba wanalo jambo si wakuwaendekeza hao
   
 7. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #7
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,182
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  Ili hayo yafanyike tunahitaji watu wenye utasshi kweli
  Watu wanaohubiri kilimo kutoka mioyoni mwao na kukitekeleza na sio wanaohubiri kilimo huku mioyoni mwao wakiwa waaaangalia ile budget iliyotengwa kwa ajili hiyo ni kiasi gani na fungu lao ni kiasi gani
  Tuwe na watu ambao kweli wanakiona kilimo kama mkombozi wa wananchi wengi ambao wako vijijini na wanaoangalia matatizo ya kilimo ni yapi na yanatatuliwaje na matatizo gani wkanayo wakulima
  Maana hii biashara ya kuuziwa pembejeo ambazo zinaua ardhi au mazao yananunuliwa na mizani mbovu au wakulima wanapelekewa mbegu zilizoharibika usitegemee kuna uhakika wa kufufua kilimo kwa uhakika
   
 8. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #8
  Oct 12, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Mkuu haya ndio yanayofanyika sasa kwa system za sasa.., ila hivi vyama vya ushirika vitasimamia yote hayo kuanzia kilimo cha mashamba makubwa, kwa mbinu za kisasa, kuprocess vyakula na kuvifanya finished products, kufanya marketing ya nguvu kuhakikisha products zinauzwa nje na kipato kinakuwa kwenye mfuko wa kusaidia jamii husika..(vile vile hivi vyama vitaleta ajira kwa watu wanaozunguka eneo husika )

  Sababu mkuu Blue Print ya sasa ni kuleta mtu kutoka nje ili aje afanye ambayo tunaweza kufanya lakini tofauti ni kwamba yeye profit kubwa ataondoka nayo wakati vyama vya ushirika ni kwamba vitaigawanya profit kwa wananchi husika...
   
 9. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #9
  Oct 12, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Tena tunapoelekea sasa ni watu kupigana mapanga kwa kugombania ardhi na watu kukosa hata mahali pa kuzika majivu yako...; kweli we are sitting on a time bomb
   
 10. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #10
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,182
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  Mkuu tatizo wahubiri wa hizi sera wanahubiri maneno tuu ila sio watendaji
  Wanahubiri kitu ambacho kukitelekelza ni uwongo
  Wako kwa ajili ya benefit zao na sio za wale wanaowahubiria
  Wako tayari kula jasho la wakulima kwa njia yoyote kuanzia kwenye mbolea au pembejeo mpaka mazao yao
  Wanahakikisha kuwa kuanzia mkulima mpaka consumer wa mwisho wana fungu lao la makato
  hakuna mwenye utashi wa kumuendeleza mkulima wala kuyafanya maisha ya mkulima yawe bora bali ni kumdidimiza kila siku
   
 11. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #11
  Oct 12, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145

  Hakika uliyosema FRo kwenye Red ndio uhalisia wetu sisi,ilipaswa tuwe na viongozi wazalendo wa dhati kutukwamua huko kwa kuona kuwa kilimo ndio mkombozi a Watanzania wengi Maskini walio vijijini kwetu Nchi nzima na siko kuwa na matamko ya kisiasa yasiyo na ukweli dhidi ya Watanzani asilimia 80% wanaoishi vijijini.
  0,,4450469_1,00.jpg Brother huyu akiwezeshwa na Taifa lake Maisha yake na Watanzania wengi yatabadilika na matumaini ya Taifa yenye neema kwa wote itawezekana

  agriculture-253032.jpg
  Kilimo hiki sio kuwa hatuwezi bali bidii za viongozi wetu kuonyesha dila [Vision] na kisha kuwazesha vijana wa kitanzania walisoma kilimo hasa vyuo vyetu vya kilimo kuanzia vyuo vikuu mpaka vyuo vya kawaida,hasa chuo cha Kilimo Sokoine wahitimu wake wakipewa nafsi, muongozo na kuwafanya PATRIOT kwa TAIFA lao watayatenda maajabu haya na njaa yetu na Mataifa mengine ya Africa itakwisha na tutauza kwa kupata faida.

  Cha msingi hapa ni commitment ya viongozi wetu wakuu kwa kuwa mfumo wetu ni ule wa PILAMID.Kwa style ya PILAMID kiongozi mkuu ndie muonyesha dila na mwelekeo kwa Taifa kwa ujumla na wengine wanafuata mpaka ngazi ya chini.Cha msingi ni kuhakikisha kuwa tunapata viongozi wenye dhamila ya UKULIMA wanaoujua umuhimu wa KILIMO sio tu kwa chakula bali kibiashara pia wako tayari kusimamia kilimo cha kufa na kupona.

  Tunaitaji viongozi watakokuja na mikakati ya kisasa ya kuwafanya vijana wapende kilimo kwa hiari ya kujengwa kupenda kilimo.Sio kuwa vijana hawapendi kilimo lakini hawajafundishwa na Taifa kuonyeshwa kuwa kilimo ni swala la msingi na kuwa si lazima ushike jembe kushinda shambani kwa level ya wasomi bali unaweza kujishughurisha na shughuli za kilimo na mtu akaweza kuendesha maisha yake kwa kupitia kilimo.Kilimo kimekuwa ni familia moja moja kuwafundisha watoto wao kuhusu kilimo na watoto walio wengi hawajui umuhimu wa kilimo.
   
 12. M

  Mkandara Verified User

  #12
  Oct 12, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  VoiceofReason,
  Kwanza kabisa, Jina na mada hii vinafungamana kabisa. Unajua inashangaza sana kuona viongozi wetu wakitafuta njia mbadala za ku sustain uchumi wetu nje kabisa ya ukweli uliopo. Ukweli ni upi?

  1. Nchi nzima waajiriwa ktk kazi hawafiki millioni 5 which is 10%, more or less ya population - Hakuna Ajira za kutosha!
  2. Wafanyabiashara wadogo wadogo ni asilimia 10 nyingine - Hawalipi kodi
  3. Wakulima kama walivyokuwa enzi za Nyerere hawafiki asilimia 30 (nakisia) - Ukulima leo ni ghali.
  Hivyo, Wazururaji, wabangaizaji, walanguzi na madalali ni asimilia 50 iliyobakia.

  Sasa maadam serikali yetu inaridhika na hali hii na badala yake kuweka matumaini kutoka nje tukitembeza bakuli la kuomba misaada bila kutayarisha mazingira bora ktk kuboresha hizo nafasi tatu za nguvukazi kwa kutegemea maendeleo yataletwa na wageni basi ndio tumeuza UHURU na UTU wa Mtanzania. Hawa asilimia 50 ya mwisho ambao serikali leo inawasahau kabisa ndio watakuja kuwa mwiba na hakika ikitokea fujo kidogo tu, fikiria yatokee maandamano kama ya Misri hili kundi litafanya nini?.. Fikirieni miji yetu ikija vamiwa na hawa watu waliokosa kabisa msaada na wakafikia kusema LIWALO na LIWE - we have nothing to lose! maanake hawawezi kubadilisha maisha yao tena na hakuna mtu anayewatazama..ITAKUWAJE Yarabi tunusuru na haya ingawa ndio serikali inayajengea mazingira!

  Takwimu zote za kimataifa zinajieleza wazi kwamba nchi zote za kusini mwa jangwa la sahara, leo hii ni maskini kuliko wakati wa Uhuru wa nchi hizo. Hizi takwimu wanazitoa wao wataalam ambao hawaishi tena kutudanganya ya kwamba Tanzania inapiga hatua kimaendeleo kuliko sijui Kenya na kadhalika lakini hawasemi kutoka wapi?..

  Maisha ya mwafirka yanapimwa kama scale ya sokohuria (wallstreet), au presha, hali kuna ukweli mkubwa kwamba Afrika tunazidi kuingia katika umaskini ambao haujawahi kuonekana hata wakati wa mkoloni kwa sababu wananchi waliweza kujitosheleza kwa chakula, leo hata kula ya mtu ni swala la mjadala!. Afrika ilikuwa nchi ya kwanza duniani kwa exports leo hii na umaskini wetu ndio consumer wakubwa wa mali ambazo asili yake zilitoka kwetu iwe ngano, mahindi, matunda spices na kadhalika!...

  Inatisha na inasikitisha sana kuona jinsi tulivyopotea, jinsi Uhuru wetu ulivyokuwa ghali ktk maisha yetu wenyewe na hakika sintashangaa kabisa kama utabiri utaonyesha Tanzania baada ya miaka 20 ijayo itakuwa kama Somalia ya leo...KILIMO ndio mkombozi wa Mtanzania na kama tutaendelea kufikiria kwamba tunaweza kuondoa umaskini kwa kutegemea wawekezaji basi tuwe tayari pia kupoteza AMANI na UTULIVU..
   
 13. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #13
  Oct 12, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Mkuu ni kweli uliyosema na I have said it once, and I will say it again...!!!, Wajukuu zetu watatulaumu sana ujinga ambao ulifanywa na hii generation yetu...!!

  At least waliotangulia walituletea uhuru.., sisi tunachofanya ni kuuza vyote tulivyonavyo na tutawaacha wajukuu zetu bila chochote. Ni kweli mkuu hapa wajukuu zetu watakuwa watumwa na Amani na Utulivu ushaanza kupotea sasa hivi, tumeona pengi tu wakulima na wafugaji wanagombania ardhi..., na huu ni mwanzo.., The Worse is About to Happen
   
 14. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #14
  Oct 12, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Watanzania tuna mawazo mazuri sana tatizo letu kubwa hatuna watu wa kutuongoza, viongozi wetu wanadhani kuwa wana akili kuzidi bwatu wote kumbe ni kinyume chake na sasa wanawaza matumbo yao tu!
   
Loading...