Wakuu habari! Naomba maelekezo, nahitaji kupata turnitin software ya plagiarism checking tafadhali. Naona nyingi zipo vyuoni. Ivi hakuna namna ya mtu binafsi kuwa nayo? Natanguliza shukrani.
Turnitin siyo software ya desktop wala app ya kudownload kama Microsoft Word au Excel. Ni system ya Enterprise ambayo inafanya kazi kwa njia ya cloud subscription.
Hii system imeundwa mahsusi kwa taasisi za elimu vyuo vikuu, colleges, na research institutions. Ndiyo maana utaona access yake iko locked behind institutional agreements, yaani mtu binafsi huwezi kuinunua moja kwa moja.
Kwa lugha nyepesi, Turnitin imejengwa ili iwe sehemu ya mfumo wa chuo: inahusishwa moja kwa moja na LMS (Learning Management Systems) kama Moodle, Blackboard n.k., ambapo mwalimu anapokea assignments na automatically zina-run plagiarism check.
Haipatikani binafsi kwasababu tatu kuu:
1. Licensing Model; Turnitin imeweka Business Model yake kwa taasisi tu, sio individuals, kwa sababu chanzo cha mapato yao ni institutional packages (ambazo gharama zake zinaanzia maelfu ya dola kwa mwaka).
2. Database Sensitivity; Turnitin ina access ya mabilioni ya makala, vitabu, dissertations, na internet sources. Ili kuilinda, hawatoi free API au standalone software mtu aweke kwenye laptop yake.
3. Data Privacy; Mara nyingi vyuo vinapoupload kazi za wanafunzi, zinaingia kwenye database yao (repository). Hii inalinda originality. Sasa kama mtu binafsi angekuwa na access ya bure, ingekuwa rahisi kucheza na data au kuvuja makala za watu.
Kwa kuwa huwezi kupata Turnitin moja kwa moja, unaweza tumia editing firms au consultants. Kuna makampuni (mfano ya academic editing na proofreading) ambayo yamesajiliwa kisheria kutumia Turnitin. Wanaweza kukucharge kati ya USD $5 – $20 kwa plagiarism report moja, kulingana na urefu wa document. Hii ndiyo njia ya haraka zaidi kwa mtu binafsi.
Usidanganywe na websites zinazodai Free Turnitin Check mara nyingi huiba content zako na kuzihifadhi, kisha zinakuwa 100% plagiarized ukija kuzi-check tena.
Kwa mtazamo wangu, njia salama zaidi ni mbili: Kwa kazi za kitaaluma rasmi, tumia Turnitin kupitia chuo chako au kupitia huduma ya wahariri waliolipia.