Turkey coup: Military attempt to seize power from Erdogan. Social Media blocked!

endorgan ameitaka marekani kama wanataka uhusiano wamsalmishe Gulen,uturuki imeifunga airbase wanayotumia wamarekani na hakuna anaeruhusiwa kuingia ama kutoka,kumbuka hapo ndo kuna mabomu ya nuclear yakiwa chini ya wanajeshi wa marekani 1500

Cha msingi hapa ni kuelewa tu kwamba raisi Erdogan ni mhuni tu na mafia kama wengine na is getting away na cronies wake.

Huu ni mpango tu amefanya kujaribu kuhalalisha sera zake za kubinya uhuru wa kutoa maoni.

Si umesikia anataka kubadilisha katiba kurudisha "Death Penalty" kwa wale watu 3000 waliokamatwa hadi leo?

Nataka wote wanyongwe na wapotee.

Hiyo yote ni kutaka kutokomeza wale wote wanaokosoa na kuonekana tishio katika serikali yake.
 
jana ulileta 'ujuvi' hapa,haya kwa nini base ya marekani imefungwa?!
 
Base ya marekani imekatiwa umeme na pia imefungwa,inasemekana jana kuna dege la mafuta wametrack lilitokea hapo base na kuanza kuzijazia mafuta ndege za waasi
 
jana ulileta 'ujuvi' hapa,haya kwa nini base ya marekani imefungwa?!

Airspace ilifungwa na jeshi na serikali ya Uturuki hivyo hakukuwa na uwezekano wa ndege za kivita kuruka angani zaidi ya helikopta ambayo baadae ilikuja kudunguliwa.

Marekani wao automatically wakaheshimu maamuzi ya serikali ya nchi rafiki kusimamisha shughuli zake na ISIS kutokea kwenye kituo chao cha kijeshi cha Incirlik.

Kama umefuatilia posts zangu nimeeleza kwamba kule Malatya ambako ndiko kikosi cha jeshi lililoasi kina mitambo kungekuwa na vurugu angani endapo Marekani ingeendelea na kazi yake ya kushambulia ISIS na Malatya ndipo kuna mpaka na Syria, Iran na Iraq.
 
kwa nini base hyo ya US imekatiwa umeme?
 
b61_0.gif
.
B-61 nuclear bomb stored in iclirk base,Turkey
 
Wakuu wa majeshi wafuatao wameendelea kuwekwa chini ya ulinzi:

General Erdal Ozturk ambae ni mkuu wa kikosi kijulikanacho kama Third Army Corps kilichopo mjini Instabul.

Hiki ni kikosi cha ardhini.

General Adem Huduti ambae ni mkuu wa kikosi cha pili cha jeshi la ardhini la Uturuki.

General Akin Ozturk ambae ni kamanda wa zamani wa jeshi la anga la Uturuki. Huyu generali aliwahi kuongoza jeshi la anga kati ya mwaka 2013-2015 kabla ya kustaafu mwishoni mwa mwaka jana.

Generali Akin Ozuk
 
Base ya marekani imekatiwa umeme na pia imefungwa,inasemekana jana kuna dege la mafuta wametrack lilitokea hapo base na kuanza kuzijazia mafuta ndege za waasi
waasi hawakuw ana ndege walikuwa na Helkopta.na hiyo hiyo Helkopta yaoilitunguliw ana ndege ya kivita ya jeshi la Uturuki.
 
n_101682_1.jpg

Kamanda wa jeshi la majini kwenye bahari ya Mediterranean Admiral Nejat Atilla Demirhan akiwa mikononi mwa maofisa usalama.
 
Arrests after coup attempt in Turkey

Arrests after coup attempt in Turkey.jpg

Surrendered Turkish soldiers who were involved in the coup are beaten by a civilian on Bosphorus bridge in Istanbul, Turkey, July 16, 2016. © Stringer / Reuters

‎Turkeycoup‬ Rais Recep Yayyip Erdogan wa Uturuki amesema serikali inaongoza nchi hiyo na yupo madarakani, baada ya jaribio la mapinduzi ya kijeshi usiku kucha.

Kwenye hotuba yake ya pili aliyoitoa kwenye uwanja wa ndege wa Ataturk mjini Istanbul, rais huyo alisema vikosi vya kijeshi haviongozi wala haviwezi kuongoza Uturuki.

Vyombo vya habari vya Uturuki vimesema wanajeshi kwenye daraja linalounganisha sehemu za Asia na Ulaya za Istanbul juu ya mlango wa bahari wa Bosphorus wamejisalimisha kwa polisi.

Kwenye hotuba yake ya kwanza, rais Ergogan aliapa kukamilisha operesheni dhidi ya watu waliopanga mapinduzi ya kijeshi ili kufanya jeshi liwe safi.

Kaimu mkuu wa jeshi la Uturuki Jenerali mkuu Umit Dundar amesema watu 194, wakiwemo polisi 41, raia 49 na watu 104 walioshiriki kwenye jaribio la mapinduzi ya kijeshi wameuawa na wanajeshi 1,563 wameshikiliwa.

Mwandishi wa habari wa shirika la habari la China Xinhua amesema milio ya risasi bado inasikika katikati ya mjini wa Istanbul, lakini hakuna milipuko wala milio ya ndege angani. Imeripotikiwa kuwa hali ya kawaida imerudi kwenye mji mkuu Ankara.
Wakati huohuo, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Lu Kang amesema China inafuatilia kwa karibu hali inavyoendelea nchini Uturuki na kutarajia utaratibu na utulivu kurudishwa mapema nchini humo.chanzo.
CRI Kiswahili

View attachment 366768 View attachment 366769 View attachment 366770 View attachment 366771 View attachment 366772 View attachment 366773 View attachment 366774
raia 49 na watu 104????
 
Waziri wa ulinzi bwana Fikri Isik leo ametangaza kwamba general Hulus Akar ambae ni mnadhimu mkuu wa majeshi na ambae alikuwa miongoni mwa waliotekwa nyara na wanajeshi, ameokolewa na wote wakiwa hai na salama.

Kulikuwa na operesheni kubwa ya kumwokoa general Akar ambe hushughulika na NATO na mejenerali wengine ambao walikuwa wamefichwa katika kambi ya Akinci iliyoko Ankara.

n_101699_1.jpg

Waziri wa ulinzi bwana Fikri Isik
 
Serikali ya Ugiriki imekubali kuwarudisha Uturuki wanajeshi nane ambao walikimbilia nchini humo na kuomba hifadhi ya ukimbizi.

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki bwana Mevlüt Çavuşoğlu amsema Ankara wametoa ombi rasmi la kuwarudisha wanajeshi hao na Ugiriki wamekubali ombi hilo.

Wanajeshi hao ambao ni sehemu ya wale walipanga jaribio la kimapinduzi nchini Uturuki jana usiku, walitua katika uwanja wa ndege wa Alexandroupolis wakitumia helikopta ya Black Hawk.
 
enjoy uko uliko...

Hapana sio kwamba na-enjoy bali nakupa habari kama zinavyojiri.

Mimi napenda sana habari za frontline.

Nilipokuwa mdogo nilikuwa "inspired" sana na Marehemu mzee Vincent Urio ambae alikuwa mpiga picha wa gazeti la Daily News.

Natafuta kazi Tanzania hata ya freelance ukiona mahala nitupie angalau ka-tip tu, mimi ntamalizia.

lol
 
Back
Top Bottom