Tupendekeze miradi gani mingine mikubwa (yenye manufaa) ya kutekelezwa kwenye kipindi cha pili cha awamu hii ya tano

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
3,262
2,000
Katika kipindi cha kwanza cha awamu hii ya tano tumeshuhudia uwezo mkubwa wa awamu hii kutekeleza miradi mikubwa mikubwa iliyokuwa imeshindikana huko nyuma, tena kwa spidi kali. Mifano ya miradi hii ni kama ifuatavyo:
1. Uhamishaji wa makao makuu ya
nchi kwenda katikati ya nchi.
2.Kuyafanya maporomoko ya mto rufiji (aka Stigler's) kuzalisha umeme wa bei ndogo sana unaotosheleza nchi nzima na kusaza (at least kwa kiwango cha matumizi ya sasa).
3. Ujenzi mkubwa wa njia za usafiri za kisasa kwenye nchi kavu (reli na barabara), majini na angani.
4. Ujenzi mkubwa wa viwanda vya kisasa na miundo mbinu za maji na afya.

Kipindi cha kwanza cha awamu hii kinakaribia kufika mwisho. Jee kuna mirdi mingine mikubwa yenye manufaa kwa taifa letu ambayo ungalipenda itekelezwe katika kipindi cha pili na cha mwisho cha awamu hii ya hapa kazi tu? Mapendekezo yako huenda yakaingizwa kwenye ilani ya uchaguzi mkuu ujao. Mifano ni kama ifuatavyo:
1. Mradi wa chuma cha pua wa Liganga. Manufaa ya mradi huu utatufanya kuachana na matumizi ya vyuma chakavu na kutuwezesha kuwa na viwanda vikubwa kama vile vya kuunda (siyo kuunganisha) magari, matrekta, pikipiki, treni na dhana mbali mbali za kazi hususani mikasi, majembe, shoka, vifaa vya hospitali nk.
Mradi huu wa chuma ulipewa kampuni moja ya Uchina ambayo imekuwa ikizengua. Gharama ya mradi ni $ 3 billion tu sawa na Tsh 6.8 trillion tu ambazo awamu hii imetuonesha tunaweza kutumia fedha zetu wenyewe za ndani.
2.Mradi wa LNG (liquified natural gas). Mradi huu utatuwezesha kuchimba na kusafirisha nje ya nchi (export) matrillion ya gesi tuliyonayo chini ya bahari huko Mtwara na Lindi na kuifanya nchi yetu kuwa nchi tajiri sana. Gharama ya mradi ni $30 billion sawa na kama Tsh 70 trillion! Uwezo huu hatuna kwa sasa. Tunafanyaje? Tuanze kidogokidogo kwa gesi iliyo nje ya bahari hususani ile ya Songosongo? Angalao kwa matumizi ya ndani.
3. Miradi ya umeme wa nuclear/ uranium kwa mfano ule ulioko Mkuju river kule Namtumbo. Gharama ya umeme utokanavyo na vyanzo hivi vya uranium ni kubwa kuliko ule utokanao na maporomoko ya maji. Jee tuachane na miradi ya Uranium kwa sasa na badala yake tuendelee kutafuta maporomoko ya maji mengine makubwa yanayoweza kuzalisha umeme mwingi?

Jaribu na wewe kupendekeza miradi mizito mizito kwa awamu hii kuiangalia utekelezaji wake. Mzee Yusuf Makamba aliwahi kusema " Mzigo mzito tumeurudisha kwa mwenyewe". Tuendelee kumtafutia mizigo mingine tuliyoisahau kabla hajaondoka.
 
white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
4,129
2,000
Nani sasa apendekeze? Kwani hiyo mingine ni akina nani waliipendekeza? Ingekuwa ni mapendekezo yetu wananchi sidhani kama kulingana na matatizo lukuki tuliyonayo tena ya muhimu, tungelipendekeza hayo!! Wakae tu wao, nadhani wako wawili, wapendekeze tena!! Ikibidi la kumtuma hata mtanzania wa kwanza kwenda anga ya juu sawa tu.
 
tinkanyarwele

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
1,513
2,000
Mimi ningependekeza Mh Rais ahakikishe kila Raia wa Tanzania ana Umeme, umeme utaleta vitu vingi sana, ikiwemo maji na kuinua shughuli nyingine za kiuchi katika jamii. Aidha hii litafanya Tanzania liwe taifa la Kwanza Afrika kote kila kijiji, kitongoji na kila kaya kuwa na huduma hii adhimu kwa Waafrika.
 
LIMBOMAMBOMA

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
5,869
2,000
Uboreshaji Wa makazi ya watumishi Wa umma hasa sekta ya elimu tuanzie nyumba za walimu hasa kwa shule za A level tuhakikishe walimu wote wanaishi kwenye nyumba za walimu. Pia na kwenye sekta ya afya pia.
 
Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
14,608
2,000
Katika kipindi cha kwanza cha awamu hii ya tano tumeshuhudia uwezo mkubwa wa awamu hii kutekeleza miradi mikubwa mikubwa iliyokuwa imeshindikana huko nyuma, tena kwa spidi kali. Mifano ya miradi hii ni kama ifuatavyo:
1. Uhamishaji wa makao makuu ya
nchi kwenda katikati ya nchi.
2.Kuyafanya maporomoko ya mto rufiji (aka Stigler's) kuzalisha umeme wa bei ndogo sana unaotosheleza nchi nzima na kusaza (at least kwa kiwango cha matumizi ya sasa).
3. Ujenzi mkubwa wa njia za usafiri za kisasa kwenye nchi kavu (reli na barabara), majini na angani.
4. Ujenzi mkubwa wa viwanda vya kisasa na miundo mbinu za maji na afya.

Kipindi cha kwanza cha awamu hii kinakaribia kufika mwisho. Jee kuna mirdi mingine mikubwa yenye manufaa kwa taifa letu ambayo ungalipenda itekelezwe katika kipindi cha pili na cha mwisho cha awamu hii ya hapa kazi tu? Mapendekezo yako huenda yakaingizwa kwenye ilani ya uchaguzi mkuu ujao. Mifano ni kama ifuatavyo:
1. Mradi wa chuma cha pua wa Liganga. Manufaa ya mradi huu utatufanya kuachana na matumizi ya vyuma chakavu na kutuwezesha kuwa na viwanda vikubwa kama vile vya kuunda (siyo kuunganisha) magari, matrekta, pikipiki, treni na dhana mbali mbali za kazi hususani mikasi, majembe, shoka, vifaa vya hospitali nk.
Mradi huu wa chuma ulipewa kampuni moja ya Uchina ambayo imekuwa ikizengua. Gharama ya mradi ni $ 3 billion tu sawa na Tsh 6.8 trillion tu ambazo awamu hii imetuonesha tunaweza kutumia fedha zetu wenyewe za ndani.
2.Mradi wa LNG (liquified natural gas). Mradi huu utatuwezesha kuchimba na kusafirisha nje ya nchi (export) matrillion ya gesi tuliyonayo chini ya bahari huko Mtwara na Lindi na kuifanya nchi yetu kuwa nchi tajiri sana. Gharama ya mradi ni $30 billion sawa na kama Tsh 70 trillion! Uwezo huu hatuna kwa sasa. Tunafanyaje? Tuanze kidogokidogo kwa gesi iliyo nje ya bahari hususani ile ya Songosongo?
3. Miradi ya umeme wa nuclear/ uranium kwa mfano ule ulioko Mkuju river kule Namtumbo. Gharama ya umeme utokanavyo na vyanzo hivi vya uranium ni kubwa kuliko ule utokanao na maporomoko ya maji. Jee tuachane na miradi ya Uranium kwa sasa na badala yake tuendelee kutafuta maporomoko ya maji mengine makubwa yanayoweza kuzalisha umeme mwingi?

Jaribu na wewe kupendekeza miradi mizito mizito kwa awamu hii kuiangalia utekelezaji wake. Mzee Yusuf Makamba aliwahi kusema " Mzigo mzito tumeurudisha kwa mwenyewe". Tuendelee kumtafutia mizigo mingine tuliyoisahau kabla hajaondoka.
Kwani nani amekuambia atarudi 2020?
 
pinno

JF-Expert Member
Jan 17, 2013
1,216
2,000
Huu ni muhimu sana

Utakuwa mwisho wa magonjwa ya kimbufi kama kipindupindu

Bill &Melinda gates wamefanya utafit wa new innovation ktk hili eneo

Wanatengeneza mrad mkubwa kwenye moja ya nchi za Africa Magharibi

Nadhan lipewe kipaumbele
Miradi mikubwa ya maji taka. Maji choo na majibtaka mengine yajengewe big underground tunnels katoka miji Kama Dar es salaam ambao una water table karibu na ardhi.

Hii biashara ya kuchimba mashimo ya choo Haina nafasi katika dunia inayokuwa kwa kasi
 
Ekuweme

JF-Expert Member
May 28, 2018
1,732
2,000
Hiyo miradi ndiyo inasababisha watumishi wasipate hata increments. Inatosha hiyo hiyo
 
pinno

JF-Expert Member
Jan 17, 2013
1,216
2,000
Nani sasa apendekeze? Kwani hiyo mingine ni akina nani waliipendekeza? Ingekuwa ni mapendekezo yetu wananchi sidhani kama kulingana na matatizo lukuki tuliyonayo tena ya muhimu, tungelipendekeza hayo!! Wakae tu wao, nadhani wako wawili, wapendekeze tena!! Ikibidi la kumtuma hata mtanzania wa kwanza kwenda anga ya juu sawa tu.
Huu ndo ujinga wa vyama vya upinzan Tz

Anachosema mleta mada ni kitu muhimu kwa Watanzania wote

Then mtu mwenye akili timamu kabisa unakoment umbufi hapa

Kama hauna la kusema ungemute tu.

Tatizo la watanzania ni ubinafsi, na kujidharau.

Ubinafsi unaona kwa kuwa ni kama hauusiki moja kwa moja na hii kazi, bas haupo hata tayar kutoa mawazo yako mawil

Kujidharau huku ndo kunaua mawazo ya watanzania.
 
Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
3,262
2,000
Mimi ningependekeza Mh Rais ahakikishe kila Raia wa Tanzania ana Umeme, umeme utaleta vitu vingi sana, ikiwemo maji na kuinua shughuli nyingine za kiuchi katika jamii. Aidha hii litafanya Tanzania liwe taifa la Kwanza Afrika kote kila kijiji, kitongoji na kila kaya kuwa na huduma hii adhimu kwa Waafrika.
Miradi ya hospitali vituo vya afya na zahanati
Haya tayari yanashughulikiwa kwa kasi kubwa katika kipindi hiki cha kwanza. Hivi punde yatakuwa historia - kwamba kulikuwa na miaka ya mgao wa umeme, dawa kutokuwepo kwenye hospitali nk.
 
pinno

JF-Expert Member
Jan 17, 2013
1,216
2,000
Katika kipindi cha kwanza cha awamu hii ya tano tumeshuhudia uwezo mkubwa wa awamu hii kutekeleza miradi mikubwa mikubwa iliyokuwa imeshindikana huko nyuma, tena kwa spidi kali. Mifano ya miradi hii ni kama ifuatavyo:
1. Uhamishaji wa makao makuu ya
nchi kwenda katikati ya nchi.
2.Kuyafanya maporomoko ya mto rufiji (aka Stigler's) kuzalisha umeme wa bei ndogo sana unaotosheleza nchi nzima na kusaza (at least kwa kiwango cha matumizi ya sasa).
3. Ujenzi mkubwa wa njia za usafiri za kisasa kwenye nchi kavu (reli na barabara), majini na angani.
4. Ujenzi mkubwa wa viwanda vya kisasa na miundo mbinu za maji na afya.

Kipindi cha kwanza cha awamu hii kinakaribia kufika mwisho. Jee kuna mirdi mingine mikubwa yenye manufaa kwa taifa letu ambayo ungalipenda itekelezwe katika kipindi cha pili na cha mwisho cha awamu hii ya hapa kazi tu? Mapendekezo yako huenda yakaingizwa kwenye ilani ya uchaguzi mkuu ujao. Mifano ni kama ifuatavyo:
1. Mradi wa chuma cha pua wa Liganga. Manufaa ya mradi huu utatufanya kuachana na matumizi ya vyuma chakavu na kutuwezesha kuwa na viwanda vikubwa kama vile vya kuunda (siyo kuunganisha) magari, matrekta, pikipiki, treni na dhana mbali mbali za kazi hususani mikasi, majembe, shoka, vifaa vya hospitali nk.
Mradi huu wa chuma ulipewa kampuni moja ya Uchina ambayo imekuwa ikizengua. Gharama ya mradi ni $ 3 billion tu sawa na Tsh 6.8 trillion tu ambazo awamu hii imetuonesha tunaweza kutumia fedha zetu wenyewe za ndani.
2.Mradi wa LNG (liquified natural gas). Mradi huu utatuwezesha kuchimba na kusafirisha nje ya nchi (export) matrillion ya gesi tuliyonayo chini ya bahari huko Mtwara na Lindi na kuifanya nchi yetu kuwa nchi tajiri sana. Gharama ya mradi ni $30 billion sawa na kama Tsh 70 trillion! Uwezo huu hatuna kwa sasa. Tunafanyaje? Tuanze kidogokidogo kwa gesi iliyo nje ya bahari hususani ile ya Songosongo?
3. Miradi ya umeme wa nuclear/ uranium kwa mfano ule ulioko Mkuju river kule Namtumbo. Gharama ya umeme utokanavyo na vyanzo hivi vya uranium ni kubwa kuliko ule utokanao na maporomoko ya maji. Jee tuachane na miradi ya Uranium kwa sasa na badala yake tuendelee kutafuta maporomoko ya maji mengine makubwa yanayoweza kuzalisha umeme mwingi?

Jaribu na wewe kupendekeza miradi mizito mizito kwa awamu hii kuiangalia utekelezaji wake. Mzee Yusuf Makamba aliwahi kusema " Mzigo mzito tumeurudisha kwa mwenyewe". Tuendelee kumtafutia mizigo mingine tuliyoisahau kabla hajaondoka.
Nimevutiwa na kazi ya ujenzi wa meli unaoendelea ziwa victoria na maziwa mengine

Uhamiaji wa serikali Dom,

Ujenzi wa SGR

Ununuzi wa Ndege na hata uongezwaji wa hifadhi mpya za wanyama

Ni mirad ambayo kutoka moyoni, ninajivunia kuona inafanywa, nailaumu kura niliyompigiaga "Baby mwenye blich la kikongo" in Roma Voice 2015 na ndo maana katika kulipiza hasira zake mimi naomba establishment isipuuzie maoni ya watu wanaotaka Mh Rais aende had kipindi cha 3.

Wamarekani wanaojifanya wanaijua demokrasia walifanya hivyo wa Roosevelt, wakampa vipindi vinne

Sisi ni nan kumuachia Magufuli awamu mbili.

Nipo tayar kufanya lolote ili mzee baba abaki had awamu ya tatu na nne ikibid, na sikumchagua 2015

Tukirud kwenye mirad
Mrad wa Uranium, Mrad wa chuma na mradi wa gesi kweli ipewe kipaumbele
 
Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
3,262
2,000
Hiyo miradi ndiyo inasababisha watumishi wasipate hata increments. Inatosha hiyo hiyo
Yaani wewe unadhani watanzania wanaolipa kodi watafurahi kodi yao muitafune kwa kujilipa increments na kujiongezea mishahara? Kama vipi acha hiyo kazi, wapo watanzania wengi tu watakaoichukua!
 
Top Bottom