Tupendekeze miradi gani mingine mikubwa (yenye manufaa) ya kutekelezwa kwenye kipindi cha pili cha awamu hii ya tano

Katika kipindi cha kwanza cha awamu hii ya tano tumeshuhudia uwezo mkubwa wa awamu hii kutekeleza miradi mikubwa mikubwa iliyokuwa imeshindikana huko nyuma, tena kwa spidi kali. Mifano ya miradi hii ni kama ifuatavyo:
1. Uhamishaji wa makao makuu ya
nchi kwenda katikati ya nchi.
2.Kuyafanya maporomoko ya mto rufiji (aka Stigler's) kuzalisha umeme wa bei ndogo sana unaotosheleza nchi nzima na kusaza (at least kwa kiwango cha matumizi ya sasa).
3. Ujenzi mkubwa wa njia za usafiri za kisasa kwenye nchi kavu (reli na barabara), majini na angani.
4. Ujenzi mkubwa wa viwanda vya kisasa na miundo mbinu za maji na afya.

Kipindi cha kwanza cha awamu hii kinakaribia kufika mwisho. Jee kuna mirdi mingine mikubwa yenye manufaa kwa taifa letu ambayo ungalipenda itekelezwe katika kipindi cha pili na cha mwisho cha awamu hii ya hapa kazi tu? Mapendekezo yako huenda yakaingizwa kwenye ilani ya uchaguzi mkuu ujao. Mifano ni kama ifuatavyo:
1. Mradi wa chuma cha pua wa Liganga. Manufaa ya mradi huu utatufanya kuachana na matumizi ya vyuma chakavu na kutuwezesha kuwa na viwanda vikubwa kama vile vya kuunda (siyo kuunganisha) magari, matrekta, pikipiki, treni na dhana mbali mbali za kazi hususani mikasi, majembe, shoka, vifaa vya hospitali nk.
Mradi huu wa chuma ulipewa kampuni moja ya Uchina ambayo imekuwa ikizengua. Gharama ya mradi ni $ 3 billion tu sawa na Tsh 6.8 trillion tu ambazo awamu hii imetuonesha tunaweza kutumia fedha zetu wenyewe za ndani.
2.Mradi wa LNG (liquified natural gas). Mradi huu utatuwezesha kuchimba na kusafirisha nje ya nchi (export) matrillion ya gesi tuliyonayo chini ya bahari huko Mtwara na Lindi na kuifanya nchi yetu kuwa nchi tajiri sana. Gharama ya mradi ni $30 billion sawa na kama Tsh 70 trillion! Uwezo huu hatuna kwa sasa. Tunafanyaje? Tuanze kidogokidogo kwa gesi iliyo nje ya bahari hususani ile ya Songosongo? Angalao kwa matumizi ya ndani.
3. Miradi ya umeme wa nuclear/ uranium kwa mfano ule ulioko Mkuju river kule Namtumbo. Gharama ya umeme utokanavyo na vyanzo hivi vya uranium ni kubwa kuliko ule utokanao na maporomoko ya maji. Jee tuachane na miradi ya Uranium kwa sasa na badala yake tuendelee kutafuta maporomoko ya maji mengine makubwa yanayoweza kuzalisha umeme mwingi?

Jaribu na wewe kupendekeza miradi mizito mizito kwa awamu hii kuiangalia utekelezaji wake. Mzee Yusuf Makamba aliwahi kusema " Mzigo mzito tumeurudisha kwa mwenyewe". Tuendelee kumtafutia mizigo mingine tuliyoisahau kabla hajaondoka.
4. SGR ifike Chato
 
Nani sasa apendekeze? Kwani hiyo mingine ni akina nani waliipendekeza? Ingekuwa ni mapendekezo yetu wananchi sidhani kama kulingana na matatizo lukuki tuliyonayo tena ya muhimu, tungelipendekeza hayo!! Wakae tu wao, nadhani wako wawili, wapendekeze tena!! Ikibidi la kumtuma hata mtanzania wa kwanza kwenda anga ya juu sawa tu.

Mbona umeongea kiukali hivyo? Lol
 
Huu ndo ujinga wa vyama vya upinzan Tz

Anachosema mleta mada ni kitu muhimu kwa Watanzania wote

Then mtu mwenye akili timamu kabisa unakoment umbufi hapa

Kama hauna la kusema ungemute tu.

Tatizo la watanzania ni ubinafsi, na kujidharau.

Ubinafsi unaona kwa kuwa ni kama hauusiki moja kwa moja na hii kazi, bas haupo hata tayar kutoa mawazo yako mawil

Kujidharau huku ndo kunaua mawazo ya watanzania.
Hayo ni mawazo yako!! Hapa akili ya mzungu na mwafrika ndio huonekana ni tofauti, kwani uzalendo unatoka wapi? Mtu hafundishwi uzalendo hata siku moja, vipaumbele vya nchi hutoka kwa wananchi na sio kwa kiongozi, shida ya praise team ndio hapo hata hamueleweki, tatizo ni kuwa na akili za kushikiwa.
 
Uboreshaji Wa makazi ya watumishi Wa umma hasa sekta ya elimu tuanzie nyumba za walimu hasa kwa shule za A level tuhakikishe walimu wote wanaishi kwenye nyumba za walimu. Pia na kwenye sekta ya afya pia.

Walimu walipwe mshahara mkubwa sawa na ma judge,madoctors na engineers,,, ita attract watu makini na walimu wanastahili mishahara mizuri kwa kazi ngumu wanayofanya
 
..BUNDUKI zisitumike kushambulia wapinzani.

..badala yake yatumike makombora ya KATYUSHA.
 
Miradi yote inayotekelezwa sasa ikisimamiwa na kukamilika kama ilivyopangwa, itatuweka mahali pazuri pa kuanzisha mingine mingi tu ambayo iko ndani ya mipaka yetu na haijawahi kuchukuliwa kwa uzito wake. Nitataja hapa michache>

1. Baharini bila kugusa maziwa yanayotuzunguka kuna samaki wengi hasa kwenye kina kirefu. Huko tungeweza kuongeza mapato zaidi kwanza kwa kuwekeza katika viwanda vya samaki katika pwani ya bahari ya hindi, na kwa njia hiyo wavuvi wakiishavua samaki wanakuja kuuza mavuno yao kiwandani.

2. Serikali ingejenga meli kubwa ya kuvua samaki kwenye bahari kuu yenye uwezo wa kuchakata mazao ya bahari, na kufungasha wakiwa huko huko baharini kabla ya kuyafikia masoko yetu na yale ya kimataifa. Meli za namna hiyo zipo... ni viwanda vinavyoelea.

3. Serikali ingewekeza katika meli za abiria zenye viwango vya kimataifa zinazoweza kutumika kama hoteli zinazoelea aidha kufanya safari za kitalii kwenye pwani yetu pamoja na mwambao wote wa pwani ya mashariki mwa bara la Afrika. Zanzibar tayari wamejikuna wanapoweza kwa kujenga meli ya abiria na ile ya mafuta, hongera kwao... Serikali ya muungano ingepaswa kufanya zaidi ya hapo.

Itaendelea....
 
Katika kipindi cha kwanza cha awamu hii ya tano tumeshuhudia uwezo mkubwa wa awamu hii kutekeleza miradi mikubwa mikubwa iliyokuwa imeshindikana huko nyuma, tena kwa spidi kali. Mifano ya miradi hii ni kama ifuatavyo:
1. Uhamishaji wa makao makuu ya
nchi kwenda katikati ya nchi.
2.Kuyafanya maporomoko ya mto rufiji (aka Stigler's) kuzalisha umeme wa bei ndogo sana unaotosheleza nchi nzima na kusaza (at least kwa kiwango cha matumizi ya sasa).
3. Ujenzi mkubwa wa njia za usafiri za kisasa kwenye nchi kavu (reli na barabara), majini na angani.
4. Ujenzi mkubwa wa viwanda vya kisasa na miundo mbinu za maji na afya.

Kipindi cha kwanza cha awamu hii kinakaribia kufika mwisho. Jee kuna mirdi mingine mikubwa yenye manufaa kwa taifa letu ambayo ungalipenda itekelezwe katika kipindi cha pili na cha mwisho cha awamu hii ya hapa kazi tu? Mapendekezo yako huenda yakaingizwa kwenye ilani ya uchaguzi mkuu ujao. Mifano ni kama ifuatavyo:
1. Mradi wa chuma cha pua wa Liganga. Manufaa ya mradi huu utatufanya kuachana na matumizi ya vyuma chakavu na kutuwezesha kuwa na viwanda vikubwa kama vile vya kuunda (siyo kuunganisha) magari, matrekta, pikipiki, treni na dhana mbali mbali za kazi hususani mikasi, majembe, shoka, vifaa vya hospitali nk.
Mradi huu wa chuma ulipewa kampuni moja ya Uchina ambayo imekuwa ikizengua. Gharama ya mradi ni $ 3 billion tu sawa na Tsh 6.8 trillion tu ambazo awamu hii imetuonesha tunaweza kutumia fedha zetu wenyewe za ndani.
2.Mradi wa LNG (liquified natural gas). Mradi huu utatuwezesha kuchimba na kusafirisha nje ya nchi (export) matrillion ya gesi tuliyonayo chini ya bahari huko Mtwara na Lindi na kuifanya nchi yetu kuwa nchi tajiri sana. Gharama ya mradi ni $30 billion sawa na kama Tsh 70 trillion! Uwezo huu hatuna kwa sasa. Tunafanyaje? Tuanze kidogokidogo kwa gesi iliyo nje ya bahari hususani ile ya Songosongo? Angalao kwa matumizi ya ndani.
3. Miradi ya umeme wa nuclear/ uranium kwa mfano ule ulioko Mkuju river kule Namtumbo. Gharama ya umeme utokanavyo na vyanzo hivi vya uranium ni kubwa kuliko ule utokanao na maporomoko ya maji. Jee tuachane na miradi ya Uranium kwa sasa na badala yake tuendelee kutafuta maporomoko ya maji mengine makubwa yanayoweza kuzalisha umeme mwingi?

Jaribu na wewe kupendekeza miradi mizito mizito kwa awamu hii kuiangalia utekelezaji wake. Mzee Yusuf Makamba aliwahi kusema " Mzigo mzito tumeurudisha kwa mwenyewe". Tuendelee kumtafutia mizigo mingine tuliyoisahau kabla hajaondoka.
Yeah,mradi mradi wa Chuma na makaa ya mawe ni miradi ya kimkakati. Hapa lazima mradi wa miundombinu kamilifu wa Mtwara Corridor lazima uhuishwe ili kuleta tija. Pia mradi wa LNG kama ulivyosema. Ni mradi mkubwa unaohitaji uwekezaji mkubwa hapo lazima kuwe na PPP approach ikiwa na Win-Win Situation.
Kwa hali ilivyo,lazima tutenge fedha kwa ajili ya njia mbili mbili kutoka Dar hadi Dodoma,hili lina gharama,ila kwa hali halisi ya sasa,hilo haliepukiki. Ni umbali wa Kilometa 458+, hivyo tunahitaji kama Tsh 500bn/-, ila faida yake ni kubwa. Hali ya sasa hairidhishi,inafahamika reli ya mwendokasi ya kiwango cha SGR ipo,ila barabara yenye uwezo mkubwa nayo ina mchango mkubwa sana. Lazima tufikiri kwa kuangalia miaka 20 ijayo.
Lakini uwezeshaji unahitajika kwa mazao makuu ya biashara ili kuongeza wigo wa fedha za kigeni,bila kusahau madini.
Mkazo pia uwe kwenye elimu ya kati ya ufundi,ni eneo muhimu sana hili kuwekeza.
 
Pendekezo lako zuri sana. Miradi mikubwa ya umwagiliaji itatuwezesha kuwa na uhakika wa chakula cha kutosha na kuuza nje pamoja na mazao mengine. Inasikitisha kuona nchi kama Misiri ambayo iko jangwani inatupita kwa mbali katika uzalishaji wa mazao ya kilimo.

Mkuu naomba nijikite kwenye uzi wako namba moja. Unapotoa uzi wako na ukadhani una hoja ya msingi ni vyema uangalie ukweli zaidi. Uzi wako unataka mapendekezo ya miradi mikubwa. Kwangu mimi na wengine nadhani mradi mkubwa unaanzia 500b fedha za kitanzania. Katika miradi iliyozidi 500b ndani ya hii miaka minne kati ya mitano ya mwanzo ni​
  1. unanunuzi wa ndege ambao ni 1t+​
  2. Ujenzi wa stiegler gorge 6.5t+ huenda ikazidi.
  3. Ujenzi wa reli ni 7.5t+ kwa matarajio ya mwanzo, huenda ukazidi iwapo utakamilika
Katika miradi hiyo ukiacha ndege zinazokuja kwa PC's miradi mingine miwili mikubwa ambayo ndio ya fedha nyingi haujakamilika na haiwezi kukamilika ndani ya hii miaka mitano ya mwanzo ya utawala wake. Hilo la kuhamia Dodoma mpaka sasa liko 50/50 na la kisiasa zaidi kwani bado halijakamilika.

Iwapo Magufuli atakaa madarakani miaka 6 ijayo ambapo itakuwa mwisho wake kikatiba, hatakuwa na uwezo tena wa kutekeleza mradi wowote utakaozidi 2t au hata kufikia hiyo 2t. Miradi pekee atakayoweza kutekeleza ni ya 500b- tena kwa mikopo.

Kwanini nakuambia hivyo, Magufuli na serikali yake ya awamu hii namfananisha na timu iliyocheza kwa nguvu zote dk 45 za mwanzo, na ikasahau kuna kipindi cha pili cha dk 45. Miradi ile mikubwa wa umeme wa maji na reli iwapo itaisha huenda ni 2022 na sio chini ya hapo. Wakati huo Magufuli atakuwa ameuchoka urais kwani hana cha kwenda kuonyesha tena, na wakati huo joto litakuwa linapanda ndani ya chama chake kusaka mrithi, labda kama ana mpango wa kujiongezea muda wa kukaa madarakani.

Kikwazo chake kwenye miradi mikubwa inayozidi 1t itakuwa, miradi hii mikubwa ya sasa itakuwa haijakamilika na ndio atakuwa anapambana kuimaliza. Mzigo wa kulipa madeni ya pesa anazokopa kwa sasa itakuwa uko shingoni, huku miradi anayojenga sasa ikiwa haijaanza kurudisha alichokopa. Kwa bahati mbaya serikali hii inahubiri kwamba miradi hii ni ya fedha za ndani, lakini ukweli unakataana na kasi ya deni la taifa. Miradi yake mingi ukiacha wa ndege na meli mingine yote ni kama huduma yaani barabara, maji na afya, hivyo ulipaji wake ni wa muda mrefu hasa ukizingatia tuna viwanda vichache na kilimo duni. Hapo sijataja changamoto nyingine zinazoweza kujitokeza zilizo nje ya uwezo wake kiuchumi, kijamii kama majanga ya njaa, bei ya mafuta kupanda, soko la dunia kuyumba nk. Ushauri wangu kwa sasa,amalize hii miradi mikubwa miwili aliyoianza ya above 5t+, kabla ya kuanza kulazimisha miradi mingine mikubwa ambayo nina hakika hataweza kuimaliza, na atakapokuja rais mwingine anaweza kuitelekeza maana nchi hii hatuna vipaombele vya nchi bali vya rais.
 
Uchumi wa viwanda kwa Tanzania must be a process. Lazima uandae mambo yafuatayo kwanza kabla ya kuingia kwenye uchumi wa viwanda (Prelude to Industrialization)

1. Tufanye Mapinduzi ya Kilimo ili kuwa na uhakika wa malighafi za viwanda. Lazima kuwe na mapinduzi katika kilimo kuwe na kilimo cha mashine chenye tija. Agrarian revolution
2. Miundo mbinu kama umeme mwingi sanakila kata na kila kijiji hadi maporini,
3. Reli iunganishe mikoa au kanda zote,
4. Meli na pantoni nyingi. Kuwe na Meli za abiria na mizigo kwenda na kurudi Tanga, Mtwara, lindi na hata huko ziwa Nyasa na Viktoria,
5. Barabara pana na nzuri kila mahali, - barabara za kwenda mikoani zote ziwe double roads and highways
6. Maji safi kila kata na kila kijiji hadi maporini ili watu wasione umuhimu wa kuhamia mijini na waweze kuanzisha miji mipya au kilimo maporini- tusijazane mijini bila tija
7. Huduma za uhakika za afya na usalama kama zahanati, polisi, ambulance na firefighters kila kata na kila kijiji kwa uhakika na ufanisi,
3. Serikali na taasisi zenye nidhamu na misimamo kwaajili ya kuwa regulators and enablers. Serikali inayowapenda nakuwa support wafanya biashara na wawekezaji. Sasa hivi ukidhulumiwa hapa tanzania ni ngumu kupata haki kwa haraka. Hata fair competition commission ni maigizo tu
4. Sheria madhubuti za kuimarisha na kulinda biashara, viwanda. Sasa hivi ukipeleka idea yako Tume ya Sayansi wanakuambia hii mbona kuna mtu alishaleta - kumbe uongo ukiondoka wanaichukua wao
5. Masoko ya uhakika ya mazao yote ya kilimo
6. Ajira ili kua na watu wenye uwezo na uchumi wa kati ambao ndio buyers - purchasing power
7. Watanzania wote wenye biashara zilizodumu zaidi ya miaka 5 wapewe mikopo nafuu na serikali na misamaha ya kodi kwa masharti kua waajiri watu. Seikali isifanye biashara bali iwawezeshe na kuwasaidia wazalendo wenye biashara kukuza na kupanua biashara zao na kuajiri watu wengi. Kila mkoa wafanyabiashara 50 wapewe hizi stimulus package za kama million 200 kila mwaka for 5 years. Hii ndio njia bora ya kuwekeza kwenye uchumi wawatu badala ya vitu

Ukishakua na mambo ya msingi kama hayo ndio unaweza kuingia uchumi wa viwanda
 
Naomba nikuulize mleta mada,kati ya miradi yote uliyoiorodhesha kuna hata mmoja ambao ulipendekezwa achilia mbali kushirikishwa wananchi au hata wale wawakilishi wao pale bungeni ambao ndio wanufaika au waadhirika wakubwa. Sawa na kumwonga kimada gari ukamwaminisha ni lake kwa kumpa funguo wakati kadi original ya gari ina majina yako na umeihifadhi kwenye sandiku lako.
 
Katika kipindi cha kwanza cha awamu hii ya tano tumeshuhudia uwezo mkubwa wa awamu hii kutekeleza miradi mikubwa mikubwa iliyokuwa imeshindikana huko nyuma, tena kwa spidi kali. Mifano ya miradi hii ni kama ifuatavyo:
1. Uhamishaji wa makao makuu ya
nchi kwenda katikati ya nchi.
2.Kuyafanya maporomoko ya mto rufiji (aka Stigler's) kuzalisha umeme wa bei ndogo sana unaotosheleza nchi nzima na kusaza (at least kwa kiwango cha matumizi ya sasa).
3. Ujenzi mkubwa wa njia za usafiri za kisasa kwenye nchi kavu (reli na barabara), majini na angani.
4. Ujenzi mkubwa wa viwanda vya kisasa na miundo mbinu za maji na afya.

Kipindi cha kwanza cha awamu hii kinakaribia kufika mwisho. Jee kuna mirdi mingine mikubwa yenye manufaa kwa taifa letu ambayo ungalipenda itekelezwe katika kipindi cha pili na cha mwisho cha awamu hii ya hapa kazi tu? Mapendekezo yako huenda yakaingizwa kwenye ilani ya uchaguzi mkuu ujao. Mifano ni kama ifuatavyo:
1. Mradi wa chuma cha pua wa Liganga. Manufaa ya mradi huu utatufanya kuachana na matumizi ya vyuma chakavu na kutuwezesha kuwa na viwanda vikubwa kama vile vya kuunda (siyo kuunganisha) magari, matrekta, pikipiki, treni na dhana mbali mbali za kazi hususani mikasi, majembe, shoka, vifaa vya hospitali nk.
Mradi huu wa chuma ulipewa kampuni moja ya Uchina ambayo imekuwa ikizengua. Gharama ya mradi ni $ 3 billion tu sawa na Tsh 6.8 trillion tu ambazo awamu hii imetuonesha tunaweza kutumia fedha zetu wenyewe za ndani.
2.Mradi wa LNG (liquified natural gas). Mradi huu utatuwezesha kuchimba na kusafirisha nje ya nchi (export) matrillion ya gesi tuliyonayo chini ya bahari huko Mtwara na Lindi na kuifanya nchi yetu kuwa nchi tajiri sana. Gharama ya mradi ni $30 billion sawa na kama Tsh 70 trillion! Uwezo huu hatuna kwa sasa. Tunafanyaje? Tuanze kidogokidogo kwa gesi iliyo nje ya bahari hususani ile ya Songosongo? Angalao kwa matumizi ya ndani.
3. Miradi ya umeme wa nuclear/ uranium kwa mfano ule ulioko Mkuju river kule Namtumbo. Gharama ya umeme utokanavyo na vyanzo hivi vya uranium ni kubwa kuliko ule utokanao na maporomoko ya maji. Jee tuachane na miradi ya Uranium kwa sasa na badala yake tuendelee kutafuta maporomoko ya maji mengine makubwa yanayoweza kuzalisha umeme mwingi?

Jaribu na wewe kupendekeza miradi mizito mizito kwa awamu hii kuiangalia utekelezaji wake. Mzee Yusuf Makamba aliwahi kusema " Mzigo mzito tumeurudisha kwa mwenyewe". Tuendelee kumtafutia mizigo mingine tuliyoisahau kabla hajaondoka.
Mawazo mazuri umeyaleta lakini yanahitaji muda ili kupisha ile miradi ya kwanza.

Miradi ya SGR na Stigler's bado iko controversial, lazima tusubiri imalizike kisha tuone kama inalipa kiasi gani (return on Investment). Kumbuka fedha karibu 90% inayo jenga miradi hiyo ni fedha ya mkopo kutoka mabenki ya kimataifa kama WB, Credit Suisse, AfDB na Exim Bank ya China. Conditions za kulipa mikopo huwa ni baada ya kulipa na mradi kuanza kuzalisha.

Hivyo basi mradi kama wa SGR unatarajiwa kumalizika labda 2021 na Stiglers ni 2023, kwa hiyo tutaanza kulipa madeni kwenye kuanzia 2022 na 2024. Tutahitaji angalao mpaka 2025 kuona kama miradi hii inalipa. Kukua kwa deni la Taifa kwa miaka 4 ya awamu ya 5 kwa Tsh 13 Trilioni ni kielelezo kuwa tunakopa sana kwa ajili ya miundombinu. Mwaka 2015 Deni la Taifa likijuwa Tsh 38 Trillion na July 2019 ni Tsh 51 Trilioni.

Lazima tuangalie nchi za wenzetu kama Ethiopia ambao wamewekeza sana kwenye ujenzi wa miundombinu lakini bado wananchi wao wana maisha ya kifukara sana. Ndiyo maana pamoja na kuwa na treni za mjini (metro), SGR na Renaissance Electricity Dam bado vijana wao kwa wingi wanakimbia nchi kwenda Ulaya kupitia bahari ya Mediterranean au kwenda SA kupitia Kenya, Tanzania na Zambia.

Matokeo tunayajua wengi wanakufa kwenye bahari na wengi tunawakamata kwenye malori.

Mawazo ya mtoa mada ni mazuri ila yanahitaji tusubiri hii tuliyoianza tuone inachangia nini kwenye uchumi. Hata kwenye maisha ya kawaida kwa mfano wakati wa kula ukataka kula wali na Ice cream na kahawa na tikiti kwa wakati mmoja huwezi fanikiwa. Maliza moja ndipo uanze jingine.
 
Mkuu naomba nijikite kwenye uzi wako namba moja. Unapotoa uzi wako na ukadhani una hoja ya msingi ni vyema uangalie ukweli zaidi. Uzi wako unataka mapendekezo ya miradi mikubwa. Kwangu mimi na wengine nadhani mradi mkubwa unaanzia 500b fedha za kitanzania. Katika miradi iliyozidi 500b ndani ya hii miaka minne kati ya mitano ya mwanzo ni​
  1. unanunuzi wa ndege ambao ni 1t+​
  2. Ujenzi wa stiegler gorge 6.5t+ huenda ikazidi.
  3. Ujenzi wa reli ni 7.5t+ kwa matarajio ya mwanzo, huenda ukazidi iwapo utakamilika
Katika miradi hiyo ukiacha ndege zinazokuja kwa PC's miradi mingine miwili mikubwa ambayo ndio ya fedha nyingi haujakamilika na haiwezi kukamilika ndani ya hii miaka mitano ya mwanzo ya utawala wake. Hilo la kuhamia Dodoma mpaka sasa liko 50/50 na la kisiasa zaidi kwani bado halijakamilika.

Iwapo Magufuli atakaa madarakani miaka 6 ijayo ambapo itakuwa mwisho wake kikatiba, hatakuwa na uwezo tena wa kutekeleza mradi wowote utakaozidi 2t au hata kufikia hiyo 2t. Miradi pekee atakayoweza kutekeleza ni ya 500b- tena kwa mikopo.

Kwanini nakuambia hivyo, Magufuli na serikali yake ya awamu hii namfananisha na timu iliyocheza kwa nguvu zote dk 45 za mwanzo, na ikasahau kuna kipindi cha pili cha dk 45. Miradi ile mikubwa wa umeme wa maji na reli iwapo itaisha huenda ni 2022 na sio chini ya hapo. Wakati huo Magufuli atakuwa ameuchoka urais kwani hana cha kwenda kuonyesha tena, na wakati huo joto litakuwa linapanda ndani ya chama chake kusaka mrithi, labda kama ana mpango wa kujiongezea muda wa kukaa madarakani.

Kikwazo chake kwenye miradi mikubwa inayozidi 1t itakuwa, miradi hii mikubwa ya sasa itakuwa haijakamilika na ndio atakuwa anapambana kuimaliza. Mzigo wa kulipa madeni ya pesa anazokopa kwa sasa itakuwa uko shingoni, huku miradi anayojenga sasa ikiwa haijaanza kurudisha alichokopa. Kwa bahati mbaya serikali hii inahubiri kwamba miradi hii ni ya fedha za ndani, lakini ukweli unakataana na kasi ya deni la taifa. Miradi yake mingi ukiacha wa ndege na meli mingine yote ni kama huduma yaani barabara, maji na afya, hivyo ulipaji wake ni wa muda mrefu hasa ukizingatia tuna viwanda vichache na kilimo duni. Hapo sijataja changamoto nyingine zinazoweza kujitokeza zilizo nje ya uwezo wake kiuchumi, kijamii kama majanga ya njaa, bei ya mafuta kupanda, soko la dunia kuyumba nk. Ushauri wangu kwa sasa,amalize hii miradi mikubwa miwili aliyoianza ya above 5t+, kabla ya kuanza kulazimisha miradi mingine mikubwa ambayo nina hakika hataweza kuimaliza, na atakapokuja rais mwingine anaweza kuitelekeza maana nchi hii hatuna vipaombele vya nchi bali vya rais.
1. Kumbuka huyu ni mwanasayansi. Mwanasayansi huwa hachoki kufanya uvumbuzi (inventions & discoveries) kwani ndiyo kazi yake. Formula ya kuipeleka nchi yetu kuwa a donor country aliivumbua mapema katika kipindi chake cha kwanza. Formula hiyo ndiyo imewezesha kuyafanya hayo mambo makubwa tunayoyashuhudia. Formula hii anaendelea kuiboresha ili iweze kufanya vizuri zaidi.

2. Kumbuka alipoanza kipindi cha kwanza alikuta Hazina iko tupu. Yaani hata mishahara ya watumishi serikali ilikuwa inakopa benki za biashara! Umeme na maji yalikuwa wa mgao, hospitalini kulikuwa hakuna dawa wala vitendea kazi hususani gloves na kadhalika. Aka brain storm na ku invent formula ambayo ndani ya muda mfupi pesa zikawa zina flow kwa wingi na kwa kasi kubwa ndani ya Hazina na kutovuja. Hadi sasa mabillion ya pesa za nje (USD) yanaingia kila mwezi kwenye akiba yetu ya fedha za nje. Haya yote ndiyo yamewezesha kufanyika hayo tunayoshuhudia ikiwemo hiyo miradi ya SGR na ujenzi wa Nyerere Hydroelectric power. Pesa zake zipo. Hao wakandrasi wa miradi hiyo hata wakiweza kukamilisha hizo kazi leo pesa yao ipo. Ndiyo maana wanafanya kazi mchana na usiku kwani pesa yao ipo.

3. Sasa kipindi hiki cha pili mwanasayansi huyu atakianza Hazina ikiwa imejaa mapesa. Atakianza Hazina ikiwa inaingiza mabillion ya dola kila mwezi bila kuvuja tofauti na alipoanza kipindi cha kwanza. Atakianza kipindi cha pili akiwa na formula iliyoboreshwa na akiwa na uzoefu wa miaka mitano. Sasa kwa akili ya kawaida tu tutegemee kweli hayo uliyoyasema au kinyume chake?

4. Usiwe doubting Thom. Tunategemea miradi mikubwa zaidi katika kipindi hicho cha pili. Usisite kupendekeza.
 
Pendekezo lako zuri sana. Miradi mikubwa ya umwagiliaji itatuwezesha kuwa na uhakika wa chakula cha kutosha na kuuza nje pamoja na mazao mengine. Inasikitisha kuona nchi kama Misiri ambayo iko jangwani inatupita kwa mbali katika uzalishaji wa mazao ya kilimo.
Misri waliwekeza kwanza kwenye Elimu/Teknolojia/ubunifu sisi tumeanzia wapi?
 
Napendekeza barabara za kuonganisha Kata, Wilaya na Mikoa zijengwe kwa kiwango cha lami, zile za kuunganisha vijiji nazo zijengwe kwa kiwango cha lami, pia napendekeza serikali kujenga na kuboresha miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji.
 
Uboreshaji Wa makazi ya watumishi Wa umma hasa sekta ya elimu tuanzie nyumba za walimu hasa kwa shule za A level tuhakikishe walimu wote wanaishi kwenye nyumba za walimu. Pia na kwenye sekta ya afya pia.
Walimu walipwe vizuri wajijengee nyumba zao, na wajinunulie magari yao, siyo sawa kila mtumishi ajengewe nyumba jirani na ofisi yake. Napinga hii idea mpaka mwisho wa dunia.
Na swala la watumishi kujirundika wizarani au Otis za wilaya na mikoa ni ujinga, ya watumishi wizarani ni wengi kuliko idara wnazo zi hudumia, watoke huko wakafanye kazi.
 
Wana siasa waache kutumia majukumu ya serikali kama mtaji wa kisiasa.
Wana siasa waipe serikali majukumu yake, wajitenge na serikali wao wafanye kazi yao ya kuishauri serikali.
 
Back
Top Bottom