Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 4,952
- 4,326
Katika kipindi cha kwanza cha awamu hii ya tano tumeshuhudia uwezo mkubwa wa awamu hii kutekeleza miradi mikubwa mikubwa iliyokuwa imeshindikana huko nyuma, tena kwa spidi kali. Mifano ya miradi hii ni kama ifuatavyo:
1. Uhamishaji wa makao makuu ya
nchi kwenda katikati ya nchi.
2.Kuyafanya maporomoko ya mto rufiji (aka Stigler's) kuzalisha umeme wa bei ndogo sana unaotosheleza nchi nzima na kusaza (at least kwa kiwango cha matumizi ya sasa).
3. Ujenzi mkubwa wa njia za usafiri za kisasa kwenye nchi kavu (reli na barabara), majini na angani.
4. Ujenzi mkubwa wa viwanda vya kisasa na miundo mbinu za maji na afya.
Kipindi cha kwanza cha awamu hii kinakaribia kufika mwisho. Jee kuna mirdi mingine mikubwa yenye manufaa kwa taifa letu ambayo ungalipenda itekelezwe katika kipindi cha pili na cha mwisho cha awamu hii ya hapa kazi tu? Mapendekezo yako huenda yakaingizwa kwenye ilani ya uchaguzi mkuu ujao. Mifano ni kama ifuatavyo:
1. Mradi wa chuma cha pua wa Liganga. Manufaa ya mradi huu utatufanya kuachana na matumizi ya vyuma chakavu na kutuwezesha kuwa na viwanda vikubwa kama vile vya kuunda (siyo kuunganisha) magari, matrekta, pikipiki, treni na dhana mbali mbali za kazi hususani mikasi, majembe, shoka, vifaa vya hospitali nk.
Mradi huu wa chuma ulipewa kampuni moja ya Uchina ambayo imekuwa ikizengua. Gharama ya mradi ni $ 3 billion tu sawa na Tsh 6.8 trillion tu ambazo awamu hii imetuonesha tunaweza kutumia fedha zetu wenyewe za ndani.
2.Mradi wa LNG (liquified natural gas). Mradi huu utatuwezesha kuchimba na kusafirisha nje ya nchi (export) matrillion ya gesi tuliyonayo chini ya bahari huko Mtwara na Lindi na kuifanya nchi yetu kuwa nchi tajiri sana. Gharama ya mradi ni $30 billion sawa na kama Tsh 70 trillion! Uwezo huu hatuna kwa sasa. Tunafanyaje? Tuanze kidogokidogo kwa gesi iliyo nje ya bahari hususani ile ya Songosongo? Angalao kwa matumizi ya ndani.
3. Miradi ya umeme wa nuclear/ uranium kwa mfano ule ulioko Mkuju river kule Namtumbo. Gharama ya umeme utokanavyo na vyanzo hivi vya uranium ni kubwa kuliko ule utokanao na maporomoko ya maji. Jee tuachane na miradi ya Uranium kwa sasa na badala yake tuendelee kutafuta maporomoko ya maji mengine makubwa yanayoweza kuzalisha umeme mwingi?
Jaribu na wewe kupendekeza miradi mizito mizito kwa awamu hii kuiangalia utekelezaji wake. Mzee Yusuf Makamba aliwahi kusema " Mzigo mzito tumeurudisha kwa mwenyewe". Tuendelee kumtafutia mizigo mingine tuliyoisahau kabla hajaondoka.