Tupendekeze miradi gani mingine mikubwa (yenye manufaa) ya kutekelezwa kwenye kipindi cha pili cha awamu hii ya tano

Nimevutiwa na kazi ya ujenzi wa meli unaoendelea ziwa victoria na maziwa mengine

Uhamiaji wa serikali Dom,

Ujenzi wa SGR

Ununuzi wa Ndege na hata uongezwaji wa hifadhi mpya za wanyama

Ni mirad ambayo kutoka moyoni, ninajivunia kuona inafanywa, nailaumu kura niliyompigiaga "Baby mwenye blich la kikongo" in Roma Voice 2015 na ndo maana katika kulipiza hasira zake mimi naomba establishment isipuuzie maoni ya watu wanaotaka Mh Rais aende had kipindi cha 3.

Wamarekani wanaojifanya wanaijua demokrasia walifanya hivyo wa Roosevelt, wakampa vipindi vinne

Sisi ni nan kumuachia Magufuli awamu mbili.

Nipo tayar kufanya lolote ili mzee baba abaki had awamu ya tatu na nne ikibid, na sikumchagua 2015

Tukirud kwenye mirad
Mrad wa Uranium, Mrad wa chuma na mradi wa gesi kweli ipewe kipaumbele
Na unajiona upo sawa kichwani kweli???roosevelt alitawala miaka gani na sasa tupo kwenye miaka ipi?tatizo umeconcentrate kwenye minute things huku ukiacha a bigger picture,ningekuona wa maana saana kuidai katiba mpya ambayo kwayo hayo yote unayoyataka yatatimia tena kwa kasi na ukamilifu badala ya kumuachia mtu mmoja ndo atapanye anavohisi yeye hata kama anatekeleza,how sure are we kama hatupigwi cha juu kwa kizazi hiki kisichopenda kuhoji kinachotawaliwa na watawala wasiopenda kuhoji?
 
Uboreshaji Wa makazi ya watumishi Wa umma hasa sekta ya elimu tuanzie nyumba za walimu hasa kwa shule za A level tuhakikishe walimu wote wanaishi kwenye nyumba za walimu. Pia na kwenye sekta ya afya pia.
Walimu wa A level ndio walimu gani hao,unawatenganishaje na walimu wa O level na Primary!
Onyesha ukomavu
 
Hiyo miradi ndiyo inasababisha watumishi wasipate hata increments. Inatosha hiyo hiyo
Mradi wa kutafuta waliopotea, kwa mfano Ben Saanane, Azory Gwanda. Pia wapatikane wale wasiojulikana waliompiga risasi Tundu Lissu. Hii ni miradi mikubwa kuliko SGR, Stieglers, n.k
 
Tujenge daraja kuunganisha Dar es Salaam na Zanzibar. Halafu tujenge flyover kuunganisha Unguja na Pemba.
 
1. Kumbuka huyu ni mwanasayansi. Mwanasayansi huwa hachoki kufanya uvumbuzi (inventions & discoveries) kwani ndiyo kazi yake. Formula ya kuipeleka nchi yetu kuwa a donor country aliivumbua mapema katika kipindi chake cha kwanza. Formula hiyo ndiyo imewezesha kuyafanya hayo mambo makubwa tunayoyashuhudia. Formula hii anaendelea kuiboresha ili iweze kufanya vizuri zaidi.

2. Kumbuka alipoanza kipindi cha kwanza alikuta Hazina iko tupu. Yaani hata mishahara ya watumishi serikali ilikuwa inakopa benki za biashara! Umeme na maji yalikuwa wa mgao, hospitalini kulikuwa hakuna dawa wala vitendea kazi hususani gloves na kadhalika. Aka brain storm na ku invent formula ambayo ndani ya muda mfupi pesa zikawa zina flow kwa wingi na kwa kasi kubwa ndani ya Hazina na kutovuja. Hadi sasa mabillion ya pesa za nje (USD) yanaingia kila mwezi kwenye akiba yetu ya fedha za nje. Haya yote ndiyo yamewezesha kufanyika hayo tunayoshuhudia ikiwemo hiyo miradi ya SGR na ujenzi wa Nyerere Hydroelectric power. Pesa zake zipo. Hao wakandrasi wa miradi hiyo hata wakiweza kukamilisha hizo kazi leo pesa yao ipo. Ndiyo maana wanafanya kazi mchana na usiku kwani pesa yao ipo.

3. Sasa kipindi hiki cha pili mwanasayansi huyu atakianza Hazina ikiwa imejaa mapesa. Atakianza Hazina ikiwa inaingiza mabillion ya dola kila mwezi bila kuvuja tofauti na alipoanza kipindi cha kwanza. Atakianza kipindi cha pili akiwa na formula iliyoboreshwa na akiwa na uzoefu wa miaka mitano. Sasa kwa akili ya kawaida tu tutegemee kweli hayo uliyoyasema au kinyume chake?

4. Usiwe doubting Thom. Tunategemea miradi mikubwa zaidi katika kipindi hicho cha pili. Usisite kupendekeza.

  1. Magufuli sio mwanasayansi bali chuoni alisoma somo la sayansi, na sasa ni mwanasiasa mkongwe ambaye ni rais wa watanzania. Muda wake mwingi karibu miaka 30 amekuwa akifanya majukumu ya kisiasa kuliko sayansi. Hivyo sio mwanasayansi
  2. Sina hakika kama alivyoingia madarakani alikuta hazina haina kitu, epuka hadithi za vijiweni. Alichofanya baada ya kuingia madarakani, ni kurudisha pesa za serekali zilizokuwa kwenye bank ya biashara na kuziweka BoT, kiongozi yoyote anayejua wajibu wake angefanya hivi. Hiyo miradi mikubwa inafanyika kwa pesa za mikopo kwa matumaini kuwa tutalipa, vinginevyo uniambie deni la taifa kupanda zaidi ya 10t+ linatoka wapi wakati pesa ni zetu?
  3. Kipindi cha pili atakapoanza atakuwa hajamaliza hiyo miradi mikubwa miwili na mzigo wa madeni utakuwa mlangoni. Narudia tena, sioni Magufuli akijenga mradi wowote mkubwa unaozidi 3t+ kwenye awamu yake ya pili kulingana na hali halisi. Siku moja aliahidi kwamba serikali yake itawekeza shilingi 12.5t alipokuwa kwenye hafla ya bank ya TIB, nilisema ile ni uwongo wa wazi kwani hana uwezo wa kupata 12t ndani ya miaka yake 10, iwe fedha za ndani au mikopo, kwani ana miradi miwili mikubwa inayovuka 12t+ ambayo hajaimaliza. Na ukweli wa hayo uko kwenye bajeti ya kilimo, toka aingie madarakani hajawahi kuipa wizara ya kilimo zaidi ya 100b@yr, wala hajawahi kutoa zote.
  4. Acha siasa nyepesi na kudhani humu ndani wote ni wajinga na hatuna uwezo wa kufahamu lolote. Anaweza kuwa na miradi mingi lakini sio mikubwa. Miradi ya chini ya 200b anaiweza, na mradi chini ya hapo sio miradi mkubwa. Ila mingi sana itakayompa sifa ni ya 50b na chini yake. Lakini je ataiacha nchi hii na deni la taifa kubwa kiasi gani, na uwezo wa kama taifa kulilipa utakuwaje, hapo ndio mjadala ungejikita.
NB: aliahidi mpaka mpaka kufikia desemba 2018 angehamia Dodoma, lakini sasa ni septemba 2019 na hajahamia na hakuna dalili. Kukujazia, wakati anakopa kwa fujo alitegemea pia kufika 2020 atakuwa anakusanya mapato ya kodi kupitia bomba la mafuta ya Uganda hapo Tanga. Je bomba la mafuta limefika wapi?
 
Warejeshe pia utawala wa sheria na kuheshimu haki za binadamu kwani maendeleo bila haki ni bure tu.
 
1. Kumbuka huyu ni mwanasayansi. Mwanasayansi huwa hachoki kufanya uvumbuzi (inventions & discoveries) kwani ndiyo kazi yake. Formula ya kuipeleka nchi yetu kuwa a donor country aliivumbua mapema katika kipindi chake cha kwanza. Formula hiyo ndiyo imewezesha kuyafanya hayo mambo makubwa tunayoyashuhudia. Formula hii anaendelea kuiboresha ili iweze kufanya vizuri zaidi.

2. Kumbuka alipoanza kipindi cha kwanza alikuta Hazina iko tupu. Yaani hata mishahara ya watumishi serikali ilikuwa inakopa benki za biashara! Umeme na maji yalikuwa wa mgao, hospitalini kulikuwa hakuna dawa wala vitendea kazi hususani gloves na kadhalika. Aka brain storm na ku invent formula ambayo ndani ya muda mfupi pesa zikawa zina flow kwa wingi na kwa kasi kubwa ndani ya Hazina na kutovuja. Hadi sasa mabillion ya pesa za nje (USD) yanaingia kila mwezi kwenye akiba yetu ya fedha za nje. Haya yote ndiyo yamewezesha kufanyika hayo tunayoshuhudia ikiwemo hiyo miradi ya SGR na ujenzi wa Nyerere Hydroelectric power. Pesa zake zipo. Hao wakandrasi wa miradi hiyo hata wakiweza kukamilisha hizo kazi leo pesa yao ipo. Ndiyo maana wanafanya kazi mchana na usiku kwani pesa yao ipo.

3. Sasa kipindi hiki cha pili mwanasayansi huyu atakianza Hazina ikiwa imejaa mapesa. Atakianza Hazina ikiwa inaingiza mabillion ya dola kila mwezi bila kuvuja tofauti na alipoanza kipindi cha kwanza. Atakianza kipindi cha pili akiwa na formula iliyoboreshwa na akiwa na uzoefu wa miaka mitano. Sasa kwa akili ya kawaida tu tutegemee kweli hayo uliyoyasema au kinyume chake?

4. Usiwe doubting Thom. Tunategemea miradi mikubwa zaidi katika kipindi hicho cha pili. Usisite kupendekeza.
Hizo dola zinazomiminika kwenye akiba ya kigeni kila mwezi zinatokana na biashara gani. Mbona fix nyingi sana.
 
Mkuu naomba nijikite kwenye uzi wako namba moja. Unapotoa uzi wako na ukadhani una hoja ya msingi ni vyema uangalie ukweli zaidi. Uzi wako unataka mapendekezo ya miradi mikubwa. Kwangu mimi na wengine nadhani mradi mkubwa unaanzia 500b fedha za kitanzania. Katika miradi iliyozidi 500b ndani ya hii miaka minne kati ya mitano ya mwanzo ni​

  1. unanunuzi wa ndege ambao ni 1t+​
  2. Ujenzi wa stiegler gorge 6.5t+ huenda ikazidi.
  3. Ujenzi wa reli ni 7.5t+ kwa matarajio ya mwanzo, huenda ukazidi iwapo utakamilika
Katika miradi hiyo ukiacha ndege zinazokuja kwa PC's miradi mingine miwili mikubwa ambayo ndio ya fedha nyingi haujakamilika na haiwezi kukamilika ndani ya hii miaka mitano ya mwanzo ya utawala wake. Hilo la kuhamia Dodoma mpaka sasa liko 50/50 na la kisiasa zaidi kwani bado halijakamilika.

Iwapo Magufuli atakaa madarakani miaka 6 ijayo ambapo itakuwa mwisho wake kikatiba, hatakuwa na uwezo tena wa kutekeleza mradi wowote utakaozidi 2t au hata kufikia hiyo 2t. Miradi pekee atakayoweza kutekeleza ni ya 500b- tena kwa mikopo.

Kwanini nakuambia hivyo, Magufuli na serikali yake ya awamu hii namfananisha na timu iliyocheza kwa nguvu zote dk 45 za mwanzo, na ikasahau kuna kipindi cha pili cha dk 45. Miradi ile mikubwa wa umeme wa maji na reli iwapo itaisha huenda ni 2022 na sio chini ya hapo. Wakati huo Magufuli atakuwa ameuchoka urais kwani hana cha kwenda kuonyesha tena, na wakati huo joto litakuwa linapanda ndani ya chama chake kusaka mrithi, labda kama ana mpango wa kujiongezea muda wa kukaa madarakani.

Kikwazo chake kwenye miradi mikubwa inayozidi 1t itakuwa, miradi hii mikubwa ya sasa itakuwa haijakamilika na ndio atakuwa anapambana kuimaliza. Mzigo wa kulipa madeni ya pesa anazokopa kwa sasa itakuwa uko shingoni, huku miradi anayojenga sasa ikiwa haijaanza kurudisha alichokopa. Kwa bahati mbaya serikali hii inahubiri kwamba miradi hii ni ya fedha za ndani, lakini ukweli unakataana na kasi ya deni la taifa. Miradi yake mingi ukiacha wa ndege na meli mingine yote ni kama huduma yaani barabara, maji na afya, hivyo ulipaji wake ni wa muda mrefu hasa ukizingatia tuna viwanda vichache na kilimo duni. Hapo sijataja changamoto nyingine zinazoweza kujitokeza zilizo nje ya uwezo wake kiuchumi, kijamii kama majanga ya njaa, bei ya mafuta kupanda, soko la dunia kuyumba nk. Ushauri wangu kwa sasa,amalize hii miradi mikubwa miwili aliyoianza ya above 5t+, kabla ya kuanza kulazimisha miradi mingine mikubwa ambayo nina hakika hataweza kuimaliza, na atakapokuja rais mwingine anaweza kuitelekeza maana nchi hii hatuna vipaombele vya nchi bali vya rais.

Umeongea kisomi zaidi kuliko mapraise team.Miradi yote ni nadra kukamilika term hii.Pia siasa ni upepo sio hesabu je asiporudi kipindi cha pili je.Pia sioni return in investment kwa uchumi Wa kijamaa.Mingi ni ya kisiasa ilianzishwa
 
Hizo dola zinazomiminika kwenye akiba ya kigeni kila mwezi zinatokana na biashara gani. Mbona fix nyingi sana.
Unataka kujua hiyo formula aliyoivumbua? Wewe unachojua ni biashara pekee ndiyo huingiza pesa?

Soma hii nakala toka kwa Mtalii wa Kisiasa alivyokuwa akimjibu Zitto leo kudhihilisha pesa inavyomiminika Hazina na kufanya maajabu. Ni pesa yetu. Kumbuka kuwa hata ukikopa pesa, hiyo pesa inakuwa ni pesa yako maana baadaye huyo uliyemkopa utarudisha pesa yake pamoja na riba yake. Huyo mkopeshaji ( awe benki au mtu ye yote) ni mfanya biashara tu na hawezi kukukopesha kama wewe huna uwezo wa kurudisha mkopo wake na riba yake kwenye muda mliyokubaliana. Matajiri ndiyo hukopeshwa na si mafukara. Mafukara hupewa misaada (midogomidogo), hawakopesheki. Nchi tajiri ndizo zinaongoza kwenye kukopa:

Awamu ya tano ina miradi mingi nchi nzima,miradi inayoonekana kwa macho na sio miradi hewa ama ya kitapeli kama miradi tuliyowahi kuisikia siku za nyuma,Miradi mingi ya barabara nchi nzima, meli, vivuko, umeme, maji, afya, utalii, bandari, viwanja vya ndege. Kodi inayokusanywa haifikii hizo gharama za miradi yote hiyo.

Zitto anapaswa kujua kama tunakopa basi pesa inakwenda mahali sahihi katika miradi hiyo na si vinginevyo,Zitto alipaswa kuja na hoja kama takwimu za deni kuongezeka zimesababishwa na wizi,ufisadi au matumizi mabaya na sio kuja na takwimu za deni linalojenga miradi mbalimbali na kusema deni ni kubwa kuliko deni la Awamu ya nne,huu ni ujinga.

Nimuulize ndugu Zitto,kwani awamu ya 4 zilifanyika shughuli gani za kiuchumi zinazoonekana kwa macho haya ya mwili?!!......mbona ilikopa fedha nyingi sana!!!!

Zitto unasema zile barabara ambazo kila leo tunamkweza Magufuli zilijengwa awamu ya nne,lakini Awamu hii ya tano imeenda mbali kuzitanua na kujenga barabara nane,

Zitto unasema Pesa ambazo zilizojenga daraja la Kigamboni zilitoka awamu ya nne,lakini Awamu ya tano inajenga daraja la baharini la Surrender na daraja la Kigongo,Busisi katika Ziwa Victoria lenye urefu wa zaidi ya Kilomita tatu na nusu,Unasema UDOM ilijengwa awamu ya nne,lakini umeona mifuko ya pensheni ya Uzeeni ilivyoyumba hata kuanzisha kikokotoo kipya!?

Ni sawa kabisa Awamu ya nne ili-invest kwenye social services lakini Awamu hii ya tano ina-invest kwenye miradi mikubwa ambayo nimeitaja.

Zitto unasema Awamu ya tano imejenga Zahanati 300 nchi nzima,Unasema tukizichanganya zote pamoja zinaweza kufikia gharama za hospitali moja ya Mloganzila.

Zitto unasema Awamu ya tano imetumia zaidi ya Trilioni moja kununua ndege wakati Awamu ya nne ilitumia zaidi ya trilioni moja kujenga chuo kikuu cha Udom,Ni sawa kabisa lakini wanafunzi wanaomaliza Udom wangeenda kufanya kazi wapi!?

Awamu ya tano imeamua kufufua mashirika ya Atcl na Ttcl ili kurejesha ajira,kurejea kwa Atcl kuna hitaji iwe na ndege zaidi ya thelathini ili kukidhi soko na sasa tayari tuna ndege 11 nane tayari zinafanya biashara na zinaleta faida kubwa na tatu zinamaliziwa kutengenezwa kiwandani.

Zitto unasema Awamu ya tano haijapandisha Mshahara wala hakuna ajira ila deni limeongezeka,Awamu ya tano imejitahidi sana kulipa malimbikizo ya Watumishi yaliyotokana na Awamu ya tatu na Awamu ya nne,

Hivyo basi Awamu ya tano imetumia gharama nyingi kusawazisha makosa ya Awamu ya nne na kulipa malimbikizo na madai ya Awamu za nyuma,tunatumaini baada ya hapo Taifa litatembea kwa miguu yake na kupiga hatua kubwa mbele.

Zitto unasema Terminal three ni mradi wa Awamu ya nne lakini ahujui mradi ulisimama 2015 hadi Awamu ya tano ilipofanya tathmini upya,lakini terminal three ni theluthi tu ya miradi mikubwa ya Awamu ya tano,kutaja miradi michache tu,

1.Ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard gauge)

2.Ujenzi wa bomba la mafuta la Uganda ambalo litahusu vile vile upanuzi wa bandari ya Tanga
Ujenzi wa Export Processing Zone ya Kurasini – itakayokuwa mhimili wa biashara kati ya China na Ukanda huu wa Afrika.

3.Kufufuliwa kwa ATCL na TTCL.

4.Ununuzi wa ndege 10 zikiwemo Boeing 3 na Airbus 4.

5.kuhamia Mji Mkuu wa Dodoma.

6.Upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam.

7.Ujenzi wa daraja la kilomita tatu katika Ziwa Victoria.

8.Ujenzi wa Meli nane katika Ziwa Nyasa,Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika.

9.Ujenzi wa Bwawa kubwa la Umeme la Rufiji kwa jina la Mwalimu Nyerere Dam.

10.Mradi wa kuzalisha megawati 240 za umeme wa Kinyerezi II unaoendelea kujengwa.

11.Miradi ya kupanua viwanja vya ndege nchini kwa mfano- Dodoma, na mingine inayoendelea -katika viwanja vya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya n.k.

12.Ujenzi wa maghala ya taifa ya kuhifadhi chakula yenye uwezo wa kuhifadhi tani 350 yatakayojengwa kwa msaada wa Serikali ya Hungary katika sehemu mbalimbali nchini hususan katika mikoa inayozalisha mazao ya nafaka kwa wingi.

13.Ujenzi wa Viwanda kama cha kutengeneza marumaru cha Mkuranga, Pwani ambacho ujenzi wake unaendelea
Kiwanda cha kuzalisha mbolea mkoani Lindi – kinajengwa
Kiwanda cha bidhaa za chuma – mkoani Pwani ambacho kiko mbioni kukamilika.

14. Sambamba na ujenzi wa meli 8, kuna upanuzi wa banadari ya Mwanza, na kuna ujenzi wa meli yenye kubwa ukanda wa A.Mashari na Kati - huko Mwanza (unaendelea).

15. Upanuzi wa viwanja wa ndege mbalimbali hapa nchini.

16. Upanuzi, ujenzi na uboreshwaji wa miundo mbinu mbalimbali ya barabara hapa nchini.

17. Uimarishwaji wa miundombinu na usambazaji wa umeme hapa nchini.

18. Elimu na mikopo kwa vijana wetu, Elimu bora hadi kidato cha 4, mafunzo bure kupitia VETA, etc

19. Ujenzi na ukarabati wavyama hospitali, vituo vya afya na zahanati mbalimbali hapa nchini, uboreshaji wa huduma za afya ikiwa ni pamoja na kuweka vifaa vya kisasa na kuongeza maarifa kwa wataalamu.

20.Interchange kubwa kabisa ya Ubungo.

21.Fly Over ya Mfugale pale Tazara.

22.Daraja la baharini la Surrender.

Kwa hakika vitu ni vingi ila muda ni mchache.

-Nikukumbushe tu Awamu ya tano ilivyoanza 2016.

Hostel za Chuo cha UDSM.
Hostel za Askari Magereza.
Ununuzi wa Ndege 2 (Nyingine 3 zikaja ndani ya Mwaka huo huo wa 2016).
Ujenzi wa Flyover Tazara na Ubungo
Upanuzi wa Airport Mwanza
Upanuzi barabara ya Moroco Dar es Salaam.
Upanuzi wa Kisasa Airport Dar
Kukomesha Rushwa
Kurejesha nidhamu Makazini.

-Na haya yalianza tarehe 12/4/2017;

Uzinduzi ujenzi wa reli kwa ajili ya treni ya Umeme.
Ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba

Kukomesha Watumishi Wenye Feki hivyo kuokoa Mabilioni ya Fedha.

Barabara ya kuunganisha Wilaya za Kibondo kigoma Kaliua huko Tabora.

Miradi Mikubwa ya Maji :

Uwezeshaji Ujenzi Bomba la Mafuta kutoka Hoima mpaka Tanga.

Kwa kweli Awamu ya tano chini ya Rais wetu John Magufuli imefanya makubwa sanaa.
Kila upitapo sasa hivi ni ujenzi unaendelea...Dar es Salaam kila kona Barabara ya Tandale-Sinza- Mawasiliano barabara imejengwa,Mitaa ya Kinondoni hivi ina lami,Ubungo Interchange inajengwa
Madaraja yanajengwa

Upanuzi wa barabara kuu ya Ubungo hadi chalinze unafanywa

Daraja Kilombero miaka yote wapigaji walikuwa wanakula hela za wananchi kuwavusha ila sasa limejengwa

-Flyovers zinajengwa

Miradi ya umeme inajengwa na miradi mingi ni kwa hela za watanzania wenyewe.

Miaka yote maeneo ya Mbezi na kimara walikuwa hawapati maji japo yanapita njia hiyo hiyo lakini sasa maji yamefika mbezi, na bado wanaendelea kutandaza mabomba ili kupeleka maji.

Awali waliokuwa wanakula hela za wananchi ni wenye miradi ya kuuza maji kwa magari. Ila sasa wananchi wamekombolewa.

Utendaji kazi umeimarika, sasa hivi kila mmoja anaona cheo akipewa ni kama kakalia kaa la moto..Yale mambo ya kupiga hela na kukaa ofisini kupiga usingizi yameisha watu ni kazi la sivyo unawajibishwa.

Madawa sasa yanapatikana hospitali, ile hali ya madawa ya hospitali yanapelekwa katika Pharmas binafsi imeisha.

Hospitali sasa za serikali ukienda mgonjwa anajaliwa sio kama ilivyokuwa awali.

Taasisi za serikali wafanyakazi wamekuwa wanawajibika ....hakika nidhamu imeimarika.
Kwa sasa taasisi za serikali zinajiendesha kibiashara na si kihasara kama ilivyokuwa awali, ilikuwa ni ulaji tuu wa hela, upigaji dili, taasisi zinakufa, hakuna gawio kwa serikali, ila sasa zinatoa gawio...Hakika kila kitu ni usimamizi imara, ukicheka na kima utavuna mabua.

Awali watu walikuwa wanaulilia uongozi, hata wasio kuwa na elimu walikuwa wanagombea kupata uongozi, sasa uongozi umekuwa mgumu sababu kama wewe si muwajibikaji una ndoto za kupiga tuu, hupati nafasi, Uongozi umekuwa una hadhi kwa sasa.

Hakika Naisifu Serikali ya CCM ya Awamu ya tano,Namsifu sana Rais wetu John Magufuli.

Nimalizie kwa kusema,Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni,Mungu Mbariki Rais wetu John Magufuli,Mungu ibariki Tanzania.

Nikiishia hapa,Mimi ni,
Msemakweli Chakubanga.
Dar es Salaam.
0755078854.

Kahorogoma akaongezea:
Ukarabati wa shule zote kongwe za serikali, songea, moshi tech, ihungo,bukoba sec, bwiru, nganza, nsumba, chuo cha ualimu patandi, butimba, iringa chuo kikuu.
 
Kama hela ya kukopa ndio wanaihesabu kama nayo ni component ya GDP na kufanya GDP iwe kubwa na ndio eti ionekane kimakosa kuwa uchumi unakuwa kwa 7% then this is very wrong and misleading.

Na ndio maana IMF baada ya kuliona hili wakasema ukweli kuwa uchumi unakuwa kwa 4% tu na sio 7% ambayo economically is not realistic.

Nchi haina uwezo kiuchumi wa kuyamudu hayo madeni na sio muda mrefu ukweli utadhihiri kwani nchi itaanza ku-struggle ku-service hayo madeni kwa sababu moja ya source of revenue waliotegemea sana kama bomba la mafuta toka Uganda ujenzi wake through Tanzania uko mashakani.
 
Unadhani wakopeshaji ni wajinga? Tungalikuwa hatuna uwezo kiuchumi wa kumudu hiyo mikopo hawangalitukopesha. Uwezo huo tunao sana na ndiyo maana wanatukopesha ili wapate faida. Sawa na nchi za ulaya na amerika zinavyokopeshwa. Kukopesha ni biashara. .Awamu hii ya tano haiendi nchi za nje kuomba omba misaada wala mikopo. Hakuna kutembeza kopo kama Matonya. Tofauti kabisa na awamu za awali. Wakopeshaji wanatufuata wenyewe nyumbani tena kwa wingi kutubembeleza watukopeshe au watupe misaada na wengi wao tunawakatalia. Tunakopa au kupokea misaada kwa masharti tunayopenda wenyewe. Takwimu za IMF hazina maana kwetu. Sisi tunasonga mbele. Wenye macho wanaona. IMF wenyewe waliporudi mara ya pili (wakiwa na timu nyingine) na kwenda kujionea kwa macho yao tunavyosonga mbele walibadilisha hiyo takwimu yao na kusomeka 6.7%. Takwimu ya Benki ya Afrika inasomeka 7.5%!
 
Tujenge barabara km 100 pembezoni mwa bahari kwa lengo la kutenga utalii wa bahari , sambamba nakupima viwanja vya ujenzi wa mahoteli ili kukuza utali bahari, na hakika tutachochea ongezeka la fedha za kigeni na ajila
 
Uzi huko poa, wachangiaji kama wa Facebook,
Ndio tatizo=

Akili kubwa:
!) bado atujaekeza kwenye hospitali zetu za rufaa mbaka za halmashauri,
a) vipimo S, scan, ECG, ECHO, MRI, XRAY,
B) maabara za serikali ziwe kubwa sio kama sasa utafikiri umeenda grosary

C, tufanye marekebisho mochwari zetu za kuhifadhia maiti ziwe mbali kidogo, mfano kama ile ya pasmoto mjini Morogoro iko nje kabisa na hospitali
D)mji kama wa Dar pangejengwa sehemu moja, kubwa ina kila kitu, pawe ndio kituo cha kuhifadhia maiti katika jiji la Dar, haijalishi umefia nyumbani, au hospital iwe mloganzira, Muhimbili, temeke, amana au popote pale maiti zinapelekwa hapo kituo kimoja Dar nzima,

E) mpango wa kurekebisha jiji la Dar, likae kwa mpangilio wa jiji sio hivi sasa ni hovyo kama ni mzigo utengwe kabisa,
F) jangwani ni kero pajengwe daraja refu kutoka Magomeni mbaka faya
G) pajengwe daraja la mzunguruko kutoka jangwani kwenda Muhimbili kurudi mkwajuni, kama tumeweza kujenga la salender mbaka Coco atushindwi la mzunguruko pale jangwani yaani ni ju kwa ju
Na wasilisha,,
 
Pamoja na yote yaliyochangiwa napendekeza tuwe na hospitali kama Muhimbili kila mkoa. Watu kutoka pande mablimbali za Africa waje kutibiwa hapa.
 
Unadhani wakopeshaji ni wajinga? Tungalikuwa hatuna uwezo kiuchumi wa kumudu hiyo mikopo hawangalitukopesha. Uwezo huo tunao sana na ndiyo maana wanatukopesha ili wapate faida. Sawa na nchi za ulaya na amerika zinavyokopeshwa. Kukopesha ni biashara. .Awamu hii ya tano haiendi nchi za nje kuomba omba misaada wala mikopo. Hakuna kutembeza kopo kama Matonya. Tofauti kabisa na awamu za awali. Wakopeshaji wanatufuata wenyewe nyumbani tena kwa wingi kutubembeleza watukopeshe au watupe misaada na wengi wao tunawakatalia. Tunakopa au kupokea misaada kwa masharti tunayopenda wenyewe. Takwimu za IMF hazina maana kwetu. Sisi tunasonga mbele. Wenye macho wanaona. IMF wenyewe waliporudi mara ya pili (wakiwa na timu nyingine) na kwenda kujionea kwa macho yao tunavyosonga mbele walibadilisha hiyo takwimu yao na kusomeka 6.7%. Takwimu ya Benki ya Afrika inasomeka 7.5%!
Wewe piga porojo hapo, hata Greeks nao walikuwa na akili kama yako kipindi fulani.
 
Mindsetting inahitajika kwa Watanzania. Wazungu walisha 'set mind' zetu kwamba nchi zetu ni masikini - poor countries aka developing countries aka undeveloped countries. Ukweli ni kwamba wao ndiyo undeveloping countries hadi wamefikia stage ya dume kupanda dume na jike kupanda jike (regession)! Sisi ni matajiri. Si umeona mijitu kama ya kampuni toka Uingereza ya Acasia ilivyosononeka kuiacha nchi yetu baada ya kung'olewa na awamu hii ya tano! Wauza unga wakubwa wameng'olewa na kadhalika. Yaani mengi makubwa yamefanyika katika awamu hii ambayo huko nyuma yalikuwa yametushinda. Ukatae au unune lakini ukweli unabaki pale pale.
 
Hapo unaingiza siasa. Wauza unga wakubwa wamedakwa enzi za JK nao ni Shkuna, Lwitiko, Mwanaidi na Dorine Liyumba.
ACACIA na Barrick ni mtu na mtoto, mwanzo alikuwa anafanya mtoto sasa amekuja baba.
 
Namkubali sana JPM na naunga mkono miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali ya awamu ya tano. Hata hivyo, binafsi siungi mkono suala la kuhamia Dodoma kwa sasa. Mradi wa kuhamia Dom umetumia/ na unaendelea kutumia pesa nyingi san ambazo zingeelekezwa kwa miradi mingine ingefaa zaidi. Nashauri, kwa awamu ijayo, serikali itenge zones za Kilimo. Kila ukanda uwe angalau za zao moja la biashara ambalo linalimwa kwa technolojia ya Kisasa, mathalani watu wa Kusini Wapewe nyenzo na elimu sahihi ya Kilimo cha Kisasa cha Korosho, Kanda ya Ziwa zao la Pamba liboreshwe, Kigoma serikali itenge Maeneo ya kuanzisha Plantations za Kilimo cha Michikichi. Ianzishwe operation ya KILIMO NI MOYO WA VIWANDA ili kuchochea mapinduzi halisi ya Viwanda.
 
Back
Top Bottom