Tupende kusaidia wenzetu

Tupende kusaidia wenzetu

flowers

Member
Joined
Jul 4, 2017
Posts
70
Reaction score
201
Kwenye jamii zetu nyingi Kuna matabaka mbalimbali,Watu wa kati wa juu Na wa chini.Na inatokea tunaishi kwa kuchangamana.
Rai Yangu,inapotokea unakaa Na jirani hajiwezi kabisa Si kwa mavazi ama kwa chakula au chochote msaidie Hata kwa Nguo kuu kuu.Maana kwa kufanya hivyo Utapata thawabu toka kwa Mungu.

Kuna watu mtaani wana hali ngumu,ajabu Unakuta Watu wanatupa vyakula ivyo Nguo havai miaka Na miaka mpaka mende wanatoboa Anaona choyo kumpa jirani yake.Katoto ka jirani Nguo ya Shule imetoboka hasemi Ngoja nipitie kwa Fundi angalau apate kauniform Na ukiangalia Kweli Baba mama wamepigikaa Ba kila wakijitahidi hawapati

Ni vyema kutambua Hata viganja vya mikono havilingani hivyo basi Ni vyema tukasaidiana Kutoa Ni moyo Na Si utajiri.Kutoa Si Lazima uwe nacho kingi Hata kidogo.Chakula unaweza ukamgawia jirani asiyeweza Hata unga kidogo,kamchele,chumvi naye akasogeza Siku.
Toa nenda zako usongoje shukrani.Aliyekupa wewe ndiye aliyemnyima yule.
 
Tunajirimbikizia tu cc wenyewe wakati wenzetu hawana kabisa.... asante kwa kunikumbusha mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom