ngudengude
JF-Expert Member
- Jul 2, 2015
- 1,175
- 466
inachukua mda gani kulipwa pesa iliyobaki?Baada ya kupata taarifa ya haya mabank kufilisiwa niliamua kufatilia.
Kiasi kinacho ongelewa kinatolewa na bima ya amana kupitia bodi ya bima ya amana.
Bima ya amana ni kiasi kilichowekwa kisheria kinacholipwa na mabenki yote nchini kuelekea bodi ya bima ya amana ili kuweza kuwafidia wateja banki inapotangazwa kufilisika...
Sasa sheria ya Bima ya amana inaeleza wazi kuwa kiasi kinacho lipwa na Bima ya amana kisizidi million na nusu.
Hivyo basi kama uliweka laki tano basi utalipwa laki tano yote na bima ya amana.
Kama uliweka million 20 utapewa million moja na nusu na kiasi kilicho baki utalipwa na bank husika baada ya kukusanywa kwa mali na madeni yote ya wateja wa bank na orodha ya madai kupitia utaratibu maalum hivyo hakuna pesa ya mtu inayopotea bank inapo filisika.....
Pia bima ya amana hii ni ya serikali hivyo ni bima tofauti na zingine ambazo bank inaweza kuwa nazo.