Tupeane Taarifa benki zinazosuasua ili tutoe fedha zetu kabla hazijatangazwa mfilisi

Kama unataka usalama wa pesa zako we kaziweke CRDB au NMB, hizi ndio benki zitakazobaki ikiwa zingine zote zitafilisika.
 
Hakuna atakayepoteza hela yake hata kama bank ikifilisika kuna mambo mnachanganya...
Hebu fafanua vizuri unamaanisha nini kusema hivyo?
Watu msimu huu wa kupeleka watoto shule huwa wanajitahidi kuweka vipesa
vyao benki viwasaidie,sasa unapofungia benki na karo zinatakiwa
afu unasema hakuna atakayepoteza fedha zake,hii lugha
inamsaidiaje mtoto kwenda shule?
 
Hebu fafanua vizuri unamaanisha nini kusema hivyo?
Watu msimu huu wa kupeleka watoto shule huwa wanajitahidi kuweka vipesa
vyao benki viwasaidie,sasa unapofungia benki na karo zinatakiwa
afu unasema hakuna atakayepoteza fedha zake,hii lugha
inamsaidiaje mtoto kwenda shule?
Huyo jamaa anapiga siasa kwenye maisha ya watu...
 
Wanaotaja NBC jueni ni benk ya 3 kwa ukubwa wa assets.....
Hata profit wanapata kubwa
 
Huko ACB Jaman bdo hawajafikiwa??
Maana wk iliyopita walikusanya kard wakasema wanataka kutoa kard mpya... Isije ikawa janja janja
 
Baada ya kupata taarifa ya haya mabank kufilisiwa niliamua kufatilia.
Kiasi kinacho ongelewa kinatolewa na bima ya amana kupitia bodi ya bima ya amana.
Bima ya amana ni kiasi kilichowekwa kisheria kinacholipwa na mabenki yote nchini kuelekea bodi ya bima ya amana ili kuweza kuwafidia wateja banki inapotangazwa kufilisika...
Sasa sheria ya Bima ya amana inaeleza wazi kuwa kiasi kinacho lipwa na Bima ya amana kisizidi million na nusu.
Hivyo basi kama uliweka laki tano basi utalipwa laki tano yote na bima ya amana.
Kama uliweka million 20 utapewa million moja na nusu na kiasi kilicho baki utalipwa na bank husika baada ya kukusanywa kwa mali na madeni yote ya wateja wa bank na orodha ya madai kupitia utaratibu maalum hivyo hakuna pesa ya mtu inayopotea bank inapo filisika.....
Pia bima ya amana hii ni ya serikali hivyo ni bima tofauti na zingine ambazo bank inaweza kuwa nazo.
Kwahiyo we unaamini hadi benki inafikia kufilisika hawakufanya jitihada za kukusanya hayo madeni?
 
Huko ACB Jaman bdo hawajafikiwa??
Maana wk iliyopita walikusanya kard wakasema wanataka kutoa kard mpya... Isije ikawa janja janja
Mkuu shituka umeambiwa benki ya uhakika ni crdb na NMB hizo zingine inabidi kuishi mguu nje mguu ndani.
 
Haki za mteja bank inapo filisiwa

Benki inapokua inafilisiwa, Deposit Insurance Board (DIB) ambayo ipo kwa mujibu wa kifungu cha 36 na 37 cha Sheria Na. 5 ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, hufanya utaratibu wa kuwalipa wateja amana zao.

Members wa bodi hiyo ni Gavana wa BOT (Mwenyekiti), Makatibu Wakuu wa Hazina wa Tanzania Bara na Visiwani, na Wajumbe wengine watatu ambao huteuliwa na Waziri wa fedha ambao ni wajuzi na wabobezi k atika masuala ya kibiashara, utaalamu au taaluma na wenye tabia na mwenendo mzuri na uzoefu ktk sekta ya zinazohusiana.

Bodi hutoa malipo ya awali kwa wateja wote ambayo kiwango cha kuanzia huwa Tsh milioni moja na nusu. Hii ni kwa mujibu wa tangazo la Serikali Na. 198 la mwaka 2010.

Kwa wateja ambao kiwango cha amana zao wakati wa ufilisi ni chini ya na hakizidi tshs 1.5m hao watalipwa amana zao zote kulingana na kiasi walichokuwa wameweka.

Kwa wateja ambao kiwango cha amana zao kitakuwa kimezidi 1.5m hawa kwanza watapokea hiyo 1.5m kama malipo ya awali kisha kiasi kilichobakia watalipwa baada ya mali zote za benki kuthaminishwa na kufilisiwa.

Ni wajibu wa yeyote anayeidai benki inayofilisika kuwasilisha maombi ya madai ukiambatanisha ushahidi wa nyaraka kwa hiyo bodi.Ili fedha ziweze kulipwa kutoka kwenye "protected deposit" ya bodi ambayo vyanzo vyake vya fedha hutokana na michango ya kila mwaka kutoka kwenye hayo mabenki nk.

Ikifikia hatua ya liquidation na kuteuliwa kwa mfilisi bodi itachukua au kupokea kiwango kilichozidi kutoka kny assets za benki kilichofidiwa kwa depositors. Hii kiutaalamu tunaiita "subrogation right".

Hivyo kiwango cha 1.5m ni kiwango cha awali na sio kiwango cha mwisho,baada ya kulipwa 1.5m ,unaandika maombi ya madai ukiambatanisha nyaraka zote kwa board ambapo utalipwa pesa zako zote kupitia protected deposits.

Chanzo: Maelezo kutoka Wataalamu wa Fedha/ Uchumi

SIGNATUREReport
Like
Kwanza kabisa sina imani na hizo sarakasi za Deposit board..
 
Kwahiyo we unaamini hadi benki inafikia kufilisika hawakufanya jitihada za kukusanya hayo madeni?
Kama serikali yenyewe imetoa taarifa kuwa watalipwa mil 1.5 halafu yeye anapiga blahablaha.

Naamini angekua mmoja wa waathirika wa kufilisiwa kwa hizo benki sidhani kama angeandika utumbo huo.

Usifanye mchezo wengine mafao yao ya uzeeni walihifadhi huko halafu leo unakuja kuambiwa utapewa hela ya boda boda..
 
Benk ya uhakika ni world bank hiyoo haiwezi filisikaa hamieni hukoo wakuuu hizi zingine wekeni ela za mboga
 
Kumbe kuficha hela kwenye mifuko ya sandarusi na madumu ya maji nimeona umuhimu wake. walioweka pesa kwenye hutu tubenki tusicho macho wala mkia sipati picha hali zao kwa sasa!.
Mimi ni miongoni wa hizi benki uchwara wiki ijayo nimefanya maamuzi ya kuhamia NMB ama crdb sipendi ujinga.....hela yangu naitafuta kwa shida sana.
 
Back
Top Bottom