Tupeane mawazo wapendwa

Maty mpendwa kuna mambo hayavumiliki , me wifi yangu hadi alitaka kufa na ujauzito kwa pressure mume ana nyumba ndogo 3 na zote ni wadada wa mujini na familia ya kiume inajua, mume anarudi manane ya usiku hadi apige round nyumba ndogo zote. Wazaz wanamwambia avumilie. Hamjali kamtelekeza na mtoto wa miaka 4. Hapo kuna uvumilivu tena???
 
Huwa najiuliza mara nyingi lakini nakosa jibu zuri, naomba nipate mawazo tofauti tofauti, inaweza kutusaidia wengi wetu.

Wanandoa wengi hasa wa miaka ya sasa, wakikorofishana korofishana baada ya muda wanachoamua ni tuachane bwana kila mtu ataanza nataka niishi kwa amani, nahitaji furaha mimi maisha yenyewe mafupi haya. Ukute hiyo ndoa baba msomi ana kazi nzuri na mama vile vile ndio balaa, kila mtu anasema usinibabaishe ninaweza kumudu maisha.

Hapo kuna watoto mmezaa, lakini kila mtu utamsikia napenda kuishi kwa amani, ni vipi kuhusu watoto? Je hao hawatakiwi kuishi kwa furaha na amani wakiwa na baba na mama? Hivi hamuwezi kukaa mkazungumza na kuelewana ili mlee watoto pamoja badala yake mnafikiria kuachana?

Hivi kuachana ni suluhisho la matatizo yako? Na je ukiachana na mwenzio ndio kusema hutaki kuoa/kuolewa tena? Na je ukioa/olewa halafu huyo mwingine akawa na matatizo pia pengine kuliko uliyoyakimbia mwanzo utaachana nae pia? Au utavumilia?

Tushirikiane kupeana mawazo wandugu




Sasa hivi kushindana kumekua kwingi, kila mmoja kwenye ndoa anataka kua mbabe. Longi ilikua binti anafundishwa uvumilivu wa kila kitu katika ndoa, sasa hivi mkaka atapata wapi mtu wa kumbabaisha na akababaishika? Kitu kingine ni ile ya wote wawili au mmoja wapo kukosa busara ya kumappreciate mwenzio kwamba hata kama humpendi ana nafasi muhimu ya mme/mke. Guys kwa upande wangu nimepata mume ambae ndio ana kasoro lakini ananiheshim, anajali ndoa yetu na mahitaji ya ndani na nje (hata kama tunasaidiana), anajali na kupenda maendeleo ya watoto wetu - kunapotokea tatizo lazima ni fight mana c kazi ndogo kuanza tena kua katika market ya dating. Na hasa hapa Bongo IT IS HARD FOR MEN TO BE MEN na IT IS HARD FOR A WOMAN TO BE A WIFE.
 
Huyo mwanaume alibadilika ghafla au ndo aliolewa na player akitumaini kumbadilisha?
Na kama alibadilika baada ya kuoa ameshajiuliza ni kwa nini?

Maty mpendwa kuna mambo hayavumiliki , me wifi yangu hadi alitaka kufa na ujauzito kwa pressure mume ana nyumba ndogo 3 na zote ni wadada wa mujini na familia ya kiume inajua, mume anarudi manane ya usiku hadi apige round nyumba ndogo zote. Wazaz wanamwambia avumilie. Hamjali kamtelekeza na mtoto wa miaka 4. Hapo kuna uvumilivu tena???
 
Nnunu nimeshaingia kazini. Nachoweza kusema kuhusu nyumba ndogo si kuwa inarekebisha nyumba kubwa ila inafanya husband arudie vows. Maana nikigundua kuna kimada mziki wake ni lazima urudie maneno yote mazuri ulonambia toka tuna date mpaka unaapa kanisani. Haa. Mwanzo wife anakuwa na hasira, baada ya muda anashukuru nyumba ndogo kwani amefufua mapenzi katika ndoa. Kwa experience yangu wanaume wakibambwa wanarudisha descipline na mapenzi yana double! Na hii si kurekebisha nyumba kubwa ila inamfanya mume nae atie akili. Unafikiri ni rahisi ku divorce mke alokuzalia watoto wanaokufanya nawe uitwe kidume.

Mimi nina experience ya ndugu yangu yaani mume wake alicheat alafu yeye mwenyewe cheater ndo kaita kikao cha wana familia kwani anaogopa ndoa isije vunjika.

Inawezekana mkikaa bila hawa vicheche ku interrupt ndoa yenu ndoa ikawa boring. Hizo ndo challenges zenyewe. Ila sasa kilichoharibu maradhi!


ha ha ahaha nimecheka mpaka machozi ya furaha yamenitoka, ASANTE KWA KUNIONGEZEA UHAI NA AFYA YANGU,,,kumbe sikukosea kukumiss kwenye hii thread nzuri ya MATY....yaani napiga picha kama nakuona unavyojifanya umekasirika sana,kumbe nia yako mume aendelee kukubembeleza zaidi....kubebembelezwa kuna raha bwana asikwambie mtu....na hasa ukibembelezwa na kiumbe kinaitwa mwanaume, raha yake haisimuliki ilivyo nzuri....safi sana nyumba kubwa umeonesha ni jinsi gani unaujua utamu wa kubembelezwa na mume.....lol
 
Mi mwenzangu najivumilia tu milima mabonde mafuriko elninyo nimo tu, mbele kwa mbele huko tutajua


SAFI SANA GAGA, MUNGU AZIDI KUKUZIDISHIA MOYO WA UVUMILIVU.
MANAKE IMEANDIKWA,
TUNAYAWEZA YOTE KATIKA YEYE ATUTIAYE NGUVU.

Ila pia mwambie MUNGU asante kwasababu unakutana na magumu na yanayovumilika...lol
 
ULICHOANDIKA NI KWELI KABISA MATY....siku hizi ndoa ikidumu zaidi ya mwaka bila kuvunjika...ni jambo la kwenda kwenye nyumba ya ibada kutoa sadaka ya shukrani,elimu na pesa walizonazo wanandoa ndo zinazowapa mabichwa na confidence ya kitoto ya kuvunja ndoa zao..bila kukumbuka kuwa walishaweka ahadi ya kuvumiliana kwenye shida na raha hadi kifo kitakapowatenganisha...:angry:
 
Mie kwa kweli uvumilivu siwezi nikishindwa nasepa zangu isiwe tabu ung'ang'anie ya nini ilhali mtu ameshakuchoka?
 
degree ya uvumilivu kwenye ndoa ni ndogo sana kwa maisha ya sasa
ukizingatia wana ndoa wengi wana'jua' haki zao na hakuna anayetaka kujiweka chini
haya yote nadhani yameletwa na utandawazi..na hii kitu equality wanawake tunaililia pia i think inachangia kwa namna moja au nyingine
hakuna mwanamke wa siku hizi anataka kunyenyekea, wote wana/tuna penda kujilinganisha na wanaume..
mbaya zaidi ukikuta mdada kasoma ndo kabisaa hapo ni maswala ya 'nini nini usinichoshe nisikuchoshe nataka amani'..
tofauti na mama zetu walikuwa ni wanyenyekevu wazuri sana na wao pia walikuwa wanaangalia consequences za kuachana kwa watoto
lifestyle imebadilika generation hii ni selfish haiangalii watoto
in a nutshell, anayeweza kuifanya ndoa iendelee kuwepo ni mwanamke, na mwanamke wa sasa si mvumilivu.

Ni mtazamo tu.


Hakika sweetdada umelonga mwanakwetu, hata mimi nilizoea kusikia wanasema Nyumba ni mwanamke.
Na je mwajua kuwa ndoa kwa wingi zimeanza kuvunjika kuanzia miaka ya 80 na kuendelea?! kabla ya hapo mama zetu walikuwa wavumilivu na wanyenyekevu kwa kiwango cha juu sana. Hapa swali ni je akina mama wa sasa waweza kurejea hali hiyo ya zamani?
 
mimi yalinikuta na naapa sitakaa nioe tena hapa duniani,nina 40years old,wanawake wakiwa na kazi na pesa wanakuwa na kiburi ambacho hakuna mwanaume wa kuzuia,na kama unaona mwanamke mwenye pesa anaishi kwenye lindoa la matatizo ujue hapo kuna kitu,labda huyo mwanamama ana kahuruma na watoto,thats all,dunia inabadilika na hii ndio hali halisi:frusty::frusty::frusty::frusty::frusty::frusty:
 
usichoke hiyo ndio reality watu wanavamia ndoa kwa kuangalia vitu vya ajabu ambavyo sio endelevu kama vile pesa, umaarufu, nk so mambo yakiharibika na mapenzi yameisha. kingine hakuna mafunzo ya namna ya kuishi ndani ya familia. wadada wengi wa sasa wanajilemba lakini hawana elimu ya kuishi na familia wanajua ndoa ni ...............tu kumbe kuna mambo mengi ya ziada. Mi naona wazazi inabidi wawaelimishe watoto wao namna ya kuishi na mume/mke.
 
nilidhani lbd ndoa za kilokole zinaweza kuwa na unafuu!!

Hivi juzi tu hata mwezi haujaisha dada mmoja mpiganaji kweli kweli na mwanamaombi aliolewa na kk mmoja mlokole mwenzie, kweli harusi ilikuwa nzuri!! wiki ile niliyofiwa akaja kunipa pole akiwa na mama mmoja mchungaji rafiki yangu, baada ya kuona muda umeenda sana, nilimuuliza nawewe unakesha?? akasema ndio, nikamuuliza shemeji vipi hata kasirika akasema tumeshaachana!! nilishika mdomo.

kumbe nasikia walitengana baada ya week 2 tu!! yule mama mchungaji aliniambia kuwa baada ya tu ya siku 2 za ndoa akaanza kusuluhisha kesi zao mpaka mwisho amechoka.

Nikasema duh!! kwakweli kuna haja ya kuendelea kuwa single mpaka kieleweke!!!


suzy habari yako imenishangaza ,,
mungu atusaidie kuzijenga ndoa zetu katika misingi imara ,pasipo kila mmoja kujiona yeye ndio yeye
 
mimi yalinikuta na naapa sitakaa nioe tena hapa duniani,nina 40years old,wanawake wakiwa na kazi na pesa wanakuwa na kiburi ambacho hakuna mwanaume wa kuzuia,na kama unaona mwanamke mwenye pesa anaishi kwenye lindoa la matatizo ujue hapo kuna kitu,labda huyo mwanamama ana kahuruma na watoto,thats all,dunia inabadilika na hii ndio hali halisi:frusty::frusty::frusty::frusty::frusty::frusty:

pole topthinker naamini umeumbwa uishi kwa amani na furaha ,samaki mmoja kioza sio wote ndugu:amen:
 
The topic is hot...Ndoa yangu bado changa so naobserve na kulearn... Thanx Maty kwa kuanzisha hii thread... Okey, 2endelee...
Usiogope mwali doa zote sio lazima ziwe na matatizo, ila ujue pia kila siku sio jumapili. jiweke imara ili hata kama yakikupata matatizo ujue unakabiliana nayo vipi. Meanwhile enjoy you marriage
 
ha ha ahaha nimecheka mpaka machozi ya furaha yamenitoka, ASANTE KWA KUNIONGEZEA UHAI NA AFYA YANGU,,,kumbe sikukosea kukumiss kwenye hii thread nzuri ya MATY....yaani napiga picha kama nakuona unavyojifanya umekasirika sana,kumbe nia yako mume aendelee kukubembeleza zaidi....kubebembelezwa kuna raha bwana asikwambie mtu....na hasa ukibembelezwa na kiumbe kinaitwa mwanaume, raha yake haisimuliki ilivyo nzuri....safi sana nyumba kubwa umeonesha ni jinsi gani unaujua utamu wa kubembelezwa na mume.....lol

mnaona ni sawa kwasasa may b coz hayajawafika, kupigania ndoa ya mwanaume mwenye kimada sio shughuli ndogo, ombeni yacwafike, coz kuna mawili, mume kashalowea huko au atarudisha fikira nyuma na kujirudi....ni kheri mkiweza kuhimili hiyo mikiki mikiki, kwa wengine tulikaribia kukata tamaa, unamuonea mwanaume kinyaa haswa kila dk unahic limetokea huko, bac hamu nalo huna hata chembe, kuirudisha hali ya kumtamani tena nayo ni shughuli pevu...pweehhh ningekuwa mtawa mie japo ningemic hii mitikicko ya lyfe....lol
 
Dah! mawazo yenu niliyoyapata hapa inaonyesha ndoa ni ngumu sana asee

Maty,hivi kuna mtu alikuchapia eti ndoa
rahisi? lol huyo mkimbie kwa spidi ya tsunami! ndoa shughuli,ndoa inataka moyo.
 
Back
Top Bottom