Tupeane mawazo wapendwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tupeane mawazo wapendwa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Maty, Apr 21, 2011.

 1. Maty

  Maty JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2011
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 2,170
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Huwa najiuliza mara nyingi lakini nakosa jibu zuri, naomba nipate mawazo tofauti tofauti, inaweza kutusaidia wengi wetu.

  Wanandoa wengi hasa wa miaka ya sasa, wakikorofishana korofishana baada ya muda wanachoamua ni tuachane bwana kila mtu ataanza nataka niishi kwa amani, nahitaji furaha mimi maisha yenyewe mafupi haya. Ukute hiyo ndoa baba msomi ana kazi nzuri na mama vile vile ndio balaa, kila mtu anasema usinibabaishe ninaweza kumudu maisha.

  Hapo kuna watoto mmezaa, lakini kila mtu utamsikia napenda kuishi kwa amani, ni vipi kuhusu watoto? Je hao hawatakiwi kuishi kwa furaha na amani wakiwa na baba na mama? Hivi hamuwezi kukaa mkazungumza na kuelewana ili mlee watoto pamoja badala yake mnafikiria kuachana?

  Hivi kuachana ni suluhisho la matatizo yako? Na je ukiachana na mwenzio ndio kusema hutaki kuoa/kuolewa tena? Na je ukioa/olewa halafu huyo mwingine akawa na matatizo pia pengine kuliko uliyoyakimbia mwanzo utaachana nae pia? Au utavumilia?

  Tushirikiane kupeana mawazo wandugu
   
 2. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #2
  Apr 21, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Usipoachana utakuwa na nyumba ndogo
   
 3. bacha

  bacha JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 4,336
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  oooops!!!!!
   
 4. bacha

  bacha JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 4,336
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  mmmh, kazi ipo!!!!!!
   
 5. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #5
  Apr 21, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160

  Tena kubwa si mchezo....................
   
 6. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #6
  Apr 21, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kama umegundua mwenzio sio chaguo lako sahihi mnaachana tu kila abebe chake kuliko kukaa mnasoneneka.
  Maisha mtu inabidi aishi kwa fraha na amani tele sio kuishi kama digi digi.
  Ukiona umepata mme anakula bwibwi na wewe hupendezewi na tabia hizo piga chini tafuta chaguo lako sahihi.
   
 7. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #7
  Apr 21, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Nyumba ndogo inahusika kushape nyumba kubwa kwa taarifa yako.
   
 8. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #8
  Apr 21, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mie naungana na wanotaka kuachana mambo yanapokuwa magumu kwani maisha ya kuteseka c mazuri wakati unaweza kuishi kwa furaha.

  Kuhusu watoto hiyo itakuwa ndio historia yao, but as long as nitataka kuishi maisha yanayo rizisha na wanagu ntajitahidi waishi hivyo.Amen
   
 9. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #9
  Apr 21, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,990
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Siyo suluhisho,nmnazungumza,yanaisha.
   
 10. sweetdada

  sweetdada JF-Expert Member

  #10
  Apr 21, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 540
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  degree ya uvumilivu kwenye ndoa ni ndogo sana kwa maisha ya sasa
  ukizingatia wana ndoa wengi wana'jua' haki zao na hakuna anayetaka kujiweka chini
  haya yote nadhani yameletwa na utandawazi..na hii kitu equality wanawake tunaililia pia i think inachangia kwa namna moja au nyingine
  hakuna mwanamke wa siku hizi anataka kunyenyekea, wote wana/tuna penda kujilinganisha na wanaume..
  mbaya zaidi ukikuta mdada kasoma ndo kabisaa hapo ni maswala ya 'nini nini usinichoshe nisikuchoshe nataka amani'..
  tofauti na mama zetu walikuwa ni wanyenyekevu wazuri sana na wao pia walikuwa wanaangalia consequences za kuachana kwa watoto
  lifestyle imebadilika generation hii ni selfish haiangalii watoto

  in a nutshell, anayeweza kuifanya ndoa iendelee kuwepo ni mwanamke, na mwanamke wa sasa si mvumilivu.

  Ni mtazamo tu.
   
 11. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #11
  Apr 21, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ndoa nyingi za wasomi ndio huwa zina matatizo. Na matatizo mengi kwa kiasi kikubwa huwa yanasababishwa na akina mama, tena kama mama ana elimu kubwa au ana uwezo mkubwa wa kipesa kuliko baba hapo tena ndo balaa. Ule ubaba unakuwa hauna maana kabisa. Mama ndo atataka kutawala nyumba, ukisema hiki jibu lake usinibabaishe na visa kedekede. Jaribu kufanya kautafiti kadogo tu, hata viongozi na wasomi wengi wanawake aidha huwa hawana waume au ndoa zao huwa zina migogoro mikubwa sana.

  Ninayo mifano mingi sana ambayo nimeishuhudia mimi mwenyewe ya wanandoa ambao mama aidha ana uwezo na elimu kubwa kuliko baba au wako sawa. Wengine huwa wanafikia hata hatua ya kulala vitanda tofauti, asubuhi kila mtu anaondoka na gari yake japo wanafanya kazi ofisi moja. Basi ilimradi vurumai.
  Akina mama/dada jirekebisheni (siwatuhumu). Fedha na elimu haviwezi kununua mapenzi.
   
 12. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #12
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  My dear
  Tunarudi kulee
  je mlioana kwa ajili gani?
  Pesa,mlilazimishwa, matatizo, upendo wa kweli etc

  Na kitu kingine kinacho changia
  ni uhuru na sheria zinazotulinda..
  ni ile unaniletea uzushi na mwita lawyer wangu..
  system ziko hapo kutulinda lakini cheki tunavyo chukua advantage ...

  Sababu nyingine ni kuwa mroho/selfish
  mmezaa mnafamilia lakini bado unataka
  kuishi maisha ya mtu singo.. nimesema
  selfish sababu watu hawataki ku comprise vitu
  fulani maishani na anajua hichi kitu kinaweza kusambaratisha
  ndoa yangu..

  Kuna sababu nyingi tu..
  dahh ndoa nyingi USANII +SHOW OFF
   
 13. nnunu

  nnunu JF-Expert Member

  #13
  Apr 21, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 656
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
   
 14. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #14
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Daaahh
  jamani Fidel umeanza ae
  kaniletee fimbo.. ukileta nyembamba
  wajia nini kitatokea mmmhhh
   
 15. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #15
  Apr 21, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160

  Haisaidii kabisa nikwambie hata nyumba kubwa nayo siku hizi imekosa masters ya uvumilivu
   
 16. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #16
  Apr 21, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,713
  Trophy Points: 280
  Mapenzi ya siku hizi uongo/udanganyifu mwingi
  tamaa imetawala kuliko upendo wa kweli
  mke/mume mnajaribu kuongea haisaidi hakuna mabadiliko
  unavumilia miaka na miaka mwishowe unapata
  matatizo ya kiafya kwa nini usubiri upate ugonjwa wa moyo
  bora kila mtu kuchukua hamsini zake.
   
 17. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #17
  Apr 21, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Maty nimependa mawazo yako,ivi mtu anapokupa psychological abuse kila wakati ina maana kweli kuendelea kukaa na mtu huyo sababu ya watoto tu mpaka siku utakapokuwa kichaa usemee unavumilia.
   
 18. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #18
  Apr 21, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  nilidhani lbd ndoa za kilokole zinaweza kuwa na unafuu!!

  Hivi juzi tu hata mwezi haujaisha dada mmoja mpiganaji kweli kweli na mwanamaombi aliolewa na kk mmoja mlokole mwenzie, kweli harusi ilikuwa nzuri!! wiki ile niliyofiwa akaja kunipa pole akiwa na mama mmoja mchungaji rafiki yangu, baada ya kuona muda umeenda sana, nilimuuliza nawewe unakesha?? akasema ndio, nikamuuliza shemeji vipi hata kasirika akasema tumeshaachana!! nilishika mdomo.

  kumbe nasikia walitengana baada ya week 2 tu!! yule mama mchungaji aliniambia kuwa baada ya tu ya siku 2 za ndoa akaanza kusuluhisha kesi zao mpaka mwisho amechoka.

  Nikasema duh!! kwakweli kuna haja ya kuendelea kuwa single mpaka kieleweke!!!
   
 19. Maty

  Maty JF-Expert Member

  #19
  Apr 21, 2011
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 2,170
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Dah! mawazo yenu niliyoyapata hapa inaonyesha ndoa ni ngumu sana asee
   
 20. Maty

  Maty JF-Expert Member

  #20
  Apr 21, 2011
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 2,170
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Hapa ndio nimechoka kabisa lol
   
Loading...