jimyjooo
Senior Member
- Feb 2, 2017
- 129
- 66
naomba nami niunge hukoVLOOKUP nimeizungumzia Kwa clip fupi kule Telegram Sijajua kama upo kule..
Kiufupi sana.. VLOOKUP Hukuwezesha kutafuta kitu chochote katika Sheet Vertically ndani ya sekunde tu...
=VLOOKUP (D10,A1:F10,4,FALSE)
D10 hii ni CELL ambayo utakuwa ukiandika jina la hiyo item unayoitafuta so inategemea Unataka ionekane wapi katika Sheet yako
A1:F10 ni data zote ambazo Unataka ziwe considered ukiangalia vizuri nimeanza na A1 hadi F10 so lazima I select data zako zote
4 hii ni Column.. Je hiyo value au price ipo katika colum ya ngapi kutoka mwanzo?
FALSE ni kuwa jina utakalo liandika li match sawasawa na unachokitafuta ukiandika TRUE inaamana ikutafutie Value yeyote ambayo inakaribiana
Bonyeza Enter na Anza ku search items katika Cell D10
Hakikisha umeandika formula pale ambapo Unataka Jumla itokee... Andika kama inavoonekana Kwenye picha halafu bonyeza enter..
Rudia mara mbili Tatu utazoea.. Usisahau kuingia Kwenye Telegram nitakuwa naweka video fupi ili ieleweke vizuri