Kuna barua muhimu ya kijeshi inabidi ipelekwe mji B kutoka mji A.Kati ya mji A na mji B hakuna kituo cha mafuta.Gari iliyopo ikijazwa 'full tank',ina uwezo kusafiri nusu ya umbali kati ya A na B.Licha ya hii gari hii,kuna gari zingine tisa zenye uwezo sawa na gari hili.Hakuna kamba ya kuvutia gari,hakuna uwezekano wa gari kubebana wala kusukumana,hakuna vifaa vya ziada vya kubebea mafuta.Mji A na mji B kuna vituo vya mafuta vyenye mafuta ya kutosha.(SWALI)Kwa kutumia idadi yoyote ya magari kati ya yaliyopo(10),utafanyaje kuisafirisha barua hii muhimu kutoka A hadi B.(HINT):huruhusiwi kuitelekeza gari yoyote njiani kati ya mji A na mji B.
Tawire umepatiaYaani tangu mchana nafikiria ila sijapata jibu, ngoja nichakachue.... Kwa kuwa kuna magari kumi na full tank ya gari moja itawawezesha kufika nusu ya safari, basi ningewashauri wafungue Tank moja la gari nyingine kisha waijaze mafuta na waibebe kama ziada kwenye gari itakayosafiri.. Kisha wajaze Tank ya hilo Gari, kwa mantiki hii watafika mwisho wa safari bila tatizo lolote.. ......... Lol
Upo sahihi lakini magari utayatelekeza njiani,nenda na hii solution katika swali la tupe maujanja part 2!Hii kali, lakini ngoja nijaribu.Kuna gari 10 zenye full tank na zote zitaishia katikati ya safari kabla mafuta hayajaisha. Itakuwa hivi. Zitaondoka zote hadi robo ya safari. Gari tano zitatoa mafuta yake yaliyobaki kwa gari tano, hivyo gari hizo zitafika katikati ya safari zikiwa na mafuta ya ziada. Pale magari matatu yatafaulisha mafuta yaliyobaki kwenye magari mawili yaliyobaki ambayo yataenda hadi robotatu ya safari na gari moja litaachia mafuta yaliyobaki kwa gari moja litakalomaliza safari na kuwahisha barua hiyo muhimu