KAYGREKO
Member
- Jan 18, 2013
- 37
- 32
Mara nyingi huzuka mjadala wa umuhimu wa lugha ya kiingereza inapotokea Mtanzania kuhojiwa kwa kiingereza na akawa hajielezi vizuri kama wanavyojieleza ndugu zetu wa mataifa mengine ya kiafrika yanayotumia kiingereza.
Hapa hupatikana wale wataohoji kuwa elimu ya Tanzania ipo chini na kuponda mfumo wetu wa elimu, lakini aidha kutakuwa na wale wataotetea kuwa si aibu wala vibaya kwa mTZ kutojua kiingereza kwa sababu sisi tuna lugha yetu ya kiswahili. Ili mradi kila mara mjadala humalizikia palepale katika miono miwili isiyokaribiana.
Binafsi huku nilipo nimeweza kuwaona wabongo wanaoongea sana wanapokuwa ktk kundi la wabongo, ila inapotokea kujiunga na mapopo(hapa nikimaanisha wanigeria) wabongo hao huwa kama wamemwagiwa maji ya barafu.Huwezi kuamini kama wao ndiyo wale waliokuwa waongeaji wazuri .
Hushindwa hata kushiriki na wengine hutafuta hoja ya kujiondosha. Ajabu ya mambo mapopo wengine huwa HAWANA HATA DARASA MOJA!!! Ila kwa kuwa huwa wanarap ile pidgin english huonekana eti WANAJUA SANA KULIKO CC WABONGO.
Hali hii ya kutoweza kujieleza kwa kiingereza imesababisha asilimia kubwa ya wabongo wajijengee INFERIORITY COMPLEX.Imewafanya wengi wajihisi unyonge pale wanapohitajika kujieleza kiingereza.
Hivi aliyezaliwa na kuishi USA, akaacha masomo akiwa shule ya msingi atakuwa bora kuliko mTZ aliyekwenda University ?kwa sababu tu huyu mTZ hatokuwa fluent in english kama alivyo wa USA?
Of course kuna ukweli kuwa yeyote anaejua lugha ya kiingereza humsaidia sana ktk mawasiliano yake na wageni. HILI HALIHITAJI MJADALA WALA UBISHANO. Na ni vizuri mno wabongo kujua kiingereza,ILA HAKUNA HAJA YOYOTE KWA YULE ASIYEJUA KIINGEREZA AJIHISI UNYONGE.Kutojua kujieleza kifasaha kwa kiingereza does not necessarily mean kwamba mtu huyo hana elimu.KUNA TOFAUTI KUBWA MNO KATI YA KUWA NA ELIMU NA KUJUA KIINGEREZA.
Natamani siku JPM atapokwenda kuhutubia UN aongee Kiswahili na apatikane mkalimani kama wanavyofanya viongozi wa nchi nyingine.Marais wanaotumia lugha za kwao siyo kwamba hawajui kiingereza na Mungu hakuziumba lugha zao na kuzifadhilisha kuliko yetu..
LAZIMA TUJIVUNIE LUGHA YETU NA WAKATI HUO HUO TUSIISHI KAMA KISIWA.TUJIFUNZE LUGHA ZA KIGENI ILA TUSIJIINGIZE UNYONGE KWA KUTOJUA LUGHA YA KIINGEREZA.