Tuongee Asubuhi STAR TV: Mgogoro Libya...Changia Mawazo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuongee Asubuhi STAR TV: Mgogoro Libya...Changia Mawazo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Yahya Mohamed, Sep 3, 2011.

 1. Yahya Mohamed

  Yahya Mohamed Verified User

  #1
  Sep 3, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Baada ya Kimya kirefu kutokana na Majukumu mengine ya kikazi kesho nitakuwapo hewani kujadili kuhusu Mgogoro wa Libya na Nafasi ya AU katika siasa za Afrika.

  Wageni ni HEBRON MWAKAGENDA na DEUS KIBAMBA - Dar

  Comments za wanaJF zitajumuishwa pia, zile tu ambazo zitatufikia kabla ya saa 1:00 asubuhi. Vinginevyo unaweza kutuma LIVE Text kupitia simu yangu ya kiganjani ambayo ni 0685 358973

  Alamsiki
   
 2. kinja

  kinja Senior Member

  #2
  Sep 3, 2011
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kwanza hongera star tv kwa mada hii. Mimi naipongeza AU hasa South Africa kule security council. Pamoja na siasa za Libya kuwa za kinafiki kwa hawa NTC, Maana wengi ni defected leaders wa serikali ya Gadafi. So if Gadaf ni tatizo basi wao ni sehemu ya tatizo hilo.

  AU haitambui NTC lakini kuna nchi nyingi members wa AU wanaitambua NTC sijui hapo pamekaaje? Natamani siku moja GADAFI declares victory vs traitors and NATO. Shame to those takes life for oil ie NATO and their allies
   
 3. Paul Kijoka

  Paul Kijoka JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,400
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Nimefuatilia sana kipindi. Msemaji umeonekana kuwa msemaji mwenye uelewa hasa katika mambo ya ungwine (historia). Lililonishangaza ni jinsi ulivyotengenezwa kuuza elimu yako kwa CCM hasa kwa kuponda mambo yote yaliyokuwa against chama na kujifanya unaelezea mazuri tu huku ukisahau kuwa nchi yetu inakombwa na wahuni. Binafsi sijakufagilia.
   
 4. brazakaka

  brazakaka Senior Member

  #4
  Sep 3, 2011
  Joined: Mar 3, 2010
  Messages: 118
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Umoja wa Afrika kwa kukaa kimya ni kama vile umebariki Majeshi ya NATO yaungane na waasi kumwondoa Gaddafi na umekwenda kinyume na malengoya kuanzishwa kwake ambayo ni kudumisha Umoja wa kindugu baina ya Wanachama wake, kupinga ukoloni barani Afrika na kukuza ushirikiano wa Kimataifa.

  Isitoshe wakuu wa nchi hizi hukutana kila mwaka kuratibu masualambalimbali ya Kisiasa, Kiutamaduni, Afya, Sayansi na Ulinzi, hivi walishindwa nini kuchukua jukumu la kulinda raia wa Libya na badala yake wakawaachia NATO ambao waliamua ku side na waasi? Kukosekana kwa umoja kwa viongozi wa Afrika kutasababisha western powers waendelee kutudharau na kutushambulia kila mara watakapojisikia kufanya hivyo.
   
 5. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #5
  Sep 3, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,773
  Likes Received: 2,675
  Trophy Points: 280
  Mgogoro wa Libya ni wakupikwa na nchi za magharibi Marekani ikiwemo. Lengo lao(nchi za magharibi + Marekani )

  kwanza kudhoofisha Umoja halisi na wenye nguvu za kujitegemea wa Waafrika ambao Comred Ghaddaf alikuwa tayari kuugharamia kwa rasilimali za waafrika wa Libya kama Baba wa Taifa la Tanzania Mwl. J.K.Nyerere alivyotumia rasilimali za waafrika wa Tanzania kupigania uhuru wa waafrika jambo ambalo alifanikiwa kwa kiasi kikubwa. Kwa kifupi Ghaddaf alikuwa anataka kukamilisha kazi walioianzisha wapigania uhuru wa Afrika (Kwame .N, P.Lumumba,Mwl.J.K.Nyerere,N.Mandela na wengine wa aina yao) yaani Afrika huru yenye Umoja, Amani, na uwezo wa kujitegemea.

  Pili kuiba rasilimali za waafrika waishio Libya ili kutuliza hasira za raia wa nchi zao ambao kwa sasa wanalazimishwa kufunga mikanda, kila mtu anajua uchumi wa nchi hizo unavyo yumba.

  AU ya sasa haina uwezo wa kuwasaidia waafrika kufikia lengo lao la kuwa wamoja, wanoishi kwa amani, huku wakipiga hatua kujiletea maendeleo ya kwel i(Rejea mahojiano ya Dr. Salim Salim(former OAU secretary) aliyoyafanya jana na idhaa ya kiswahili ya BBC.

  Lakini ninaamini harakati za Waafrika kujikwamua kutoka ghiliba hizi za nchi za magharibi hazijakoma bado, kwani kwa sasa waafrika hawa wazalendo wanafuatilia kwa makini jinsi juhudi za waafrika wenzao wapigania maendeleo ya waafrika zinavyozimwa kwa hila na wanaotaka afrika iendelee kuwa tegemezi kifikra na kwa kila hali ya namna yoyote ile. Mbinu watakazozitumia Waafrika wazalendo hawa kurudisha hadhi ya Afrika mbele ya mabara mengine zitabadilisha historia ya Ulimwengu.
   
 6. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #6
  Sep 4, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Asante kwa mada nzuri mkuu,

  Hili liwe somo kwa nchi hizi za Africa hasa kwa hao viongozi wanaotaka kuongoza watu mpaka wajichokee wenyewe mfano Gaddafi haingii utawale watu karibu miaka 42 then ukasema kuna demokrasia regardless kua unawapa watu mahitaji ya msingi, kuvamiwa kwa kwa huyu bwana ni sahihi kabisa na pia viongozi wa Africa walioshindwa kukemea hili wanaogopa nchi za magharibi kwa kua wanawapatia misaada,yangu ni hayo kaka.
   
 7. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #7
  Sep 4, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu yahya muhamedi ebu muulize mwanaharakati Deus nini hasa chanzo cha huu mgogoro?

  Kama ni nguvu ya umma; je ni kweli nguvu ya umma inayotumika kumuondoa col Gaddafi madarakani?? Je hiyo si vita kweli ni hayo hongereni star tv mna mada nzuri sana zinatuelimisha.

  Natarajia majibu hapo asubuhi
   
 8. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #8
  Sep 4, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Hii ni tia maji tia maji kwa Viongozi wote wadanganyifu wababe na madharimu Libya lazima kulikuwa na Tatizo Gaddafi lazima atakuwa na Tatizo kukaa kwake madarakani Miaka zaidi ya 40 Na Plan yake ilikuwa kumachia Mwanae aongoze so Yeye Alipindua nchi kutoka kwa Mfalme wa Libya Nae Ndio hivyo auae kwa upanga uuliwa kwa Upanga Atoke tu na hao watakao ingia watakubalika na baadae watachokwa lifes goes on tu.

  Nchi zingine zitatia Adabu ziendelee kutawala au Kuongoza! Kaua Askari wake wengi waliokataa kuua Raia waliokuwa Wanaandamana Tatizo lake linafanana na la Mkwe re Visasi na Upendeleo hata usiohitajika na ulazima wowote na masikio yake ameziba
   
 9. jambo1

  jambo1 JF-Expert Member

  #9
  Sep 4, 2011
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hongera Start TV kwa Kipindi kizuri kwa mustakabari wa Taifa na dunia kwa ujumla..!
  Swali kwa wachangiaji wakuu..
  Je hakuna hatari yeyote kwa harakati hizi za kuwang'oa viongozi waliokaa madarakani kwa muda mrefu kama vile Ghadaf(Libya), Ben Ali(Tunisia),Hosen Mubarak(Misri) zikahamia katika kuvingo'oa vyama vya siasa ambavyo na vyenyewe vimekaa madarakani kwa muda mrefu huku vikisimamia chaguzi ambazo zimejawa na mizengwe..?
  Asante sana Star TV..,tutakuwa pamoja katika kipindi Tanesco wakijaaalia..!
  Inshallah..!
   
 10. j

  juni Member

  #10
  Sep 4, 2011
  Joined: Apr 5, 2011
  Messages: 87
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ukiwasikiliza viongozi wa nch za kiafrika mf wazr mambo ya nje kenya. utagundua wanaunga mkono harakat za wanalibya kumuondoa gadaf tatizo walikuwa wanaogopa kumpinga wazwaz mfadhil wao huyo pia ni nan kiongoz wa kiafrika msaf kias cha kuunga mkono harakati za kumuondoa dikteta. vinginevyo watakuwa wanapalilia njia watakayopita wao wenyewe. ni vyema sa viogoz wetu wakajifunza kwanba hakuna nguvu ya kijesh inaweza kushinda ya umma. wananch wazalendo nao wametiwa moyo kwamb licha ya ghrama kubwa wanaweza k
  Jukwaa la Siasa
   
 11. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #11
  Sep 4, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Gadafi ni mkabila aliwagawa walibya ,hamna uhuru wa kujieleza,na kwa nchi kama libya huduma za kijamii zilitakiwa ziwe ktk hadhi ya juu zaidi,misaada yake mingi ilikuwa ya kubagua jamii fulani mfano alijenga misikiti wala sio shule au vyuo ambavyo vingekomboa jamii nzima!libya is better without Gadafi aliitenga libya na jumuiya za kimataifa!
   
 12. MAGAMBA MATATU

  MAGAMBA MATATU JF-Expert Member

  #12
  Sep 4, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 60
  Sikutegemea kiongozi kama Membe angeweza kuongea kuwa hawawatambui Waasi wa Libya,tatizo serikali ya TZ inatanguliza sana siasa kuliko hali halisi ya matatizo ya watu,Libya ni nchi ya walibya na siyo nchi ya Gadafi kama Membe anavyofikili,yeye ni kiongozi inabidi kabla hajaongea afikili mara mbili.
   
 13. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #13
  Sep 4, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  kwa jinsi mgogoro huu unavyokwenda nahisi libya itatumbukia kwenye matatizo makubwa siku za usoni'gaddafi na wafuasi wake hawawezi kukubali kushindwa kirahissi'tukumbuke kuna watu wengi wapo nyuma ya gadafi'mabomu ya kujitoa muhanga yakianza ndiyo iraq mpya imezaliwa ndani ya libya
   
 14. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #14
  Sep 4, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Tutajie ukabila wa Gadafi na jinsi alivyowagawa wa Libya!
   
 15. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #15
  Sep 4, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Hakuna lolote kwenye vita vya Libya zaidi ya mafuta, kama suala kukaa muda mrefu madarakani mbona Malikia wa Uingereza hawajamtoa!
  Wala hakuna nguvu ya umma pale Libya, waliongusha utawala wa Libya ni Nato na US, kama hawa wazungu wanawapenda waafrica mbona hawaendi Zimbabwe kumtoa Mugabe!
   
 16. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #16
  Sep 4, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa anaeongea kavaa shati jekundu na tai pumba sana huyu jamaa sijui Star tv huwa wanamtoa wapi
   
 17. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #17
  Sep 4, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,823
  Likes Received: 922
  Trophy Points: 280
  Nashauri Umoja wa Afrika uvunjwe..iundwe taasisi nyingine mpya ya kusimamia kipindi cha mpito ambacho kitakua na maelengo na mipango madhubuti kwa ajili ya Afrika kwa mda mrefu..ikiwemo kutoa utaratibu wa nchi kuongozwa kwa kufuata katiba na kusimamia kwa dhati raslimali za nchi husika kwa kila mtu wa nchi hiyo...

  Baada ya hapo malengo na mipango ya kiuchumi, Ulinzi wa Afrika yawe mamoja ili kwamba kama nchi za Nato ambazo ni magaidi zikija kutaka kupiga Afrika yetu sote tuipiganie Nchi hiyo iliyovamiwa
   
 18. k

  katununu Member

  #18
  Sep 4, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 20
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 5
  <br />Sio kweli Ritz.kwanza tukubali kuwa kutawala muda mrefu ni chanzo cha udikteta;na ha a demokrasia ya leo au xa magharibi ni matokeo ya funzo la udikteta;pili,hata kama chama cha labour kina mpango wa siri kuondoa Ufalme Uingeleza,lakiini ni ukweli kuwa ufalme huko ni figur <br />
   
 19. k

  katununu Member

  #19
  Sep 4, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 20
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 5
  Kwanza jukubali kuwa kutawala muda mrefu nichanzo cha udikteta.historia ni hakimu mzuri,demokrasia ya leo au yakimagharibi nimatokeo ya somo la udikteta;na ukweli ni kuwa Malkia hana nguvu yoyote,ni sawa
   
 20. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #20
  Sep 4, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Ukituambia huyo jamaa aliyevaa shati jekundu na Tai anaongea Pumba, kitendo cha kumuita tu jamaa unaonyesha kwa jinsi ulivyo na mawazo hasi juu yake na hujui siasa za Tanzania...SI jamaa anaitwa DEUS Kibamba na kama humuji Kibamba inaelekea upo sayari Nyingine na alikuwa anaongea kwa kunukuu AU Charter na Democracy charter kama ni pumba basi pumba zinatoka katika misahafu hiyo Mkuu.

  ADIOS
   
Loading...