utekelezaji majukumu -- na hasa usimamizi -- kuhakikisha uwajibikaji, uwazi na ukweli kambi ya upinzani bungeni unajengwa na mazingira ya wao kufanyia kazi bungeni-- kuwepo kwa kanuni zinazoruhusu wapinzani hata kama ni kundi dogo kufanya kazi kwa ufanisi, kuhakikisha kuwa wananchi wa kada mbali na hasa wasionacho:msela: Wanawakilishwa kikamilifu. Yote haya yanapaswa kupimwa dhidi ya mazingira ya bunge la sasa hivi.
Haya ndiyo maudhui ya kipinndi chetu cha kesho alhamisi kuanzia saa 1.30 asubuhi kwenye tuongee asubuhi.
Nakaribisha hoja waungwana.
asante paul mabuga-mchango wangu
1. Kanuni hazijaanza leo -kama kawaida yao ccm badala ya kutatua matatizo ya wananchi wanakesha kutafuta jinsi ya kuupozesha upinzani.
2. Ccm lazima wajue kila wanachofanya kina mwisho -wajifunze misri na tunisia.
3. Hoja sio wapinzani kuungana -hawawezi kuungana wakati wana ilani tofauti, wametokea vyama tofauti na wana vipa umbele tofauti- hoja ni mustakabali wa nchi hii-mfumuko wa bei, katiba mpya, makazi duni, elimu duni, afya duni, ukosefu wa maji, uadilifu na uwajibikaji kwa walio madarakani.
4. Chadema inasifa kupitia kanuni kuunda au kutounda kambi ya upinzani kwa maana kwamba wana 12.5% ya wabunge -vyama vilivyobaki haviwezi kuwa na kambi ya upinzani ila watakuwa wapinzani kwa hoja wanazozisimamia.
5. Spika wa bunge asiwe mnafiki atapoteza maana ya bunge -tumeshaona anakuwa kibaraka na mkandamizaji-aruhusu mijadala asikimbie mijadala -ataliua bunge.
6. Kwa hiyo kimsingi hoja hapa ni kwamba nini mbunge kama mbunge anasimamia, mbunge anatakiwa kusimamia anaowawakilisha na kuhakikisha serikali inafanya kazi yake, sio kazi ya bunge wala spika kuilinda serikili.
7. Mafanikio ya bunge lolote yanategemea umahiri na ujasiri wa spika-lakini kwa ninavyoona mimi mama makinda anaogopa mijadala na hivyo bunge halitafanikiwa. Ni kibaraka wa serikali tooooooooooooo bad.