Tuongee Asubuhi Alhamisi Live on Star Tv | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuongee Asubuhi Alhamisi Live on Star Tv

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Paul Mabuga, Feb 9, 2011.

 1. P

  Paul Mabuga Verified User

  #1
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Utekelezaji majukumu -- na hasa usimamizi -- kuhakikisha Uwajibikaji, Uwazi na Ukweli kambi ya Upinzani Bungeni unajengwa na mazingira ya wao kufanyia kazi Bungeni-- Kuwepo kwa kanuni zinazoruhusu wapinzani hata kama ni kundi dogo kufanya kazi kwa ufanisi, kuhakikisha kuwa wananchi wa kada mbali na hasa wasio nacho wanawakilishwa kikamilifu. Yote haya yanapaswa kupimwa dhidi ya Mazingira ya Bunge la sasa hivi.

  Haya ndiyo maudhui ya Kipinndi chetu cha kesho alhamisi kuanzia saa 1.30 asubuhi kwenye Tuongee asubuhi.

  Nakaribisha hoja waungwana.
   
 2. D

  DENYO JF-Expert Member

  #2
  Feb 9, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 699
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  asante paul mabuga-mchango wangu

  1. Kanuni hazijaanza leo -kama kawaida yao ccm badala ya kutatua matatizo ya wananchi wanakesha kutafuta jinsi ya kuupozesha upinzani.

  2. Ccm lazima wajue kila wanachofanya kina mwisho -wajifunze misri na tunisia.

  3. Hoja sio wapinzani kuungana -hawawezi kuungana wakati wana ilani tofauti, wametokea vyama tofauti na wana vipa umbele tofauti- hoja ni mustakabali wa nchi hii-mfumuko wa bei, katiba mpya, makazi duni, elimu duni, afya duni, ukosefu wa maji, uadilifu na uwajibikaji kwa walio madarakani.

  4. Chadema inasifa kupitia kanuni kuunda au kutounda kambi ya upinzani kwa maana kwamba wana 12.5% ya wabunge -vyama vilivyobaki haviwezi kuwa na kambi ya upinzani ila watakuwa wapinzani kwa hoja wanazozisimamia.

  5. Spika wa bunge asiwe mnafiki atapoteza maana ya bunge -tumeshaona anakuwa kibaraka na mkandamizaji-aruhusu mijadala asikimbie mijadala -ataliua bunge.

  6. Kwa hiyo kimsingi hoja hapa ni kwamba nini mbunge kama mbunge anasimamia, mbunge anatakiwa kusimamia anaowawakilisha na kuhakikisha serikali inafanya kazi yake, sio kazi ya bunge wala spika kuilinda serikili.

  7. Mafanikio ya bunge lolote yanategemea umahiri na ujasiri wa spika-lakini kwa ninavyoona mimi mama makinda anaogopa mijadala na hivyo bunge halitafanikiwa. Ni kibaraka wa serikali tooooooooooooo bad.
   
 3. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #3
  Feb 9, 2011
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Mabuga ndugu yangu, tatizo la sasa nadhani ni juu ya WAPINZANI kuanza kuchezewa bila wao kujua, hii hoja mlivyoiandaa binafsi naona kama mmeandaa na majibu.

  Ingependeza mkajaribu kuangalia hivi:

  Hali ya sasa ya kambi ya Upinzani bungeni, bila mshikamano kuna ufanisi wa kambi hii?

  SASA: Hapo ndipo wale wanaopenda kuona upinzani unaungana watamwaga sera zao, wale wanaoona hakuna haja watamwaga sera zao. Wale wanaodai kuna mkono wa chama tawala katika vyama vya upinzani pia watamwaga sera zao.

  HATA HIVYO: Tutajitahidi kutazama mjadala kuanzia mwanzo hadi mwisho, 'nadhani' nitapiga simu na nitajitambulisha kama Paul!
   
 4. Innobwoy

  Innobwoy JF-Expert Member

  #4
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 980
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 60
  Bro Mabuga naomba uwape notice Tanesco maani siku hizi sa12 alfajiri wanakata na wanaleta sa4 usiku,kama vipi ipelekeni live na Radio free ili wakichukua umeme radio zetu za mkulima zinasaidia,
   
 5. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #5
  Feb 9, 2011
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Mkuu Denyo,

  Binafsi nadhani itabidi aidha tuangalie upya kanuni za bunge au tufanye kutafuta jinsi nyingine ya kundi dogo nalo kuwa na uwakilishi kama kweli tunahitaji kuwa na demokrasia ya kweli.

  Aidha, ni vema spika akitoka chama tawala basi naibu wake iwe ni LAZIMA atoke muungano wa vyama vya upinzani BILA kupigiwa kura na wabunge wa chama kinachotawala.

  CCM wasiifurahie hali ya sasa kwani endapo siku moja wao watakuwa chama cha upinzani wataona athari ya mambo haya
   
 6. P

  Paul Mabuga Verified User

  #6
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nakushukuru sana Robot!
  Nazingatia sana ushauri wako na pia nategemea mchango wako!
  Niliona ni vema niweke maudhui badala ya kichwa cha mada ili waungwana wachangie!
  :clap2:
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Feb 10, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Natamani niweze kutoa mawazo asubuhi hii.
   
 8. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #8
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Tatizo lako paul mabuga unabana sana muda wa wananchi kupiga simu. Unaendesha mjadala hadi sa tatu kasoro robo matokeo yake wanapiga simu watu wawili na kipindi kinaisha. Wewe ndio unakua mzungumzaji mkuu badala ya watu uliowaalika. Nakuomba mabuga ujifunze kwa samadu hasan na rymond nyamuhula ambao wanatoa muda wa kutosha kwa wananchi kupiga simu. Ukiendelea hivya basi mabuga utakua unaondoa dhana ya tuongee asubuhi na kuwa muongee asubuhi.
   
 9. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #9
  Feb 10, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,003
  Likes Received: 325
  Trophy Points: 180
  Tutaifuatilia kwa makini then tutatoa maoni kwa simu
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Feb 10, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Nimejaribu kupiga lakini mmh..
   
 11. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #11
  Feb 10, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,003
  Likes Received: 325
  Trophy Points: 180
  Kipindi kimeanza lakini wageni waaliktwa simba chawele na H.R, Lisu amepata dharura amenda jimboni kwake leo asubuhi naona kipindi hakiko balance kwani kimepwaya
   
 12. c

  chigwiye JF-Expert Member

  #12
  Feb 10, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 353
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mabuga,Theme utadhani risala,muisamarize iwe short and clear to the point.mtu akisoma hapo hata hawe jua mnataka nini specificaly.Chkua ushauri wa INVISIBLE
   
Loading...