Tunu Pinda, amepata ajali ya gari Morogoro

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,480
Mke wa waziri mkuu mstaafu Tunu Pinda, amepata ajali ya gari Morogoro, akitokea Dodoma kuelekea Dar es salaam. Amepata majeraha na anaendelea na matibabu.
69cbc9206e7575ec45c42707181641a5.jpg


=======================================

Mtu mmoja afariki katika ajali ya gari na 4 wamejeruhiwa akiwemo mama Tunu Pinda Morogoro.

Mtu mmoja amefariki dunia na wengine wanne wamejeruhiwa akiwemo mke wa waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda Mama Tunu Pinda baada ya gari walilokuwa wakisafiria kumgonga mwendesha pikipiki wakati akikatisha barabara katika eneo la Mkundi barabara ya Morogoro Dodoma manispaa ya Morogoro.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa nane mchana katika eneo la Mkundi ikihusisha gari lenye namba za usajili STK 9242 gari la mke wa waziri mstaafu Mizengo Pinda likitokea Dodoma kwenda jijini Dar-es-Salaam na pikipiki ambapo mkuu wa mkoa wa Morogoro Dokta Rajabu Rutengwe anaelezea kuhusiana na ajali hiyo.

Majeruhi wengine wa ajali hiyo ni dereva wa gari hilo Bw Anjelo Mwisa, mlinzi wa mke wa waziri mkuu mstaafu Gaudensi Tembo na kijana wa familia ya Mama Tunu Pinda Bwana Gilbert Sampa.

Kwa upande wake mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro Dr Rita Liamuya amesema hali ya mke wa waziri mkuu mstaafu na majeruhi wengine zinaendelea vizuri na kueleza kuwa majeruhi hao wanatarajia kuhamishiwa jijini Dar-es-Salaam kwa matibabu zaidi.

Chanzo: ITV
 
Mke wa waziri mkuu mstaafu Tunu Pinda, amepata ajali ya gari Morogoro, akitokea Dodoma kuelekea Dar es salaam. Amepata majeraha na anaendelea na matibabu.
Ni ajali kama ajali zingine....akatoe shukrani kwa Mungu kwa kuepushiwa kifo
 
kwa mwendo wa hovyo wa dereva na upitaji wake magari na jinsi alivyotupita kwenye kibao cha 50.na hata ajali kapata kwenye 50kph niwe muwazi nilitamani angekufa tu yule dereva.ule udereva wa misafara na ving'ora anauleta bila kuangalia speed za alama.anatembea speed za kipumbavu angekufa tu.pole yangu kwa mama pinda nawale wawili wengine lakini si kwa dereva
 
Mtu mwenye bodaboda amepoteza maisha hapohapo....inasemekana kijana huyo mwenye bodaboda alikuwa anakatiza barabara ndipo alipokutana na gari likiwa mwendo kasi. gari la mke wa pinda limehalibika upande wa mbele.
 
Back
Top Bottom