Tungo ya turufu

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,638
697,929
Naiandika tungo hii nikijua ya kuwa
Ni kwa wale wana kaya kuu, walio mahiri
Kabisa katika kaya iliyotukuka sana!
Wenye hekima kama wendawazimu na
Wenye busara kama vichaa nikijua fika ya kwamba hawa ndio watakuwa wa kunielewa
Ni tungo ya turufu, turufu ya mustakabali wa kaya yetu! Kaya yetu tuipendayo sana

Naiandika kwa wana kaya wote, watukuka sana! Waheshimiwa sana! Waliojikweza Kabisa! Na hata kwa wale waliolala kuzimu wasubiriao parapanda kuu, nyamafu waonao lakini hawaelewi, wasikiao lakini hawajibu, waliolala daima wakitazama upande!

Nalisema kuwa nani atudanganyae kwamba ustaarabu ni kuwa na miguu minne na kibanda cha ngazi? Kusoma mabuku mengi na kutafakari tusiyoyajua? Hakika siri za kaya hii ni nyingi na zisizoelezeka, na kamwe hatuwezi kuzifahamu zote hata kwa kutumia ujinga wa mwerevu wa bana mtwana kitwana!!!

Twalikumbuka kusahau kuwa ile kweli iitwayo kweli kuu ndio uongo na uoza unukao kuliko manukato ya yule mteule!
Natujiongopee basi ya kuwa hii iitwayo kweli kuu ndio dira yetu ituongozayo kusiko! Kwanini basi tusikae sisi kwa sisi! Sisi na wale na kusemezana wenyewe yale yatuhusuyo kama kaya...vipaumbele vyetu kanuni zetu maono yetu.....
 
Duu!!sory mkuu mrisho mpoto una undugu nae
 
Sehemu ya pili;

Kwanini basi tutunge kanuni tusiyoitumia? Faida yake nini kununua kitu kisha usikitumie? Kimekuwa pambo?
Kwanini sasa tupelekwe kushoto? Tupelekwe kulia? Tuviringwe viringwe? Tupinduliwe juu chini , tufinyangwe finyangwe kama chachandu na salo la muuza mbilimbi?

Kwanini basi tukubali? Natulikatae hili
Natutunge kanuni yetu wenyewe, ya wana kaya wetu wenyewe , bila kupangiwa bila kulazimishwa bila kutungiwa bila vikwazo vitisho na pingamizi
Hii ndio itakuwa kanuni yetu rasmi
Itakayoongoza kaya hii hadi pale penye uhuru wa kweli usalama kwa wote na neema kuu! Neema kwa kila mwana kaya bila kubaguana

Tazama basi twalifundishwa kuita ni ustaarabu kupenga kamasi kwenye leso na uvundo wake kuufutika kibondoni, tukashinda nao kutwa, tukakesha nao kucha, tukatoa vibindoni mwetu, tuoshe uvundo ule uoza ule utelezao kama gilisi ya gali moshi. ... eti twauita usafi basi na mate tuyatemayo nayo tuyatendee vivyo hivyo

Hatuwezi kuwa na majigambo ya kuwa na vipara na vitambi vya vitimbi kwa ajili ya kubukua miongo lukuki?
Haijalishi ni mabuku mangapi tumebukua!au ni stashahada na shahada ngapi tumepata au tumesafiri ughaibuni mara ngapi kutafuta maarifa...!!!
Natujitafakari...! Tumeelewa na kuelimika kiasi gani
Maarifa kiasi yenye kuakisi uhalisia ni bora kuliko kubukua mabuku mia ya Max na Lenin , wale wana kaya waliosifika enzi yao halafu ukatoka kapa
 
Sehemu ya pili;

Kwanini basi tutunge kanuni tusiyoitumia? Faida yake nini kununua kitu kisha usikitumie? Kimekuwa pambo?
Kwanini sasa tupelekwe kushoto? Tupelekwe kulia? Tuviringwe viringwe? Tupinduliwe juu chini , tufinyangwe finyangwe kama chachandu na salo la muuza mbilimbi?
...itaendelea
Nadhani tunafundishwa kareti alafu mwisho wa siku tutapandishwa ulingoni
 
ngoja nikanywe maji nipunguze maumiv ya kichwa manake habari za hii kaya ni pasua kichwa
 
Sehemu ya tatu;

Hakika kining'ina na kilembwe cha mtwana kufa kunoga kitawahukumu! Tulonge nini basi? Tugonde nini basi? Turopoke na kujikweza kwa takwimu hewa na neema kavu! Tukisema hivyo hata shetani hatatuamini
Tutasilibaje udi na uturi kwenye ngozi isiyooshwa na gagulo lisilofuliwa?
Tangu lini uvundo ukafutikwa kwa manukato na uaridi?
Hakika wendawazimu si lazima kuchojoa gagulo na kupayuka hadharani

Wanakaya sasa wamekuwa wehu, mwendawazimu ana afadhali, wale vigego wao wamepindika wakapinda, utanyoroshaje mkwiji kwa boriti ya ribiti

Sikukosea kabisa sikukubali sikuongopa niliponena ya kuwa tunakimbia tunapohitajika kutembea na tunachutama tunapohitajika kunyooka...
Mambo gani hii sasa tunafwanya?
 
Sehemu ya nne;

Tazama basi tumekuwa wabaya mno hata tukipelekwa kwa shetani hatatupokea, atatimua mbio
Tumekuwa wachafu mno hata tukienda jehanam hatutapokelewa...maarifa yetu yamekuwa si kitu bali mizizi ya uovu, tumelemewa na kaput ya dhuluma, ubinafsi uzandiki uovu na unafiki

Kaya imemezwa na utapeli wizi ubakaji ubinafsi nk
Kaya imechoka inachechemea inaumwa lakini bana kubwa na mutu ile napatia sisi takwimu ile

Tazama viumbe hawa wa kaya hii wanaojifanya kuwa na furaha katikati ya dimbwi la ufukara mkuu, ni waathirika wa maamuzi ya hovyo kwa kisingizio cha dumekilasaa
Ushindi wa kishindwa, waathirika wa matokeo bandia, kaya haitamaniki tena
Hakuna tumaini tena na kila uchwao ni mwangwi wa vilio vya kukata tamaa

Wakati unakuja wa kuipigania kaya hii na kuiunda upya ili wana wetu na wana wa wana wetu waje wapate mahali pa kuhemea wasiwe wakimbizi watukumbuke na kutuenzi kwa kuipigania kesho yao ndani ya kaya yao tukuka....!!!

======WAKATI SI MILELE====
 
Back
Top Bottom