KENGE 01
JF-Expert Member
- Mar 12, 2021
- 1,770
- 4,394
Kenge kwenye moja na mbili
Hivi ni kweli MTAJI WA MASKINI NI NGUVU?? Kama ni kweli acha nikawe mwizi..Ngoja kwanza nikiwa mwizi si ZA MWIZI NI AROBAINI?? Amakweli NGOMBE WA MASIKI HAZAI,NA AKIZAA ANAZAA KILEMA nikomae hapahapa nyumbani
Potelea pote zikifika 40 nikakamatwa nikapigwa ntaachiwa tu na hata nikipata kilema UKIPEWA KILEMA,UNAPEWA NA MWENDO lakini hapana MCHUMA JANGA,HULA NA WAKWAO..Bora niwe dalali ntakula HALALI..kuliko kuwa Mwizi/Jambazi ntaeishia kula Mabanzi
Walakini MTEGEMEA CHA NDUGUYE, HUFA MASKINI Kama nikiendelea kuwategemea hawa ndugu watanisaidia kwa majungu na nikiwapa mgongo WATANIPAKA MAFUTA KWA MGONGO WA CHUPA.(sengenya)
Ni kweli MWISHO WA DHAMBI,AIBU aisee hata mkidinyana gizani Mimba na naradhi vitawaumbua tu si MFICHA MARADHI,KIFO HUMUUMBUA?? Hata mkipiga dili za dawa zikatiki NDEGE MJANJA,UNASA KWENYE TUNDU BOVU kabisaa na ujanja wake wote na ukiwa Tapeli ipo ile SIKU YA KUFA NYANI,MITI YOTEE HUTELEZA shwaaa..Au kibaka au Jambazi ipo siku HAMADI KIBINDONI,SILAHA MKONONI watakutia nguvuni yataanza MAJUTO,MJUKUU sasa unalaumu akili WHY!! "KWENYE MSAFARA WA MAMBA,KENGE HAWAKOSI
JASIRI HAACHI ASILI bora kujichanganya kupata mchongo kuliko kusikiliza viongozi na propaganda za UONGO tutachelewa sana kuwaamini viongozi wavaa Sifongo kwasababu ALIESHIBA,HAMJUI MWENYE NJAA,sasa CAG kaumbua madudu lakini msumeno wa Sheria hautowakata viongozi alafu eti SHERIA NI MSUMENO,HUKATA HUKU NA HUKU hapana bwana mnatudanganya tuuu.
Lakini kwenye michongo tutafte marafiki wanaoleweka kwasababu ukitokea Msala POTI wanasomba wote siku zote wanaamini NDEGE WAFANANAO HURUKA ANGA MOJA
Mkuu usidharau hustle za mtu, ATEMBEA NA JUA,HUJUA bora kupambana kwenye jua na mvua kwasababu AISIFUYE MVUA,HUMNYEA kuliko kumngoja aliejuu eti kisa ALIYE JUU,MGONJE CHINI
Eti SUBIRA YAVUTA HERI?? aisee nachanganyikiwa wakati navuta subira naskia NGOJANGOJA YAUMIZA MATUMBO lakini sasa ntakaaje kusubiri iyo subira sina mtaji Unakuta nina familia eti nikae nivute subira wakati MKAA BURE SIO SAWA NA MTEMBEA BURE?
Nazidi kuchoka kabisa KENGE MIMI NIMENASA KWENYE MKENGE..kila nikiangalia time inavyokimbia nami natamani nikimbizane na muda,Umri lakini ndoivo HARAKA HARAKA HAINA BARAKA na SIMBA MWENDA POLE NDIO MLA NYAMA
Mkuu kuna mshkaji wangu anatafuta ridhiki Mkoa A na Familia yake ipo Mkoa Z yaani "distance relationship" huwa kila uchwa mwamba anazozana kwenye simu na akinifata namwambia rudi nyumbani usalimie familia,Hutaweza kurekebisha familia ukiwa mbali nayo mzee baba FIMBO YA MBALI HAIMPATI MWEWE Akashtuka ASHAKUM SIO MATUSI lahaula akashika njia fasta akafunga safari kwa furaha na MCHUMIA JUANI,HULIA KIMVULINI
Aisee natamani kuendelea kuandika ila TAMAA MBELE,MAUTI NYUMA nikiendelea hapa NTAKATA KAULI lakini pia KILA LENYE MWANZO,LINAMWISHO kwasababu HAKUNA MAREFU,YASIO NA N'CHA
Wako mtiifu,KENGE
NAWASILISHA