Tungekuwa wapi leo bila Rais Samia?

Kwakweli bila Rais Samia sijui ata tungekuwa wapi maana duuuh,
Acha Ulevi kipi kizuri alichofanya
Amewapa matumaini
MAFISADI
Amewapa matumaini
MABEBERU
Amewapa matumaini
matapeli wa ccm
Amewapa matumaini wanamtandao

Amewaacha wanyonge wateseke na kuongeza bei za umeme
Amewavunjia mitaji wamachinga wako hoi taabani
Sasa nafuu yake iko wapi sijaiona mie
 
Huelewi maana ya mifano utanipotezea muda tu.
Hata Nigeria kwenye taarifa ya habari ya leo kuna issue ya inflation. Briefly nilitaka nikuambie inflation siyo kigezo cha ubora wa Kiongozi ndiyo maana hata Nchi zilizoendelea zina suffer
wengi humu ni watoto wa Primary wanafungua keshokutwa
hawajawahi kuvaa sandarusi na makatambuga
hawajawahi kupanga foleni ya sukari mgao kilo 1 Duka la kaya mpaka unaweka jiwe kwenye foleni.
leo Mama kaupiga mwingi hawaoni tofauti
awamu iliyopita kila kiongozi haachi Document au Briefcase ni kutumbuliwa au kupotezwa
 
Mkuu acha Viroba kurudi na sio Rombo tu
Bar zote ni 24hrs na Pool table ruksa
Mwendazake na Kolomije walifunga kila kitu eti watu wafanye usafi
mm nina shift za usiku mchana nipo free nikapumzike wapi?
sasa ndio Tanzania niijuayo
Kuhusu kufanya biashara mda wote naunga mkono,ule ulikuwa ujinga,hata siku ya usafi acha watu wafanye biashara na ukaguzi ufanyike atakayebainika hajasafisha mazingira hatua zichukuliwe ila sio kufunga biashara kwa masaa zaidi ya 5..

Mwisho kama kuna vitu vilizuiliwa kwa sababu vinaleta madhara kama viroba sio sawa kuruhusu inamaana hata madawa ya kulevya yatatuhusiwa sasa hii haijakaa sawa kabisa.
 
Ndugai alitumia uhuru wake kwa kutoa maoni waziwazi, nini kilimkuta? Usiegemee upande mmoja tu wa shilingi mkuu.
 
Sema kama sio Mungu Kwa sababu Mwenyezi Mungu ndio kamtoa Samia kama zawadi Kwa watanzania..

Samia mbele kwa mbele
Hakuna kitu kama hiki, unajipendekeza tu ndugu. Wewe toa maoni yako, ni wapi parekebishwe ili maisha ya watanzania yawe bora
 
Mkuu Mwananchi Huru usijali.. kama siyo SSH angetokea mwingine ambaye angefanya maajabu zaidi yake tu..
Jina la Kiongozi lisikupe taabu.. kuna ambaye angefanya maajabu usinge amini basi tu hakupata nafasi..
 
Mkuu Mwananchi Huru usijali.. kama siyo SSH angetokea mwingine ambaye angefanya maajabu zaidi yake tu..
Jina la Kiongozi lisikupe taabu.. kuna ambaye angefanya maajabu usinge amini basi tu hakupata nafasi..
Naomba nikujibu Mimi hivi,

"Ndio maana kibali kikawa kwa Samia coz Mungu anawajua wote ila akampenda zaidi Mama Samia, Tumuunge mkono"
 
Kwakweli bila Samia sijui ata tungekuwa wapi leo Watanzania, Kila nikiwaza naona giza, Mungu amlinde Mama huyu
 
Ni kweli maamuzi anayoyafanya Rais kisera kwa sasa, matunda yake tutayaona miaka 3-4 ijayo.

Ila wajinga wanataka waone leo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…