Tunduru: JWTZ wazima wizi na mauaji ya waendesha boda, amani yarejea

kumusoma

JF-Expert Member
Feb 3, 2014
566
889
Jeshi la wananchi wa Tanzania wilayani Tunduru, limezima mara moja matukio ya wizi wa pikipiki na mauaji ya waendeshaji wa hizo pikipiki na amani imerejea.

Taarifa za uhakika kutoka Tunduru zimeeleza na kuzibitishwa na wakazi wa wilaya hiyo, kwa mujibu wa taarifa hizo wimbi la wizi na mauaji ya waendeshaji pikipiki maarufu kama bodaboda lilitandanda wilayani hapo takriban miezi minne (Juni, Julai, Agosti na Septemba) ya Mwaka huu 2022 na kuleta hofu kubwa kwa wakazi wa Tunduru hususani wamiliki na waendeshaji wa pikipiki hizo.

Taarifa zimeendelea kuwekwa wazi kuwa, takriban vijana kumi na tano waliuwa na miili yao kuokotwa ndani ya mapori yanayozunguka wilaya hiyo huku wakiwa wamekwisha haribika sana.

Baada ya hofu hiyo kutanda kila kona ya wilaya ya Tunduru ndipo katika tukio la mwisho la wizi na mauaji hayo, kijana mmoja mdogo mwendesha boda alipouwawa iligundulika baadae kuwa kijana huyo ni mdogo wake afisa mmoja wa JWTZ.

Afisa huyo alipatwa na uchungu mkubwa sana na aliwatonya maafisa wenzake wa JWTZ kuhusu kadhia hiyo. Taarifa zinasema kwamba JWTZ waliweka wapelelezi wao makini kuzunguka wilaya yote ya Tunduru na viunga vyake na ndipo muuaji mmoja alipokamatwa.

Taarifa hizo zimesema kuwa muuaji huyo alikamatwa na jamaa wa JWTZ na kupewa mateso ya kutosha ndipo alipotaja wezi wote kwa majina na sehemu wanazotoka. Taarifa hizo zinasema mwizi huyo alifariki dunia baadae.

JWTZ waliendelea kuifanyia uchunguzi wa kina repori ya mwizi huyo ambaye yeye mwenyewe kabla ya kufariki alisema kuwa, aliuwa vijana nane wa boda boda.

Alipoulizwa na maafisa hao mahiri kabisa wa JWTZ kuwa anawauwa vipi hao boda boda, mwizi huyo ambaye kwa sasa ni marehemu alisema huwapiga nyundo kichwani na wao kupoteza fahamu ndiyo uwamalizia.

Wananchi wamewapongeza JWTZ kwa kazi nzuri sana waliyofanya na wamewaomba waendelee kuwalinda.
 
Jeshi ni mwiko kutumika dhidi ya raia, kazi ya Jeshi ni kulinda raia, Watanzania wajinga sana na low IQ.

Jeshi na wanajeshi wanakuwa trained kupigana vita dhidi ya adui aliye nje ya mipaka ya nchi na siyo raia wake eti wanakwenda kupiga bodaboda halafu mnasifu kwani Tanzania ni failed state hadi Jeshi lilinde amani?

Low IQ!
 
Jeshi ni mwiko kutumika dhidi ya raia, kazi ya Jeshi ni kulinda raia, Watanzania wajinga sana na low IQ.

Jeshi na wanajeshi wanakuwa trained kupigana vita dhidi ya adui slide nje ya mipaka ya nchi na siyo raia wake eti wanakwenda kupiga bodaboda halafu mnasifu kwani Tanzania ni failed state hadi Jeshi lilinde amani?

Low IQ
Wewe kenge ni mwizi wa bodaboda nini!?,umewahi kupoteza ndugu kutokana na vibaka,panya road, jambazi etc!???, Katika mapambano huwa inatumika silaha yoyote,kama polisi walishindwa kazi unataka jeshi liangalie tu?,nyie ndo huwa mnatetea wezi wanaouawa Kwa risasi eti ilitakiwa wapelekwe mahakamani, wakati mwingine bora kukaa kimya kuliko kuonyesha utaahira wako.
 
Jeshi ni mwiko kutumika dhidi ya raia, kazi ya Jeshi ni kulinda raia, Watanzania wajinga sana na low IQ.

Jeshi na wanajeshi wanakuwa trained kupigana vita dhidi ya adui slide nje ya mipaka ya nchi na siyo raia wake eti wanakwenda kupiga bodaboda halafu mnasifu kwani Tanzania ni failed state hadi Jeshi lilinde amani?

Low IQ!
Kazi ya Jeshi wakati wa amani, ni kusaidia taasisi za kiraia, hapo labda ujambazi muhamidhie maeneo mengine.
 
Back
Top Bottom