Tunduma: Ndugu wawili Wakatwa vidole vya miguu na Balozi wa nyumba 10 akiwashuku kwa wizi

The Sunk Cost Fallacy 2

JF-Expert Member
Nov 8, 2022
7,382
8,437
Vijana wawili ambao ni ndugu wamekatwa Vidole Vya Miguu na Balozi wa Nyumba Kumi kwenye Kata ya Mpemba wakishukiwa Kwa wizi.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi linamshikilia Kiongozi huyo wa Chama kubwa(CCM) Kwa kosa Hilo la Ukatili.

My Take
Kimaadili haifai Kwa Kiongozi au Mtu yeyote kujichukulia Sheria mkononi hata Kama wahusika wametenda kosa.

======

VIJANA wawili ambao ni ndugu wa familia moja Zephania Tinkson Mdolo (20) na Kelvin Tinkson Mdolo (17), wamedai kukatwa vidolegumba vya miguu na mtu aliyefahamika kuwa ni balozi wa nyumba kumi katika Kata ya Mpemba Mjini Tunduma mkoani Songwe kwa kuwatuhumu kuwa ni wezi.

Wakizungumzia tukio hilo lililotokea tarehe Novemba 03, mwaka huu vijana hao wanadai tarehe hiyo walikuwa kuchunga mifugo ndipo balozi aliwaita na kuwakata vidole na kuwabebesha nondo akidai kuwa ni wezi wa nondo.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Songwe, ACP Theopista Mallya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema wanamshikilia Samwel Eckson Mnkondya, anayedaiwa kuwa ni balozi, kwa tuhuma za kuwakata vidole vijana hao.

Nipashe
 
Watanzania ni wanafki,labda tuseme hawajaiba na wamefanya kosa lingine,ila kama ni wezi wameiba basi mwenyekiti hajakosea kama wale wanaochoma wenzao kama kuku choma
 
Back
Top Bottom