Mbeya: Wizi wa kipande cha nyama ya kuku na energy wasababisha Wananchi wawafukuze mtaani Balozi na Katibu wake

Mwanongwa

Senior Member
Feb 15, 2023
169
198
Wananchi wa Mtaa wa Halinji, Kata ya Nsalaga, Wilaya ya Mbeya wamewafukuza mtaani hapo Balozi pamoja na Mjumbe wake.

Balozi anayejulikana kwa jina la Mwandwanga pamoja na mjumbe wake Deo maarufu kama Tisa Tisa wametakiwa kuhama mtaani hapo kwa tuhuma za wizi.

Mjumbe huyo Deo alikamatwa kwenye Duka la mfanyabiashara mmoja mtaani hapo maarufu kama Mzambia akiiba kinywaji aina ya Energy na kipande cha nyama ya kuku.

Nje ya duka hilo pia kuna mjasiliamali anayejihusisha na uuzaji wa nyama za kuku.

Baada ya kukamwatwa kwa jamaa huyo Balozi Mwandwanga akaamua kwenda kumuwekea dhamana ndipo wananchi wakaamua kumjia juu balozi huyo na kumtaka ahame na mjumbe wake.

Mjumbe baada ya kuona mambo yamekuwa magumu akaamua kwenda kwa Mwenyekiti anayejulikana kwa jina la Zakayo ambaye pia ni Mchungaji wa Kanisa la Kilokole kwa ajili ya kumuomba ili akamuombee msamaha kwa Wananchi wa mtaa huo.


==========+===============


SERIKALI YA MTAA YAFAFANUA
Mwenyekiti wa Serikali Mtaa, Zakayo Job Chengula anasema “Hizo taarifa ni za ukweli lakini zinawahusisha Balozi na Katibu wake na si Mjumbe.

“Huko siku za nyuma kulikuwa na matukio mengi ya wizi, sasa Balozi Mwandwanga na wenzake pamoja na wananchi wakakutana bila kunishirikisha mimi na wakakubaliana kuwa yeyote ambaye atakamatwa akihusika na tukio la wizi anatakiwa kuhama Mtaa.

“Sasa kuna siku Msaidizi wa Balozi ambaye ni Katibu wa Mtaa akavuka mtaa, akaelekea upande wa mtaa mwingine wa Halinji akadaiwa kuhusika katika wizi wa vinywaji na hizo tuhuma nyingine zinazotajwa.

“Baada ya kubainika Wananchi wakakutana kikao na mhusika wakayamaliza baada ya kuomba radhi, lakini kwa kuwa walikuwa wameshatunga Sheria ya kwao wenyewe wakasema Katibu anatakiwa kuhama mtaa, pia Balozi anatakiwa kufukuzwa.

“Mimi nikawaambiwa sina uwezo wa kumvua Ubalozi, ikaidi waje watu wa chama ndio wakaamua kumvua ubalozi, pia Katibu naye akavuliwa Ukatibu.

“Baada ya hapo Wananchi wakawa wanataka wote wahama Mtaa kwa kuwa ni sheria iliyoamuliwa na Wananchi wenyewe Balozi alihusika kwa kuwa alikuwa akimtetea msaidizi wake.

“Hivyo, tukawashirikisha viongozi wa Kata, ikaonekana kweli Wananchi wamekosea kuhusu taratibu wa utungaji wa Sheria, lakini bado haiondoi uhalisia kuwa wale wahusika wawili wanatakiwa kuwajibishwa, mpaka sasa bado mchakato unaendelea kwa kuwa hatujafikia muafaka.

“Sheria haijabainisha kuwa anayetakiwa kuhama anatakiwa kuondoka na familia yake au wote wanatakiwa kuondoka, hivyo mchakato unaendelea.”
 
Kipande cha kuku na kinywaji tu ndio kinafukuzisha raia mtaa, kweli raia wamedhamiria
 
Back
Top Bottom