Ndo sababu wengi humu ni wajinga ingawa wanajiita Ma GT. Ukisoma maelezo ya Lissu ukalinganisha na michango ya wengi utagundua hoja za kijinga zilizojaa ushabiki badala ya mantiki.
Hakuna popote aliposema Lissu kwamba hakuna mwenye uwezo wa kujaza nafasi ya Katibu Mkuu ndani ya CHADEMA! Anachokisema Lissu ni sifa za mtu anaetakiwa kuwa Katibu wa Chama.
Dr. Slaa kuwa na uwezo haina maana alikuwa malaika asie na mapungufu, alikuwa nayo, tena mengi na ya hatari, kuna wakati tena sio mara moja mapungufu yake yalimezwa na uimara wa CHADEMA.
Ikumbukwe kwamba huyu hakuanzisha CHADEMA, alikuta chama kikiwa imara na ndio sababu kati ya vyama vyote alichagua kukimbilia CHADEMA baada ya kuchoshwa na ubabaishaji ndani ya CCM.
Ni sahihi kusema alikuja na ameacha mchango mkubwa ndani ya CHADEMA. Ni sahihi pia kusema CHADEMA kilimjenga na kumtangaza pia Dr. Slaa. Lkn mwisho wa siku hakuna aliye juu kuzidi chama.
Chama chochote hakiwezi kuwa chini mwanachama wake akawa juu, hili ni kwa vyama vyote.
Kumfanya mwanachama kuwa ni bora kuliko chama ndiko kulikoifikisha CCM hapa ilipo leo. Mfano mzuri tumeuona wakati wa uchaguzi, kwamba ilifikia mahali Mgombea Urais wa CCM kujitenga na chama, na kuwaomba wapiga kura wamchague yeye na sio chama chake!
Kwa umakini walionao CHADEMA, naamini atapatikana Katibu Mkuu makini kama ilivyokuwa kwa Slaa.
Muhimu watu wafahamu kwamba ni Mwenyekiti wa CHADEMA ndiye anapaswa kuwa makini kabla hajatamka jina la Katibu anayefaa. Sote tunaufahamu uwezo wa Mbowe, bila shaka atafanya hivyo kama alivyofanya kwa Dr. Slaa! Tusubiri!