Kwa sababu katiba iliyopo inampa Rais nguvu ya kutoa amri kwa jeshi la polisi
ingekuwa hana nguvu hiyo hata amri za kupiga marufuku asingeweza kutoa
Naongelea tu on the what extent Lissu anakuwa sometimes mwanasheria UCHWARAwewe unalako jambo Lissu hakamatwi kwa issues za Dr Slaa mbona unachanganya mada?
Lakini katiba haisemi hivyo ila polisi wanafanya hivyo kwa amri kutoka juu kumbuka.
Mkuu tusaidiane hapo, ni ibara ipi ya katiba inayosema raisi yuko juu ya sheria?Kuna wakati Baba wa Taifa alinukuliwa akisema "katiba hii ni nzuri sana, lakini akijitokeza kiongozi akaifuata watu watamuita dikteta "
Ndio kinachoonekana leo.
Upande wa pili wasije jisahau maana kufuata katiba ya nchi ni kiapo kinachompa mamlaka mkuu wa nchi kufanya chochote kwani ni yeye tu aliyeko juu ya sheria.
Chochote akifanyacho kijeshi ni amri.
Hili liwe funzo kwa upande wa pili kutokupuuza mambo ya muhimu kujadili kwani baadae itakuja kuwaghalimu sana .
Mkuu inakuwa kama bado hujanipata kidogo japo nakubalina na maoni yako kwa sehemu kubwa. Ngoja nikupe mfano mrahisi zaidi, leo hii polisi wamejipa mamlaka ya kutoa vibali, je sheria inasema polisi watoe vibali ili watu kukusanyika ama sheria inataka watoe ulinzi? Je hili linatekelezwa? Na kama halitekelezwi ni kipi kinachokupa imani kwenye katiba hiyo mpya wangeiheshimu? Hiyo katiba yangetekelezwa yale tu yasiyowabana watawala kwani ingechukua muda mrefu kubadili mindset za watawala.
Hivi tume huru ya uchaguzi inategemewa kuwasaidia wasio na dola au wenye dola?Na hata kina Lowassa,Sitta waliutaka urais
wangeshawishiwa kuwa tume huru ya uchaguzi itawapa nguvu popote kule watakapohamia....
nani anaejua leo tungekuwa wapi?
Shida kuu tuliyonayo sisi ni jeshi la polisi kuegemea upande wa chama tawala au tuseme kutekwa na wanasiasa na kujiingiza ktk siasa kwa kutumika kukandamiza upinzani kwa amri toka chama dola.Ndo maana nchi zinazojali demokrasia zimepiga marufuku polisi kupokea amri kutoka juu
na sisi pia tungetaka tungeweza
Polisi inakuwa ni marufuku kupokea amri
wafanye kazi kwa sheria tu zilizopo...
Labda hufuatilii tu siasa za Kenya, lakini hakuna unafuu wowote labda niseme mazingira yamebadisha watu wamekuwa na ufahamu zaidi lakini siyo katiba imewabadilisha. Ordinary Kenyan are still facing the same problems. Kwa mfano sasa hivi Kenyatta ameshawanunua baadhi ya wapinzani na anakifanyia chama chake kilichompeleka ikulu modification ya hali ya juu! Same wine, just a different bottle! Mimi mawazo yangu ni kuwa nchi zetu za kiafrika hata tuwe na katiba nzuri kiasi gani haitasaidia as long as wananchi wa kawaida hawajitambui na viongozi hawana willing ya kufanya kazi bali kuchumia matumbo yao1Kenya ya leo kisiasa ni nafuu kuliko Kenya ya Moi
sisi sasa ni kama tunafanana na Kenya ya Moi....
The Boss una hoja ya msingi sana, lakini kama umewahi kuisoma Rasmu hiyo uliyoiita ya "Sitta" utaona kuwa bado CCM walikuja na msimamo wa kumuonngezea Rais Madaraka. Hoja ya Tanganyika ilibeba mfumo tofauti na huu wa Rasmu ya Sitta yenye kutaka kuwa na Rais asiyehojika.
kwangu mimi tatizo langu na wapinzani wa CCM ni pale malengo yao yanapokwenda upogo kutokana na kukosa uzingativu katika hoja wanayoisimamia. Kwa mfano inaonekana ni kama vile Tundu Lissu anapambana na Serikali wakati ilitakiwa ionekane kuwa Lissu anapambana na serikali kwa niaba ya Watanzania wote.
kwa vyovyote vile CCM haiwezi hata kwa marungu kukubali Katiba inayopunguza madaraka ya Rais na kuyagawanya kwenye mihimili mingine, kwa kuwa chama chenyewe ni dhaifu sana kiasi kwamba bila ya kujiambatanisha na dola kitafutika kwenye Ramani ya Siasa Tanzania!!
Lakini @BAK,wako wapi hao watanzania mnaowatetea humu,mbona nchi iko kimya?!Wameridhika na hali ya mambo waacheni waendelee kula mlo mmoja kwa siku.Bado katiba hii yenye viraka chungu nzima pamoja na ubaya wake inaruhusu maandamano na mikutano ya vyama vya upinzani ambayo hakuna yoyote mwenye ruhusa ya kuwaamulia wapinzani nini kuzungumza kwenye mikutano yao na wapi pa kufanyia mikutano yao bila kujali kama wana mbunge kwenye jimbo husika au la. Na yeyote anayewazuia wapinzani kufanya hivyo anakiuka katiba ya nchi.
Lazima utakua Yes bossHakuna upinzani wa kisiasa, bali kuna Wanajazba kama Lissu!
Follow a wrong leader, and end up in a hole!
Mkuu kuna nchi ikithibitika tu kuwa Polisi wamepokea maagizo kabla ya kuchukua hatua
hao polisi wanaweza kuondolewa moja kwa moja na hata kupelekwa mahakamani
ndio mymain point here
ukiwabana polisi kisheria hawana jinsi
Hakuna upinzani wa kisiasa, bali kuna Wanajazba kama Lissu!
Follow a wrong leader, and end up in a hole!
Usipotumia akili na kuendesha siasa kwa mikakati endelevu, ndugu yangu utaandamana mpaka wamarekani wawahurumie kwa kuishiwa soli za viatu.Lazima utakua Yes boss
Kwa mfano unadhani wanatakiwa kutoa nini ili wapate hicho "kitu" wanachotaka?Huwezi pata kitu bila kutoa kitu UKAWA wanataka kupata kitu kikubwa zaid bila kutoa kitu that is naturally impossible