GE2025 Tundu Lissu: Ulimwengu unajua hakuna Kesi bali ni Siasa, nimepewa Kesi ili wasisumbuliwe na No Reforms, No Election

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Mwenyekiti CHADEMA Taifa, Tundu Lissu amesema "Mahakama yako vilevile iko kwenye Mahakama ya Umma, iko kwenye Kizimba cha Umma"

"Watu wa Taifa hili wanajua na Ulimwengu unajua hakuna Kesi hapa bali ni Siasa, ni mwaka wa Uchaguzi, na mwaka wa Uchaguzi Kiongozi Mkuu wa Chama cha Upinzani amekamatwa amepewa Kesi ya Uhaini si kwasababu ni mhaini ni kwasababa ya Siasa, ili Watu waende kwenye Uchaguzi wasisumbuliwe na No Reforms, No Election"

"Nchi yetu imechafuka kwasbababu ya Kesi hii"

Bofya hapa: Kujuya Yanayojiri Kesi ya Uhaini ya Lissu Julai 15, 2025 Mahakama ya Kisutu

Your browser is not able to display this video.
 
Tundu Lissu: Ulimwengu unajua hakuna Kesi bali ni Siasa, nimepewa Kesi ili wasisumbuliwe na No Reforms, No Election

Aache kutapata ulimwengu ndio nini, ulimwengu ndio umemtuma akinukishe? Aache kulialia alijitakia huyo lofa. Alishaajiandaa ndio maana ameshahamishia familia yake Ulaya na inahudumiwa na wazungu kwa gharama ya kukinukisha ili wazungu wachukue walichokubaliana. Huyo ni adui wa Taifa.
 
Adui wa Taifa n8 yule anaegiza watu watekwe na kuwawa ili yeye asikosolewe hata akiuza bandari zetu na kuruhusu ufisadi.
 
Na wewe ni adui wa nini ?
E
 
Lisu ni kiongozi wa Chama cha watu wa nje sio watanzania
Tofauti ya Chadema na vyama vingine vyote vya siasa Tanzania ni hixi

1.Vyama vingine vyote vya siasa vinawaamini watanzania .Chadema inawaamini watu wa nje zaidi.

2.Vyama vingine huhangaika kujinadi kwa watanzania wawaelewe kuwa wanaweza kushika dola.Chadema hujinadi zaidi kwa watu wa nje kuwa kinaweza kushika dola na kutaka wawaelewe

3.Vyama vingine vinaamini kuwa kura ya watanzania ndio inaweza kuwapa dola Chadema wanaamini kuwa mashinikizo ya kimataifa ndio yaweza kiwezesha kushika dola

4.Chadema haiamini vyombo vyetu vya sheria kama mahakama zetu na wanasheria wetu wanaamini zaidi wa nje tofauti na vyama vingine

5.Vyama vingine vinaamini katika kufanya propaganda za nguvu za kisiasa ndani ya nch kujijenga i wakati Chadema inaamini kufanya propaganda za kisiasa nje ya nchi zaidi kujijenga nje ya nchi na kwa watu nje

Ndio maana unakuta hata kesi ya Lisu Wanachadema na Lisu mwenyewe wakiona kuna watu wa nje ya nchi mahakamani huwa wehu kwa kufurahi kuwa watu wa nje wamo mahakamani hujisikia kama wako mbinguni.Ona Lisu hapo kaona kuna watu wa nje mzuka wa kiingereza umempanda ili wamsikie kwa Lugha ya kwao .Hapo kichwa chake na mdomo viko nje ya nchi haviko Tanzania

Wakati vyama vingine vyote vilivyobaki wala haviwahitaji wawemo mahakamani kukiwa na kesi zao

6.Chadema huamini zaidi kwenye mifumo ya kisiasa ya nje kama ya mataifa ya ulaya huko au Kenya nk wakati vyama vingine vyote huamini kuwa mifumo ya kisiass sio uniform kuwa lazima ifanane na nje

7.Chadema huamini zaidi kupata fedha kutoka nje wakati vyama vingine huamini zaidi kupata fedha kutoka ndani ya nchi

8.Chadema huviamini zaidi vyombo vya habari vya nje kuliko vyombo.vya habari vya ndani tofauti na vyama vingine

Kifupi Chadema ni foreign imported product kutoka nje ya nchi kwa manufaa ya watu wa nje wakati vyama vingine vyote vya siasa ni locally grown product ilizolishwa na watanzania wenyewe kwa ajili ya watanzania wenyewe
 
Ccm inahangaika na Lissu bure, bora upinzani wa Lissu kuliko upinzani wa ndani ya chama hicho unaozidi kuibuka kwa kasi ya ajabu kila uchao. Waachane na Lissu wakashughulikie nyufa mbaya chamani kwao
 
Madaraka yamekuwa matamu mpaka watu wamesahau kwamba wataondoka kama walivyokuja, wamesahau mafundisho ya madrasa na vipaimara ili wakue wakiijua dini, wamuogope na kumheshimu Mola kwa kutenda haki.

Walllah siku inakuja watanuka mbele ya dunia kabla hawajafa, wapambe wao watawakimbia na kujitenga nao, mioyo yao itaungua kwa uchungu wakitafuta muda WA kutubu na hawataupata.
 
Uko
Uko ya ngapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…