Tundu Lissu: Tutanyolewa bila maji suala la mchanga wa madini, tusikurupuke

Tumeibiwa ndio lakini ndivyo mikataba ilivyosainiwa.Kwamba mchanga usafirishwe nje kwa ajili ya processing. Mwenye jukumu la kuthibitisha ndani ya mchanga kuna nini ilikuwa ni vyombo vyetu vya kiuchunguzi lakini hawakufanya hivyo.Hivyo wao hawana kesi ya wizi kwa mujibu wa mikataba iliyopo.
Hivyo ushauri wa Lissu ni muhimu kisheria ili kufikia malengo yetu kama taifa, yaani kuivunja mikataba hii ya kitapeli.Hongera Lissu kwani pia umezingatia busara inayosema" haraka haraka haina baraka"
Wewe na mwenzako huyo nadhani mna matatizo kichwani. Hata kama mkataba umesainiwa kuruhusu mchanga kusafirishwa, na hata kama vyombo vyetu vimekagua, so what ... independent investigators nao wameleta ripoti tofauti. Kwa hiyo unataka tuachie wizi huu na mali iliyoibwa iende. Maamuzi lazima tuyachukue kuanzia sasa ili wajue watanzania hatutaki upuuzi. Mwambie mwenzako Lissu aende kumshauri kwanza watuhumiwa wa ufisadi waondoke chadema. Aache kudandia gari kwa mbele
 
Hii ndo ile inaitwaga mguu wa shingo mguu wa roho.....
Na tukijiondoa MIGA trust me hakuna investors yoyote ataefanya kazi na sisi maana ataku! hana uhakika na mali zake

Mfalme yuko uchi hakuna wa kumwambia woooote wanamsifia kapendeza
Na kweli kama wakija na malengo ya kutaka kufanya wizi wa mali zetu bora wapotelee hukohuko. Hatuwahitaji majizi. Wananchi wetu wwnyewe hali ngumu halafu tuendelee kuwanyenyekea majizi. Khaaaaa !
 
Kama alishauri na ushauri wake umetekelezwa malalamishi ya nini. Mbona anasema tutanyolewa bila maji. Ina maana amegundua ushauri wake ulikuwa mbovu
Hujanielewa. Alishauri lakini kwa sababu yeye ni upinzani ( Chadema) wakaona ushauri wake hauna maana. Karudia kushauri tena na anasema tusipokuwa makini tutanyolewa bila maji.
 
Bora awe anatoa ushauri kwenye legal aspects alizo specialize kuliko kuropoka ovyo; the common practice ya uwekezaji kwenye maliasili ni kwamba resource siku zote zinabaki kuwa mali ya host nation mwekezaji asset zake ni investment tu alizowekeza. Mchanga na madini ni mali ya Tanzania mwekezaji anafanya uwekezaji kwa niaba ya nchi (kwa malipo ya kufidia gharama zake na kutengeneza faida) serikari ina haki ya kuhakiki kama inapata fair deal kutokana na kinachozalishwa kwa mujibu wa sharing agreements.
Hivi tunafahamu lissu ame specialize katika nini???Ninavyojua lissu alifanya utafiti katika mgodi wa Bulyankulu miaka ya 1996 na kuwahi kufunguliwa kesi akitetea wachimbaji wadogo waliodhaniwa kufukiwa wakiwa hai ili mwekezaji apewe mgodi. Eneo hili alilifanyia kazi vya kutosha kabla ya kuendelea kufanya kazi marekani, akiendelea na tafiti za namna hii.Kwa hiyo Lissu anafahamu hii mikataba ya madini na consequences zake kisheria
 
Huyu sasa atakuwa Mh: Willy anahusika, aisee hii inshu hii inaenda hadi kwenye mizizi, Magu the Ngosha kaza moyo baba waweze kumkuta hata mzazi wako wa jinsia tofauti yupo uchi halafu inakubidi umtazame, inahitaji moyo wa chuma aisee la sivyo waweza tizama pembeni na kupita ukijifanya hujamuona.
 
Tundu lissu anashindwa kuelewa kuwa kudeclare kiasi cha madini tofauti na kilichopo katika makontena ni kuvunja mkataba!?...hivyo automatically Acasia wamekuwa wakivunja hiyo mikataba ambayo tobo lisu anadhani itatushinda.
Siyo kuelewa lisu yeye kila cku ni mpingaji kwa hiyo hata serekali ifanye mema ya kiasi,ivunbue madudu kiasi gani bado atapinga na kutaka kuleta ushauri tu
 
Hivi nchi hii ingetokea vita ya wenyewe kwa wenyewe jamaa wataendelea kuchimba madini au watakimbia na kuacha mashimo tujizike humo?
 
Kama huelewi vitu au mambo,si vibaya ukasoma post angalau upate mwanga na ujue nn kinazungumzwa.sio unaongea tu ili na ww tujue unaelewa.toa hoja watu wasome ili akilizao zipate cha kufikiri,haya lisu hawezi wewe unaweza nini?
Hawezi!!?Soma post uelewe usikurupuke
 
Tundu lissu anashindwa kuelewa kuwa kudeclare kiasi cha madini tofauti na kilichopo katika makontena ni kuvunja mkataba!?...hivyo automatically Acasia wamekuwa wakivunja hiyo mikataba ambayo tobo lisu anadhani itatushinda.
Mheshimiwa, kwa mujibu wa mkataba wao declaration halali ni ile inayotokana na assaying iliyofanywa na chombo cha serikali kiitwacho TMAA, kwa hiyo hadi sasa Acacia hawajasema uongo, kisheria. Ingekuwa TMAA wametoa jibu halafu Acacia wakafoji, au kama TMAA wakikana viwango vilivyoandikwa kwenye containers, hapo kwa mujibu wa mkataba ndipo watakuwa wamedanganya. Lakini hadi sasa, reference figure ambayo kimkataba ni halali ni ile iliyoandikwa na TMAA na kukubaliwa nao kabla ya kufunga (seal) container. Na mkataba wao unasema kama hiyo figure inabishaniwa, basi kuna arbitration sample ambayo inapaswa kupelekwa kwa independent lab, in the presence of representatives from both Tanzania Government and Acacia. Kilichofanyika hadi sasa ni kuwa mlalamikaji (serikali yetu) amejichukulia sheria mkononi akachukua samples zake bila kuwepo uwakilishi wa mlalamikiwa, na amezifanyia analysis kwenye lab yake mwenyewe, siyo independent, kinyume na mkataba. Sijui mnanielewa wakuu?

Wametuibia kweli, lakini tumechukua hatua ambazo zitatuumiza zaidi. Tumempa mwizi wetu nafasi ya kutupiga zaidi badala ya sisi kumpiga.
 
Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu ameibuka na kuishauri serikali jambo la kufanya kutokana na matokeo ya uchunguzi wa mchanga wa madini uliofanywa na kamati ilyoundwa na Rais John Magufuli.

Tundu Lissu

Tundu Lissu anasema Tanzania ni mwanachama wa 'The MIGA Convention' hivyo ukiwa mwanachama ukachukua mali za wawekezaji wao utapelekwa kwenye mahakama za kimataifa na kwenda kushughulikiwa huko, hivyo Tundu Lissu ametoa ushauri wa namna nzuri ya kushughulika na watu

"Sisi Tanzania ni wanachama wa kitu kinaitwa 'The MIGA Convention' Multilateral Investment Guarantee Agency ya benki ya dunia, ukiwa mwanachama wawekezaji wakileta mali zao kwako, ukichukua mali zao kama walivyochukuliwa mali zao namna hii utapelekwa kwenye mahakama zao za kimataifa unaenda kushughulikiwa huko, tumesaini mkataba wa ulinzi wa wawekezaji na mataifa wanayotoka wawekezaji hao Marekani, Canada, Uingereza wote ni mabosi wakubwa makampuni ambayo Rais ameyakamatia mali zao yanatoka kwenye hizi nchi tuna 'bilateral investment treaties ambazo zinalinda mikataba hii" alisema Tundu Lissu

Makontena ya mchanga wenye madini yaliyozuiliwa bandarini

Tundu Lissu anasema hili suala tusipokuwa makini nalo linaweza kuleta matatizo makubwa huku akimtaja muhusika wa mikataba iliyolifikisha taifa katika hasara iliyobainika katika uchunguzi huo.

"Rais anajiingiza kwenye mgogoro mkubwa, akimkamata Dalali Kafumu peke yake, tutamwambia kwanini siyo Gray Mwakalukwa mikataba yote hii imeingia wakati wa Mr. Gray Mwakalukwa, kwanini siyo Daniel Yona, kwanini siyo Jakaya Kikwete sababu alikuwa Waziri na mimi nina mkataba wa Bulyankulu na kwanini siyo mawaziri wote, kwa sababu mikataba iliingiwa wakiwa mawaziri" alisema Tundu Lissu

Rais Magufuli akipokea ripoti ya kamati

Lakini mbali na kusema yote hayo Tundu Lissu alitoa ushauri wake katika suala hilo...

"Kama unataka kufanya haya unayoyafanya elewa hali halisi ilivyo, tatizo liko wapi kama tatizo ni kwamba tunapata mapato kidogo na kweli wanatupiga kweli kweli ila kama utaka kufanya mambo kweli kweli kajiondoe kwanza MIGA ili hao wawekezaji wasikushtaki kwenye hizo mahakama za huko, maana wakikushtaki kule unanyolewa bila maji, hakuna ndege ya Tanzania itakanyaga hizo nchi wataikamata, hakuna hela tutaweka kwenye nanii za kimataifa watazikamata, kwa sababu tunavunja mikataba ya kimataifa inayolindwa na sheria za kiwekezaji za kimataifa, kwa hiyo anzia huko juu ukimaliza mikataba ya kimataifa, njoo kwenye mikataba kati ya nchi na nchi ondoa hiyo mikataba ukishaondoa hiyo hushtakiki nje, baada ya hapo njoo ndani sababu bado unaweza kushtakiwa ndani" alisisitiza Tundu Lissu

Hivi mkataba unasemaje,unasema makampuni ya madini ya danganye kwa ku-declare kiwango cha madini tofauti na kile kilichopo! I don't think so.Nadhani haya makampuni ndiyo yaliyoanza kuvunja mkataba. They have a case to answer.

Hata hivyo ushauri wa Lissu sio mbaya, ufanyiwe kazi.
 
Tundu lissu anashindwa kuelewa kuwa kudeclare kiasi cha madini tofauti na kilichopo katika makontena ni kuvunja mkataba!?...hivyo automatically Acasia wamekuwa wakivunja hiyo mikataba ambayo tobo lisu anadhani itatushinda.
Nawapenda wa tz mlivyo na akili
 
Mheshimiwa, kwa mujibu wa mkataba wao declaration halali ni ile inayotokana na assaying iliyofanywa na chombo cha serikali kiitwacho TMAA, kwa hiyo hadi sasa Acacia hawajasema uongo, kisheria. Ingekuwa TMAA wametoa jibu halafu Acacia wakafoji, au kama TMAA wakikana viwango vilivyoandikwa kwenye containers, hapo kwa mujibu wa mkataba ndipo watakuwa wamedanganya. Lakini hadi sasa, reference figure ambayo kimkataba ni halali ni ile iliyoandikwa na TMAA na kukubaliwa nao kabla ya kufunga (seal) container. Na mkataba wao unasema kama hiyo figure inabishaniwa, basi kuna arbitration sample ambayo inapaswa kupelekwa kwa independent lab, in the presence of representatives from both Tanzania Government and Acacia. Kilichofanyika hadi sasa ni kuwa mlalamikaji (serikali yetu) amejichukulia sheria mkononi akachukua samples zake bila kuwepo uwakilishi wa mlalamikiwa, na amezifanyia analysis kwenye lab yake mwenyewe, siyo independent, kinyume na mkataba. Sijui mnanielewa wakuu?

Wametuibia kweli, lakini tumechukua hatua ambazo zitatuumiza zaidi. Tumempa mwizi wetu nafasi ya kutupiga zaidi badala ya sisi kumpiga.
Kazi kweli kweli.
 
Lissu badala ya kwenda kwao kuhimiza watu wajenge nyumba za bati waache kulala na mbuzi na ng'ombe anakubali kupokea rushwa kuangamiza watanzania na wizi wa wazi wazi kabisa.. wamedanganya hapo tayari weshavunja mkataba..hatuibiwi tena.
 
Back
Top Bottom