Tundu Lissu: TLS tumeomba mwaliko wa Magufuli tukampongeze Ikulu

haahaa lissu noma.....
Kesha shinda urais sasa unadhani anapalilia nini, lazima atafute mbinu ya kukaa meza moja na wafalme! hahaha, halafu akifika huko atamuambia rais, mkuu zile zilikuwa kampeni tu, wacha tule kuku, wewe kaza buti ili watz wanyooke, ahahaha, chezea siasa weye
 
Kesha shinda urais sasa unadhani anapalilia nini, lazima atafute mbinu ya kukaa meza moja na wafalme! hahaha, halafu akifika huko atamuambia rais, mkuu zile zilikuwa kampeni tu, wacha tule kuku, wewe kaza buti ili watz wanyooke, ahahaha, chezea siasa weye
Kibatari wewe
 
Dar es Salaam. Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Tundu Lissu amesema uongozi wa chama hicho umemwandikia Rais John Magufuli kutaka kukutana naye Ikulu ya Dar es Salaam kwa ajili ya kujitambulisha rasmi na kufanya mazungumzo.

“Ni mkutano baina ya Rais na rais,” alisema Lissu katika mahojiano na gazeti hili alipotembelea ofisi za Mwananchi Communications Limited (MCL) inayozalisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti.

Lissu, ambaye pia ni mbunge wa Singida Mashariki, alichaguliwa kuwa rais wa chama hicho mapema mwezi huu, na Rais ni mmoja kati ya viongozi kadhaa waliowaandikia kuomba kukutana nao.

Aliwataja wengine kuwa ni Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Jaji Mkuu, Mkuu wa Jeshi la Polisi na marais wawili wastaafu, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete.

Alisema tayari Jaji Mkuu ameshakubali ombi lao.

Kuhusu ombi lao kwa Rais Magufuli, Lissu alisema atatumia fursa hiyo vizuri, iwapo watakubaliwa.

“Nikifika nitaanza kwa kumshukuru Rais kwa kuwafundisha Watanzania maana ya utawala wa sheria, uhuru wa mawazo, uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa Mahakama na Bunge,” alisema Tundu Lissu.

Lissu alifafanua baadaye kuwa Rais Magufuli amefumbua wengi macho kujua vitu hivyo kutokana na jinsi anavyoendesha nchi, ndio maana atamshukuru.

“Tumeomba appointment na Rais Magufuli tuzungumzie utawala wa sheria,” alisema Lissu.

“Leo ni Jumatano? Barua tulimpelekea Jumatatu. Tutaenda kujitambulisha na kuzungumzia utawala wa sheria na mwelekeo wa taifa hili. Ni between presidents. Tuna imani kwamba atatukaribisha. Tutamweleza maoni yetu, pale tunapoona amekosea tutamweleza na pale anapoona tuna matatizo atatueleza.”

Alisema wanajua kuwa Rais ana shughuli nyingi, lakini wanatarajia atatenga muda kwa ajili yao.

“Tunafahamu yuko busy, lakini kama anaweza kuangalia Shilawadu, atakuwa na muda hata nusu saa au saa nzima ya kuongea na kiongozi wa chama cha mawakili wa Tanganyika,” alisema.

Lakini akaonyesha jinsi alivyopania kueleza matatizo anayoyaona katika utawala wa sasa.

“Nakwenda kumpa vidonge vyake, kabisa! Wala sitammezea. Nitamwambia kwa heshima zote kwamba Mheshimiwa Rais, sisi kama mawakili wa Tanganyika tuna wasiwasi mkubwa na mwelekeo wa Serikali yako,” alisema.

“Wamenituma nikueleze mwelekeo na matendo ya Serikali yako. Unatawala vibaya, nje ya Katiba, wameniambia nije nikwambie ujirekebishe. Nakwenda kumsimanga tu. Halafu tukitoka pale namwambia Mheshimiwa Rais tupige picha, wajue nilikuja.”

Alisema iwapo Rais hatakubali kuwaalika, ataueleza umma.

“Atakuwa amenirahisishia, nawaita waandishi wa habari nawaambia. Tulimwambia Bwana mkubwa tumsalimie na tumweleze kwamba haturidhiki na utawala wake, yeye amekataa amekimbia,” alisema Lissu.

Hata hivyo, mkuu wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Gerson Msigwa amemtaka Lissu kusubiri taratibu za kiutawala.

Msigwa alimshangaa Lissu kwa kitendo chake cha kuzungumza katika vyombo vya habari ilhali anajua utaratibu wa kiutawala.

“Yeye kama ameandika barua barua si asubiri majibu? Muulizeni inakuwaje kabla hajapewa majibu anaenda kutangaza katika vyombo vya habari? Si asubiri utaratibu wa kiutawala,” alisema Msigwa.

Lissu alisema ofisi nyingine walizopeleka maombi kama hayo ni ya Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Jaji Mkuu, Mkuu wa Jeshi la Polisi na marais wastaafu, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete.

Kwa upande wake, Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Paramagamba Kabudi alisema hana taarifa juu ya barua hiyo kwa kuwa tangu ateuliwe hajaingia ofisini.

“Nimekuwa katika vikao vya Kamati za Bunge vinavyoendelea mjini Dodoma, hivyo sina habari hiyo,” alisema.

Hata hivyo, Profesa Kabudi alisema inawezekana ni kweli rais huyo wa TLS amewasilisha barua hiyo ofisini kwake lakini yeye bado haijamfikia.

Chanzo: Mwananchi
 
Mwanasheria wa Chadema na rais wa TLS akiwa anahojiwa na radio Times FM akijibu ni jambo gani ambalo wanaweza kumpongeza rais Magufuli amedai yapo na TLS wameomba mwaliko wa rais ili wakampongeze.

Tundu Lissu amedai rais ametenda mengi na mengine ni mazuri na pia anastahili pole kwa kuwa kazi ya urais ni kazi ngumu, akisema alimuona jana alikuwa amechoka

Pia amewaambia wananchi kuwa wasiipe TLS nguvu kubwa kwakuwa TLS haisimamii mahakama wala haiteui majaji na hivyo sio wategemee kuwa kesi za uonevu , au kucheleweshwa kwa kesi ni jambo ambalo linaweza kutatuliwa na TLS pekee


Duh!
Wazungu wa "wingereza" husema...."water will finds its level"...
Kadri maji yanavyotuama na kupata kina chake stahiki, ndivyo wajumbe ktk maji hayo wanakomaa ktk kweli na uhalisia, na wataanza ishi kulingana na "kina chao astahiki, na si vinginevyo", na kuachana kabisa na "alinacha" zilizotangulia...
....na nadhani, hakutakuwa na nafasi kwa raisi wa TLS kufika ikulu, bila kupita kwa gwiji, "simba marara" wa tasnia ya sheria, "Tanzania muzima"... mheshimiwa Prof. Kabudi...huo ndo mlango!
 
Ameanza kumsifia tena!!????
Haya bhana
Anamsifia kwa jitihada zake za kupambana na kuumiza wengine bila mafanikio,rejea urais wa TLS nini kilijili, na ni jambo la busara rais mwelevu kukutana na rais kimeo pengine mmoja anaweza kukopy ya mwenzie
 
Nashangaa Tundu Lissu alivyomwita Mhe. Rais Magufuli kuwa ni rais wa ajabu aijawai tokea!!!!. Sasa kulikoni amuandikie barua ya kutaka kuonana nae Mhe. Rais baada yeye kuchagua kuwa rais wa TLS.
Vipi km ameshagundua km rais wa ajabu atake kuonana nae??? Je kuna umuhimu wa kuonana na rais wa ajabu ???
 
Nashangaa Tundu Lissu alivyomwita Mhe. Rais Magufuli kuwa ni rais wa ajabu aijawai tokea!!!!. Sasa kulikoni amuandikie barua ya kutaka kuonana nae Mhe. Rais baada yeye kuchagua kuwa rais wa TLS.
Vipi km ameshagundua km rais wa ajabu atake kuonana nae??? Je kuna umuhimu wa kuonana na rais wa ajabu ???
adb7ec27d04900d8e2ba8c11a3a94898.jpg
Huna maana nenda huko
 
Back
Top Bottom