Tundu Lissu: TLS tumeomba mwaliko wa Magufuli tukampongeze Ikulu

Mwanasheria wa Chadema na rais wa TLS akiwa anahojiwa na radio Times FM akijibu ni jambo gani ambalo wanaweza kumpongeza rais Magufuli amedai yapo na TLS wameomba mwaliko wa rais ili wakampongeze
Tundu Lissu amedai rais ametenda mengi na mengine ni mazuri na pia anastahili pole kwa kuwa kazi ya urais ni kazi ngumu, akisema alimuona jana alikuwa amechoka

Pia amewaambia wananchi kuwa wasiipe TLS nguvu kubwa kwakuwa TLS haisimamii mahakama wala haiteui majaji na hivyo sio wategemee kuwa kesi za uonevu , au kucheleweshwa kwa kesi ni jambo ambalo linaweza kutatuliwa na TLS pekee

Ahahahahaha
 
Lissu bana!ameomba mualiko kwa 'dikteta' ili akampongeze 'dikteta' kwa kazi nzuri anayoifanya!!
Hawa ndio wanasiasa wetu
 
Kumbe anajua TLS ni nothing kwenye muhimili uliojichimbia zaidi!!!

Tuliwaambia humu manyumbu kuwa hiyo TLS haina lolote.

Ni kachama kadogo mno ambako kalipewa kiki ya muda mfupi na rais mwenyewe pamoja na Mwakyembe.

Lakini hako kauchaguzi kao walikokafanya wiki ilopita na hizo shamrashamra zake ungedhani ni ujio wa pili wa yesu kumbe hamna lolote.
 
Naona Lissu analainisha maneno kidogo ili rais apate moyo kuwaita Ikulu

Siasa ni tamu sana.
 
Huyu anakuja na ujanja gani kwa haya...mmmmmh

Nitamsikiliza nijue kama kamaanisha au mmmmh

Hapa kazi tu
 
Kazimisi juisi za mkwere eeh, kule ni maji ya kunywa tu hamna kingine siku hizi.

Pole sana barafuyamoyo, Lissu umjuaye hayuko kama wewe unayetegemea kupost pumba za kujipendekeza kwa watawala ili mkono wako uende kinywani na wanao waende chooni. Huyo ni viwanja vingine, juisi ambayo wewe unaona kuwa ni dili, mwenzio ni kitu cha kawaida sana.

Nimeziona post za namna hii mara nyingi sana, hao wanaokwenda ikulu ni viongozi kutoka vyama vya upinzani ambao hawapandi daladala kama wewe, ebu fikiria gharama ya kununua mafuta ya gari kutoka atokako hadi kufika ikulu haitoshi kununua juisi mahali kokote aliko? Au juisi ya ikulu ndio yenye ladha nzuri kuliko juisi zote? Ushabiki mwingine ni shida tupu!
 
Back
Top Bottom