Tundu Lissu katika hilo la kuwataja waliomshambulia kazingatia ushauri aliopewa na "wadau" wake.Hakika ilikuwa ni kujiweka mahali pa hatari sana kusema kuwa waliomshambulia anawajua wakati bado yupo juu ya kitanda hospitalini,ilikuwa ni hatari kwake na kwa dereva wake.
Tunashukuru kuwa sasa kwa kinywa chake,ametujengea picha kujua "ushahidi wa kimazingira" wa wahusika.Nyumba ni za serikali,majirani zake ni viongozi wa bunge na serikali,huku Naibu Waziri na kule Naibu Spika.Tena katika eneo lenye CCTV masaa 24.
Ni ajabu kuwa mpaka sasa,hata jirani yake Naibu Spika hajafika kumjulia hali mbunge,kiongozi mwenzake wa bunge na jirani yake nje ya bunge.Tulisema hapa,matibabu sio hisani bali ni haki yake,lakini sababu kuna muhimili mmoja umejichimbia chini zaidi,muhimili mwingine unaongozwa tu kwa "remote control".Aibu sana
Ni bahati mbaya kuwa hata wale walio na propaganda,wametoa video ya Makamu wa Rais na Lissu katika lile eneo ambalo Lissu anamwambia VP mwambie Rais nashukuru sana,lakini wakaacha pale alipomuuliza "Ni kweli Rais kakutuma au umepitia tu baada ya kuja kwenye sherehe za kuapishwa?".Kama kakutuma,basi mwambie Mh.Rais nashukuru sana.
Lakini hawajaeleza Pindi Chana aliulizwaje?Kwamba toka September 07 mpaka leo ndio unakuja??Lissu amekuwa very technical kwenye haya mahojiano.Jambo jema...
Ahadi ya kijasiri ni ile ya kusema atarudi na kuongeza nguvu zaidi,maana upendo wa Watanzania kwake imekuwa ni deni kubwa.Lissu na kauli zake,amenirudisha tena JF
Mbowe ndio ameshushuka sio au?
Halafu ndie anayejua wenzake waliohusika.
Mara paap Lisu katimkia CCM...900 itapendeza bavicha wote wataharisha siku hyo 😀😀😀😀😀
Taarifa hutolewa kwa utaratibu upi?Maswa 1 , Siyabonga101 , dudus,
Lissu alisema wiki tatu kabla ya shambulio hilo alilalamika hadharani kwamba anafuatiliwa kila anapokwenda na siku moja aliwasimamisha watu hao katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro na kuwauliza sababu za kufanya hivyo.
“Niliwauliza kwa nini wananifuata na kama kuna mtu kawatuma, mwambieni mimi si mhalifu. Lakini sikupewa ulinzi wowote,” alisema.
Taarifa hutolewa kwa utaratibu upi?
We unamsemea?Mh Lisu katumia busara, kusema hawa fahamu hao watu na hiyo yote kupunguza maswali na shauku ya watu kutaka kujua. Mh Lisu anajua ataanzisha kitu kipya akisema anawafahamu. Ngoja arudi tutajua mbivu na mbichi
Mnataka aseme anawafahamu ili wamrudie
Sasa anko ake sabrinaHuwezi kusema unawajua bila ya kutoa ushahidi unaothibitisha unachokidai.
Mimi naamini kweli hawajui hao watu.
Ila pia naamini kuna anaowahisi kuwa ndo wahusika, kwa namna moja ama nyingine.
Suala la kujua linahusiana na ushahidi na uthibitishaji. Sasa anaweza kweli kuthibitisha endapo atasema huyu na yule ndo wahusika? Ngumu sana!
Anaeleza, Tundu Lissu maneno yanayo fikirisha.
"Kimawazo nadhani sijabadilika sana, Lissu wa kabla ya September 7 na Lissu wa Leo kimsimamo wa kisiasa hajabadilika kabisa. Lazima tupiganie demokrasia, hiyo ndiyo salama yetu . Tuwe na utawala wa kidemokrasia unao jali haki za binadamu, tuwe na utawala wa sheria, tuwe na mfumo wa uongozi unaojali maisha ya wananchi, unao wajibika kwa wananchi au kwa wawakilishi wake na huu ndio msimamo wangu unajulikana na bado upo vile vile"
Ujumbe kutoka kwa mkewe, Alice Lissu.
"Ujumbe wangu, Tundu siku zote aendelee kuwa Tundu tu. Tundu wa kabla ya tukio na baada ya tukio awe ni Tundu niliyemjua siku zote.
Nini Maoni Yako?
Ndimi, Noel Shao
[HASHTAG]#mjenziWaTanzaniaMpya[/HASHTAG]
Sasa anko ake sabrina