Tundu Lissu: Polisi wa Tanzania hawana mamlaka ya kunihoji nikiwa Kenya au kwingineko nje ya mipaka ya Tanzania

KUNA VITU KADHAA BADO VINANITATIZA

1. Kuhusu serikali kutomtembelea Lissu hapo awali.
Sasa tufanye nyumba ya jirani mtoto wao anaumwa sana. Wazazi wa mtoto wamepiga ramli na kuambiwa kuwa bibi kizee jirani yao ndie mchawi aliemroga mtoto.

Taarifa zimezagaa kijiji kizima na yule bibi amezisikia.

Hivi mnaweza kugeuka na kumlaumu yule bibi kizee eti kwa nini hajaenda kumjulia hali mgonjwa au hajampelekea hata uji tu?


2. Kuhusu polisi wa Tanzania kumhoji Lissu akiwa Kenya.
Lissu sio mshukiwa wa shambulio lake yeye mwenyewe. Kwanini awe mbishi kuhojiwa na polisi wa kitanzania popote pale duniani?

Fikiria:
Wezi wamevunja nyumba yako, wakakufunga kamba, wakaiba kilakitu wakati unawaangalia.

Wakati upo London kwa shughuli zako binafsi polisi wa Tanzania wakakuomba waje wakuhoji ili wapate maelezo yako kuhusu wezi wako pamoja na mali zako zilizoibwa.

Hivi utakataa kukutana nao na badala yake utataka uhojiwe na MI5 au Scotland Yard wa Uingereza?

Uhalifu ufanyike Tanzania, wewe ndio shahidi (eye witness) mkuu, lakini unataka uhojiwe na polisi wa nchi ya kigeni?

Makubwa haya.
 
IGP hajui taratibu za kumhoji mtu ambaye yupo nje ya Tanzania aibu kubwa sana.
Hadi sasa Mwanasheria Mkuu wa Tanzania hajamwomba Mwanasheria Mkuu mwenzake wa Kenya ruhusa ya mimi kuhojiwa na Polisi wa Kenya juu ya shambulio hilo kama inavyotakiwa na sheria husika za nchi yetu.
 
hana imani kabisa na jeshi letu la polisi,ila wafanye kwasababu wanatimiza wajibu wao
 
kuna haja ya kupeleka watu shule kwa mara ya pili maana sio kwa umbumbumbu hu
 
Matamko ya viongozi wetu huku yanatia shaka mimi Jirani yangu ni hapa in police aliniuliza Hugo alietoa hilo tamko la kutuma makachero Kenya anajua maana ya kuundwa Interpol au hakuna analolijua...anawezaje kusema police wa Nchi moja aende akafanye kazi ya kipolice Nchi nyingine...
 
Tundu ndugu na rafiki yet tunakupenda sana. Hata tusiojua kusali tunasali kwa ajili yako. Mungu akupe nguvu na moyo wa kuvumilia yote na awalipe waliokudhuru stahiki zao.
Pole sna. Upone haraka
 
Pasco police wetu hawakuwa na haja na huyo kijana (dereva). Wamemtafuta siku tatu baada ya tukio tena kupitia vyombo vya habari !!
Ukumbuke huyu kijana alikuepo kwenye tukio, hospital na hata Airport kumsindikiza bosi wake!! Na kote huko police walikuepo wakihangaika na wafuasi wa CDM wasisogelee tukio!!
After all CCTV footage ziko wapi?! Upelelezi wa kitoto
 
Propaganga za kijinga
 
cc: Lizaboni
Ruttashobolwa
Pascal Mayalla
stroke
 
 
Hujui kitu!! Mambo ya kipelelezi waachie wapelelezi wewe fanya yanayokuhusu!
 
Mara hoo jeshi la polisi kwa nini halitaki kunihoji nikasema yote yaliyotokea. Sasa jeshi hilo limeamua kuja, unadai kuwa halina mamlaka ya kukuhoji ukiwa nje ya mipaka ya Tanzania! Sasa, mbona haueleweki? Si useme tu ukiwa hapo ili sisi watanzania tujue ukweli. Sasa kama siyo jeshi la polisi kukuhoji, unataka uhojiwe na nani?
 
Huo ndio utaratibu wa kisheria, kwani haiwezekani?? Umeweka wapi akili yako, japo ni ya QT.
Mkuu swala ni warudishwe Tanzania au Tanzania wawafuate hukohuko kuwahoji. Hakuna cha Kenya wamuhoji dereva wa lisu au lisu then watume ripot.
 
Mkuu Impongo, kwanza naungana na wewe kuwa utafutwaji wa dereva wa Lissu ni kama mtuhumiwa, ndio maana nikasema humu hao makachero waliotumwa Nairobi, sio kumhoji, bali kumsomba, mzobe mzobe.

Shida kuhusu tukio hili, haiko kwa polisi tuu, any reasonable man would wish to hear that side of the story especially the miraculous escape ya ki Jemsi Bond ya dereva huyo, risasi zaidi ya 40 zimepigwa, yeye akiwa dereva, akamvuta Lissu, akwambaza kiti cha dereva, akatoka nje kumiujiza, akaingia chini ya gari, huku risasi zinarindima. Yeye hakuna hata risasi moja iliyompata!. Kwa macho ya kawaida huyu ni zaidi ya Comandoo, kwa jicho la kipolisi huyu ni zaidi ya shuhuda muhimu, na jinsi viongozi wa Chadema wanavyompa protection, kumlisha, kumtunza ugenini, leaves much more to be desired, ndio
maana sisi ma open minded, don't rule out any options even an inside job of friendly fires.

Kanisome hapa

Shambulio la Lissu: Wajue Wasiojulikana Watakaojulikana na 'Wasiojulikana' Ambao Kamwe, Hawatajulikana!.

Paskali
 
Mkuu swala ni warudishwe Tanzania au Tanzania wawafuate hukohuko kuwahoji. Hakuna cha Kenya wamuhoji dereva wa lisu au lisu then watume ripot.
'Hadi sasa Mwanasheria Mkuu wa Tanzania hajamwomba Mwanasheria Mkuu mwenzake wa Kenya ruhusa ya mimi kuhojiwa na Polisi wa Kenya juu ya shambulio hilo kama inavyotakiwa na sheria husika za nchi yetu.
Polisi wa Tanzania hawana mamlaka ya kunihoji nikiwa Kenya au kwingineko nje ya mipaka ya Tanzania'.

By Tundu Lissu, Rais wa wanasheria Tanganyika, na mwanasheria msomi...pia ni mzalendo nambari one Tanzania.
 
Hujui kitu!! Mambo ya kipelelezi waachie wapelelezi wewe fanya yanayokuhusu!
Nyamaza Wewe acha tujadili kauli ya Lissu. We nani kunizuia? Au unataka niandike upendacho?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…