Mapema leo Juni 16, 2025 Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu amefikishwa Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam kusikiliza kesi ya Uhaini na Kesi ya kuchapisha uongo Mtandaoni zinazomkabili ikiwa ni mara ya tatu kwa sasa kufika Mahakamani kusikiliza kesi yake
===
Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Upinzani nchini Tanzania CHADEMA, Tundu Lissu ameileza mahakama nchini Tanzania kuwa haki yake ya msingi ya kuwasiliana na kufanya mashauriano na mawakili wake imefinywa. Amesema amekuwa gerezani kwa siku 68 lakini mazingira kwa wakati wote yamekuwa magumu. Lissu anakabiliwa na kesi ya uhaini pamoja na kesi ya kuchapisha taarifa za uwongo mtandaoni

Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Tundu Lissu ambaye anakabiliwa na Kesi mbili kwenye Mahakama ya Kisutu, amesema kwamba kwa siku 68 ambazo amekuwa Gerezani amenyimwa haki ya kufanya mazungumzo ya faragha na Mawakili wake ambao wamekuwa wakienda kuonana naye.
Ameongeza kuwa licha ya hivyo yeye pamoja na Mawakili wake hawapati nafasi ya kubadilishana nyaraka kwa ajili ya kushughulikia kesi zinazomkabili.
Lissu akiwa kizimbani amesema kwamba amekuwa akiongea na Mawakili kwenye simu akiwa kwenye eneo ambalo halimpi nafasi ya kufanya mazungumzo ya faragha, ambapo amesema kuwa kupitia mawasiliano ya simu au eneo chumba anachotumia kuwasiliana na Mawakili wake kunaweuwezekano kupokwa kwa haki ya faragha.
Amedai kuwa mazingira ya aina hiyo ni kinyume na Sheria na kuwa Mahakama ndiyo yenye mamlaka ya kuweka utaratibu tofauti kwa wa Mawakili kumuona mteja wao akiwa Gerezani
Kesi hiyo inaendelea...