NImekuwa najitahidi sana kufuatilia dhamira ya ndani ya Tundu Lissu na nimekuja kugundua inawezekana hana nia ovu na taifa hili.
Inawezekana ana mapungufu yake mengi mathalani kutumia lugha za uchochezi au tonne mbaya anapokuwa anazungumza au inawezekana(sina uhakika) anatumiwa na mataifa ya ulaya kwa ajenda zao,lakin jamaa sio mbinafsi kabisa.Mimi siyo CHADEMA lakin nilifuatilia sana mchakato wa uchaguzi ndani ya CHADEMA na jinsi kulivyotaka kufanyika figisu jamaa asigombee.Vipaumbele vyake alivyokuwa anavieleza,vilikuwa na hoja na mashiko makubwa.
Kipindi hicho ktk kampuni moja yenye umiliki wa hisa za kifamilia,kuna kiongozi alikuwa anafanya yale yale aliyokuwa anayafanya Mbowe,ikiwemo kutaka kukalia kiti hicho yeye pekee yake na asitoe nafasi kabisa kwa watu wengine.Mimi nikawa nasema,ukishindwa kutengeneza viongozi wachanga na kutoamini kuwa mwingine anaweza kufanya majukumu yako vizuri au pengine hata kukuzidi,basi wewe unapoteza sifa ya leadership na mentorship.Kipindi hicho yulikuwa na mjadala mkali sana kuhusu uongozi wa milele na kutotengeneza successors.
Misimamo ya Tundu Lisu kupiga vita rushwa waziwazi,ni credit tosha inayofanya jamaa nimkubali.Anavyoongea kuhusu rushwa,unamuona kabisa anamaanisha.Kwa maslahi ya taifa hili,system inayolitakia mema taifa hili,ingetumia maarifa ya Tundu Lissu vizuri kutusaidia kutoka hapa tulipo.Jamaa anajua sana lakin tatizo lake anaghafirika upesi sana na yupo too emotional.
Nimekuwa namuona anavyopiga makelele mahakamani akiwa anaingia,naona kabisa hana utulivu kiasi flani.Lakin je,kuna kiongozi gani duniani asiye na mapungufu?Chunguza vizuri kwa wanaoishi karibu na marais na utajua kuwa hata wao pia wana mapungufu yao.Tundu Lissu angeachwa afanye siasa za kulisaidia taifa hili.Kwa wenye taarifa za ki intelijensia(ambao pengine wengine hatuzijui) basi watuambie sasa Tundu Lisu ana ajenda gani ya siri zaidi ya kutaka mifumo imara na kutetea wengine.Juzi nimeona amewatetea hadi wafungwa gerezani.Hajiangalii yeye tu ndiyo maana hajataka hata kulazimisha agombee urais mwaka huu.
Awe mpole tu asitunishiane misuli na walioshika mpini.Aweshawishi tu wampokee ili waungane tulijenge taifa letu.Nchi ni yetu wote.
Tupeane nafasi ya kulijenga taifa letu na tusitoe mianya ya mabeberu kujipenyeza katika huu mgogoro na kuisambaratisha nchi yetu