Elections 2010 Tundu Lissu naye mwendo mdundo...!

reflection ya watani zangu wanyaturu kuhusu democrasia ni wanapoamua kumchagua tundu lisu kwenda mjengoni.
pale singida mjini dewiji anao mtandao mkubwa sana wa upenyezaji wa rushwa ambao wakazi wa singida wanauchemshia dawa ya ki-takukuru.
 
Jamana wana JF nipeni raha Tindu lisu mambo yake yako vipi?
Tupeni new tuendelee kulamba rubisi:sad:
 
Tundu Lissu, mwanasheria machachari ambaye amekuwa anaichachafya CCM kuhusu mikataba mibovu ya madini, ameshinda katika jimbo lake ila NEC inashindwa kumtangaza kwa sababu mpinzani wake anataka masanduku yafunguliwe kura zihesabiwe tena. Lissu anagoma kwani anasema sheria ya uchaguzi inamlinda -- huwezi kuhesabu kura wakati masanduku yalilala usiku kusikojulikana. Anasisitiza matokeo ya vituoni yaliyokuwa yamehakikiwa na wakala wa vyama na kusainiwa ndiyo yatangazwe.

Lissu amebana humo humo katika chumba cha kuhesabia kura na kitabu chake cha sheria ya uchaguzi ambacho tayari kakifungua ukurasa husika na kuweka juu ya meza.

Inasemekana CCM inamuoigopa sana Lissu, haimtaki akaingia Bungeni. CCM inaona ni bora hata akina 'Slaa" watano warudi Bungeni kuliko Lissu mmoja.
 
jamani e tuwe na data mbona tunapeana presha. Hdi sasa ni Manyoni mashariki na magharibi, singida mjini tu ndo yametangazwa Channel ten ndo source me naangalia sasa hivi. Udaku noooooooooooooo
 
Yeyooo! TunduLissu usifunge huo msaafu wa sheria. Anza kuonesha machachari yako apo apo. Naomba wanasheria mumpe support,aingie mjengoni ndugu Lissu. Akitangazwa mi nachinja mbuzi wangu wawili,hata kama ni saa saba usiku!
 
tunamuhitaj sana lissu bungeni maaana kama slaa hayupo basi lazima tumpate lisu.
 
Jamani hakika akiingia bungeni Tundu Lissu basi mchezo utakuwa umekwisha. atakuwa msaada mkubwa sana ktk harakati za kuikomboa nchi hii. tunamtakia mema yote na Mungu aendelee kuwa upande wake.
 
Namwombea Lisu kila lililojema ili ashinde na aongeze nguvu bungeni.
 
Lisu pekee ni sawa na wabunge 100. Tunakutakia kila la kheri uingie bungeni utukomboe watanzania wanyonge
 
Back
Top Bottom