Utafungia Tanzania lakini si DUNIANIKitafungiwa sababu za uchochezi
HAPO NDIO UTAJUA UFIPISHO WA AKILI ZAWAKINA BA-SHITE ZILIPOAtoa cha jipime hisabati
Kesha umizwa Huyo, mdomo umeponza kichwa, acha ajifariji na kitabu, ila akumbuke pia ngawira za Lowassa alizogawana na kina Mbowe zilivyomuharibia maisha Dr Slaa.Mwanasiasa mashuhuri zaidi Afrika Mashariki Tundu Antipas Lissu anajiandaa kuandika kitabu chake kitakachosambazwa duniani kote.
Lissu ambaye ni Rais wa chama cha Wanasheria Tanganyika TLS anatarajiwa kuelezea maisha yake kwa ujumla na hasa jaribio lililopangwa na kushindwa la kuondoa Uhai wake Septemba 7.
Kiongozi huyo ambaye pia ni Mwanasheria mkuu wa Chadema anatarajiwa katika kitabu hicho kueleza uvunjifu wa haki za binadamu na ukandamizaji wa Uhuru wa kutoa maoni.
Kiongozi huyo mwenye nyadhifa kadhaa ikiwemo mbunge wa Singida Mashariki na Mnadhimu mkuu wa upinzani alipatwa na madhila ya kupigwa risasi hadharani mchana kweupe huku mpaka leo ikiwa hakuna yeyote aliyekamatwa kuhusika na tukio hilo.
Kitabu hicho cha Tundu Lissu kinatarajiwa kutafsiriwa kwa lugha kadhaa ili iwe rahisi kusambazwa duniani kote na kiwafikie watu wengi zaidi.
Mwanamke gani we unakua na roho ya kipaka hivyoKesha umizwa Huyo, mdomo umeponza kichwa, acha ajifariji na kitabu, ila akumbuke pia ngawira za Lowassa alizogawana na kina Mbowe zilivyomuharibia maisha Dr Slaa.
Malipo ni hapa duniani
Kitafungiwa sababu za uchochezi. Akitaka kiuze mhariri mkuu awe ndugu Haraka Haraka wa Lumumba.
Sidhani kama hicho kitabu kitakubaliwa kusambazwa hapa Tanzania.
Labda aandike kuhusu maisha yake binafi. Lakini kwenye Tasnia ya Sheria hawezi, sijawahi ona andiko la Lissu zaidi ya vijarida alivyoshirikishwa na wenye uwezo wao. Hata mini ninamshinda.
Mwaka 1993 hadi 1994, Julius Nyerere alitunga kitabu kiitwacho "Uongozi wetu na hatima ya Tanzania". Publishers wa Tanzania walipokipokea ili wakichapishe wakaogopa hivyo hakuna kampuni iliyokubali kukichapisha.
Nyerere nadhani akasema kimoyomoyo "Naenda Zimbabwe", hivyo akaenda Zimbabwe, akampata publisher anayeitwa "Zimbabwe Publishing House" akakitoa.
Kisha akaenda mwenyewe akaja nacho na akakisambaza yeye mwenyewe na mwaka 1995 akakitoa kwa lugha ya kiingereza kikaitwa "Our leadership and destiny of Tanzania".
Serikali ilishindwa kukizuia. Hivyo, Tundu Lissu afanye kama Julius Nyerere. Vilevile draft yake awe anaiweka kwenye email yake maana kwa jinsi anavyopekulia kila wakati nyumbani mwake wanaweza kuchukua flashdisk na computer zote za nyumbani kwake ili kisitoka.
Mimi huwa natumia mbinu hii. Kama watu wakija hata kuninyanganya kila kitu, hawawezi kuingia kwenye emails zangu na ku- deleta mambo ambayo nimeya-upload huko.
Tundu Lissu aanze kukisambaza cha kiingereza kwanza ili kelele zitokee nje ili sisi tulioko nje tuanze kuwaringishia uhondo uliomo na mjenge hamu ya kukipata.
Uzuri siandiki uchochezi, chuki na fitina. Ninaandika kwa faida ya wote wenye mahitaji kwenye tasniaMkuu kama unamshinda mbona hujapigwa risasi?