Mwanasiasa mashuhuri zaidi Afrika Mashariki Tundu Antipas Lissu anajiandaa kuandika kitabu chake kitakachosambazwa duniani kote.
Lissu ambaye ni Rais wa chama cha Wanasheria Tanganyika TLS anatarajiwa kuelezea maisha yake kwa ujumla na hasa jaribio lililopangwa na kushindwa la kuondoa Uhai wake Septemba 7.
Kiongozi huyo ambaye pia ni Mwanasheria mkuu wa Chadema anatarajiwa katika kitabu hicho kueleza uvunjifu wa haki za binadamu na ukandamizaji wa Uhuru wa kutoa maoni.
Kiongozi huyo mwenye nyadhifa kadhaa ikiwemo mbunge wa Singida Mashariki na Mnadhimu mkuu wa upinzani alipatwa na madhila ya kupigwa risasi hadharani mchana kweupe huku mpaka leo ikiwa hakuna yeyote aliyekamatwa kuhusika na tukio hilo.
Kitabu hicho cha Tundu Lissu kinatarajiwa kutafsiriwa kwa lugha kadhaa ili iwe rahisi kusambazwa duniani kote na kiwafikie watu wengi zaidi.