Tundu Lissu: Matumizi ya hovyo ya mamlaka ya kipolisi lazima yakome

Ni kweli Mkuu ame-paralyze the whole system! Lkn utashangaa kuna watu wanashangilia kwa vile hawajakumbwa na kadia hii au nduguze. Tuko pamoja kamanda Lissu!
 
Huyu ndie lissu ninayemjua, niliposema ataitumia fursa hii ya TLS kama kitego cha kujijenga kisiasa na kuendeleza siasa za chama chake cha upinzani, nilikuwa nayaona haya.

Kuna vijana wangapi waliokuwa magerezani au Rumande bila ya kufikishwa mahakamani, Lema alitutajia baadhi yao waliopo Kisongo.

Lakini Lissu ameamu kuchagua yule aliyekamatwa kwa sababu inayohusiana na ziara ya Raisi bandarini, kwa sababu hiyo kesi ndiyo yenye manufaa kwenye chama chake na yeye mwenyewe.

Lissu ataitumia TLS kama gari lake, punde tutaona mawakili wakimlalamikia nao wataitwa wasaliti waliotumwa na ccm.

Lissu is the most pathetic politician
 
Unachokisema Tundu Lisu ni kweli kabisa maana watu wengine wanafungwa kujaza jela pasipo sababu za msingi.
 
Na we una uhakika rais katoa hayo maelezo..mambo yakiwa magumu kwenu mnasema rais..ney alipokamatwa mlisema rais..kaachiwa mnasema hana mamlaka ya kusema nyimbo ipigwe au isipigwe..mi nadhani mtanyooka tu..twende hivi hivi..huyo lissu atafute rais mwingine wa kumpelekea maombi yake..lowasa si yupo??
Chizi wewe!!!
 
Huyu raisi,ni mlipuko.hafanyi kz kwa habari za mitandaoni.ila cnema zake za bandarini na kuamuru Ney aachiwe,hasemi mitandao imekosea kuandika wala kuweka picha zake.nivigumu sana kumuelewa mtu mwenyewe tabia ya visac na roho mbaya ! Kwasababu kila atakalofanya hata liwe jema,linaogopewa.hakuna anayekua na imani nalo.nimtu wa ubabe sana hivyo hata pale anapoonyesha tabasamu,ni Vigumu tabasamu lake kutafcriwa vzr.huyu mtu weka mbali na babies tu co wakuamini,wala kumfuata.
 
TunduLissu ni wapi Rais alisema UKWAJU asiachiwe?Alichofanya Rais ni kutembelea container zilizokamatwa,kama ni tatizo la kisheria au polisi usimuingize Rais kana kwamba kaamuru huyo UKWAJU asiachiwe.
Utakuwa mtu wa ajabu sana kuomba kuonana na Rais uliemwita dikteta uchwara,unaenda kuongea nini sasa na dikteta uchwara.
Akili za Tundu Lissu zinawakilisha akili za wafuasi wengi sana wa UKAWA,-Kutukana mamba kabla ya kuvuka mto
we kiazi taarifa ya Greyson Msigwa ilisema raisi kakamata container wenye akili tulishtuka raisi anakamata????
 
MATUMIZI YA HOVYO YA MAMLAKA YA KIPOLISI LAZIMA YAKOME

Waheshimiwa salaam.

Nimetoka Polisi Bandari muda huu. Nilikwenda kumwona mtu aitwaye Ramadhani Mussa Hamisi alias Ukwaju ambaye yuko mahabusu ya Polisi Bandari tangu tarehe 4 ya mwezi huu.

Ukwaju anatuhumiwa kuhusika na mzigo wa magari ya kifahari yaliyokamatwa na Bwana Mkubwa Rais siku chache zilizopita.

Leo ni siku ya 23 yuko mahabusu. Hajapelekwa kwenye mahakama yoyote na hajashtakiwa kwa kosa lolote lile.

Suala lake limeshafika kwa DPP na kwa RPC Sirro tangu siku kadhaa zilizopita lakini kila mkubwa anayehusika anaogopa kutoa maamuzi ya kumpeleka mahakamani au hata kumwachia kwa dhamana ya polisi.

Haya ndiyo madhara ya Rais wetu kuingilia majukumu ya kisheria yasiyomhusu. Rais wetu anaweza kuwa Amiri Jeshi Mkuu lakini yeye sio askari polisi mwenye jukumu la kukamata wahalifu au kupeleleza makosa wanayotuhumiwa nayo.

Ijapokuwa ni Rais ndiye anayemteua DPP, yeye sio DPP na hana mamlaka ya kuamua nani apelekwe mahakamani na nani asipelekwe.

Sasa inapotokea Rais anakwenda kwenye matukio ya uhalifu, kama ilivyokuwa kwenye suala la Ukwaju, anawafanya watendaji wanaohusika nayo washindwe kufanya kazi zao kwa mujibu wa sheria.

Katika mazingira ya sasa ya 'utumbuaji majipu', watumishi wa umma wanaogopa kufanya maamuzi kwa hofu ya kutumbuliwa majipu, hasa kwa masuala ambayo yameshafikishwa kwa Rais kwa njia extra-legal kama hili la Ukwaju.

Matokeo yake haki za wananchi za kuwa huru zinakiukwa bila sababu za msingi.

Haya ni masuala ambayo TLS chini ya uongozi wangu inatakiwa kuyashughulikia. Hii ni sehemu ya agenda tutakayompelekea Rais na IGP na AG pamoja na Waziri mpya Prof. Kabudi tutakapoenda kuonana nao kama tulivyokwishawaomba.

Kila mmoja wetu, mawakili na wasiokuwa mawakili tuyapigie kelele matumizi mabaya ya mamlaka ya kiupelelezi na ya kipolisi yanayopelekea haki za wananchi wetu kuvunjwa namna hii.

Kelele zitasaidia, ukimya ni sawa na kuyaunga mkono matendo haya mabaya.

Wasalaam.

Tundu Lissu.
wee lissu usijifanye unajua sana. hao chadema wanakupa kichwa tu. rais akienda kwenye matukio ndio watu washindwe kufanya kazi zao? huoni kama wanashindwa kutokana na mapungufu yao. kama watu wamebobea kupindisha taratibu kwa ulaji wa rushwa ndio utaona wanashindwa kufanya kazi zao. tulisema lissu atageuza tls mshirika wa ukawa polepole tunaanza kuona.
 
Mjinga sasa wewe, Tundu Lissu ameomba kuonana na Rais kama Rais wa TLS sasa kwa akili zako ndogo wewe unepeleka mbali sana. Urais ni Taasisi ambayo ipo na itakuwepo hata Rais wa sasa atakapoondoka madarakani. Acha umbwiga wewe!!
Kwani Tundu Lissu akiwa Rais wa TLS ,dikteta uchwara anabadilika?Muulizeni Lissu wenu,anataka kuongea nini na dikteta uchwara?
 
Kama una kumbukumbu pale mahakamani shahidi wa jamhuri alisema dikteta uchwara hamjui, sasa tusaidie kumtaja dikteta uchwara ni nani
Wacha kufinyanga maneno muulizeni Lissu ataongea nini na dikteta uchwara?
 
Km makonda anabambikia watu kesi za madawa ya kulevya unadhani masikini watapona kweli?
 
MATUMIZI YA HOVYO YA MAMLAKA YA KIPOLISI LAZIMA YAKOME

Waheshimiwa salaam.

Nimetoka Polisi Bandari muda huu. Nilikwenda kumwona mtu aitwaye Ramadhani Mussa Hamisi alias Ukwaju ambaye yuko mahabusu ya Polisi Bandari tangu tarehe 4 ya mwezi huu.

Ukwaju anatuhumiwa kuhusika na mzigo wa magari ya kifahari yaliyokamatwa na Bwana Mkubwa Rais siku chache zilizopita.

Leo ni siku ya 23 yuko mahabusu. Hajapelekwa kwenye mahakama yoyote na hajashtakiwa kwa kosa lolote lile.

Suala lake limeshafika kwa DPP na kwa RPC Sirro tangu siku kadhaa zilizopita lakini kila mkubwa anayehusika anaogopa kutoa maamuzi ya kumpeleka mahakamani au hata kumwachia kwa dhamana ya polisi.

Haya ndiyo madhara ya Rais wetu kuingilia majukumu ya kisheria yasiyomhusu. Rais wetu anaweza kuwa Amiri Jeshi Mkuu lakini yeye sio askari polisi mwenye jukumu la kukamata wahalifu au kupeleleza makosa wanayotuhumiwa nayo.

Ijapokuwa ni Rais ndiye anayemteua DPP, yeye sio DPP na hana mamlaka ya kuamua nani apelekwe mahakamani na nani asipelekwe.

Sasa inapotokea Rais anakwenda kwenye matukio ya uhalifu, kama ilivyokuwa kwenye suala la Ukwaju, anawafanya watendaji wanaohusika nayo washindwe kufanya kazi zao kwa mujibu wa sheria.

Katika mazingira ya sasa ya 'utumbuaji majipu', watumishi wa umma wanaogopa kufanya maamuzi kwa hofu ya kutumbuliwa majipu, hasa kwa masuala ambayo yameshafikishwa kwa Rais kwa njia extra-legal kama hili la Ukwaju.

Matokeo yake haki za wananchi za kuwa huru zinakiukwa bila sababu za msingi.

Haya ni masuala ambayo TLS chini ya uongozi wangu inatakiwa kuyashughulikia. Hii ni sehemu ya agenda tutakayompelekea Rais na IGP na AG pamoja na Waziri mpya Prof. Kabudi tutakapoenda kuonana nao kama tulivyokwishawaomba.

Kila mmoja wetu, mawakili na wasiokuwa mawakili tuyapigie kelele matumizi mabaya ya mamlaka ya kiupelelezi na ya kipolisi yanayopelekea haki za wananchi wetu kuvunjwa namna hii.

Kelele zitasaidia, ukimya ni sawa na kuyaunga mkono matendo haya mabaya.

Wasalaam.

Tundu Lissu.
Wewe huna jipya, endelea kutetea wahalifu mpaka siku moja wahalifu wakushughulikie ndio utaacha ujinga, watu wanaiba mali ya umma we unakuja tuvitabu twako hapa! Ovyo kabisa, kama ulitaka uongozi huko TLS ili kupata Wateja zaidi na kuboresha Biashara yako we weka wazi!
 
kabombe: Unajua Lissu ni nani kwa nchi hii? Yeye ni Rais wa chama cha wanasheria (TLS). Ana wajibu wa kumshauri kiongozi wa nchi kwa mambo ya kisheria bila kujali huyo Kiongozi ana tabia gani. Hizo tabia alizonazo ndo zinawafanya wanasheria wamshauri. Ulitaka waache kumshauri? TZ ni yetu sote ndugu.
Lissu anatafuta Wateja wa Biashara yake kwa nguvu.
 
TunduLissu ni wapi Rais alisema UKWAJU asiachiwe?Alichofanya Rais ni kutembelea container zilizokamatwa,kama ni tatizo la kisheria au polisi usimuingize Rais kana kwamba kaamuru huyo UKWAJU asiachiwe.
Utakuwa mtu wa ajabu sana kuomba kuonana na Rais uliemwita dikteta uchwara,unaenda kuongea nini sasa na dikteta uchwara.
Akili za Tundu Lissu zinawakilisha akili za wafuasi wengi sana wa UKAWA,-Kutukana mamba kabla ya kuvuka mto
Ooohhoooooo ohoooooooo
 
Nina uhakika 100% Rais hakutoa maagizo hayo hata taarifa ya Lissu inaonesha tu kuwa Rais hahusiki ila tu kwa sababu Magufuli ni Role model wa Tundu Lissu lazima Tundu amtaje tu
Una akili fupi kama maisha ya funza
 
Wewe kabombe soma mtiririko wa hiyo masage ya lisu,siyo kokalili msitari mmoja na kuanza kulopoka
 
Back
Top Bottom