Tundu Lissu: Matumizi ya hovyo ya mamlaka ya kipolisi lazima yakome

kasolobela

Senior Member
Mar 25, 2017
107
121
MATUMIZI YA HOVYO YA MAMLAKA YA KIPOLISI LAZIMA YAKOME

Waheshimiwa salaam.

Nimetoka Polisi Bandari muda huu. Nilikwenda kumwona mtu aitwaye Ramadhani Mussa Hamisi alias Ukwaju ambaye yuko mahabusu ya Polisi Bandari tangu tarehe 4 ya mwezi huu.

Ukwaju anatuhumiwa kuhusika na mzigo wa magari ya kifahari yaliyokamatwa na Bwana Mkubwa Rais siku chache zilizopita.

Leo ni siku ya 23 yuko mahabusu. Hajapelekwa kwenye mahakama yoyote na hajashtakiwa kwa kosa lolote lile.

Suala lake limeshafika kwa DPP na kwa RPC Sirro tangu siku kadhaa zilizopita lakini kila mkubwa anayehusika anaogopa kutoa maamuzi ya kumpeleka mahakamani au hata kumwachia kwa dhamana ya polisi.

Haya ndiyo madhara ya Rais wetu kuingilia majukumu ya kisheria yasiyomhusu. Rais wetu anaweza kuwa Amiri Jeshi Mkuu lakini yeye sio askari polisi mwenye jukumu la kukamata wahalifu au kupeleleza makosa wanayotuhumiwa nayo.

Ijapokuwa ni Rais ndiye anayemteua DPP, yeye sio DPP na hana mamlaka ya kuamua nani apelekwe mahakamani na nani asipelekwe.

Sasa inapotokea Rais anakwenda kwenye matukio ya uhalifu, kama ilivyokuwa kwenye suala la Ukwaju, anawafanya watendaji wanaohusika nayo washindwe kufanya kazi zao kwa mujibu wa sheria.

Katika mazingira ya sasa ya 'utumbuaji majipu', watumishi wa umma wanaogopa kufanya maamuzi kwa hofu ya kutumbuliwa majipu, hasa kwa masuala ambayo yameshafikishwa kwa Rais kwa njia extra-legal kama hili la Ukwaju.

Matokeo yake haki za wananchi za kuwa huru zinakiukwa bila sababu za msingi.

Haya ni masuala ambayo TLS chini ya uongozi wangu inatakiwa kuyashughulikia. Hii ni sehemu ya agenda tutakayompelekea Rais na IGP na AG pamoja na Waziri mpya Prof. Kabudi tutakapoenda kuonana nao kama tulivyokwishawaomba.

Kila mmoja wetu, mawakili na wasiokuwa mawakili tuyapigie kelele matumizi mabaya ya mamlaka ya kiupelelezi na ya kipolisi yanayopelekea haki za wananchi wetu kuvunjwa namna hii.

Kelele zitasaidia, ukimya ni sawa na kuyaunga mkono matendo haya mabaya.

Wasalaam.

Tundu Lissu.
 
Aiseee hii inafanana na wa kwangu, mwezi na zaidi sasa

Ukweli Nina hasira mpaka zinafurika

Maana kila unayeemuendea anaogopa kufanya chochoke kisa maamuzi yametoka juu

Imeniumiza, inaniumiza, naumia,

Kwa vile sina nguvu yeyote

Lkn Mungu ni mwema
 
MATUMIZI YA HOVYO YA MAMLAKA YA KIPOLISI LAZIMA YAKOME

Waheshimiwa salaam.

Nimetoka Polisi Bandari muda huu. Nilikwenda kumwona mtu aitwaye Ramadhani Mussa Hamisi alias Ukwaju ambaye yuko mahabusu ya Polisi Bandari tangu tarehe 4 ya mwezi huu.

Ukwaju anatuhumiwa kuhusika na mzigo wa magari ya kifahari yaliyokamatwa na Bwana Mkubwa Rais siku chache zilizopita.

Leo ni siku ya 23 yuko mahabusu. Hajapelekwa kwenye mahakama yoyote na hajashtakiwa kwa kosa lolote lile.

Suala lake limeshafika kwa DPP na kwa RPC Sirro tangu siku kadhaa zilizopita lakini kila mkubwa anayehusika anaogopa kutoa maamuzi ya kumpeleka mahakamani au hata kumwachia kwa dhamana ya polisi.

Haya ndiyo madhara ya Rais wetu kuingilia majukumu ya kisheria yasiyomhusu. Rais wetu anaweza kuwa Amiri Jeshi Mkuu lakini yeye sio askari polisi mwenye jukumu la kukamata wahalifu au kupeleleza makosa wanayotuhumiwa nayo.

Ijapokuwa ni Rais ndiye anayemteua DPP, yeye sio DPP na hana mamlaka ya kuamua nani apelekwe mahakamani na nani asipelekwe.

Sasa inapotokea Rais anakwenda kwenye matukio ya uhalifu, kama ilivyokuwa kwenye suala la Ukwaju, anawafanya watendaji wanaohusika nayo washindwe kufanya kazi zao kwa mujibu wa sheria.

Katika mazingira ya sasa ya 'utumbuaji majipu', watumishi wa umma wanaogopa kufanya maamuzi kwa hofu ya kutumbuliwa majipu, hasa kwa masuala ambayo yameshafikishwa kwa Rais kwa njia extra-legal kama hili la Ukwaju.

Matokeo yake haki za wananchi za kuwa huru zinakiukwa bila sababu za msingi.

Haya ni masuala ambayo TLS chini ya uongozi wangu inatakiwa kuyashughulikia. Hii ni sehemu ya agenda tutakayompelekea Rais na IGP na AG pamoja na Waziri mpya Prof. Kabudi tutakapoenda kuonana nao kama tulivyokwishawaomba.

Kila mmoja wetu, mawakili na wasiokuwa mawakili tuyapigie kelele matumizi mabaya ya mamlaka ya kiupelelezi na ya kipolisi yanayopelekea haki za wananchi wetu kuvunjwa namna hii.

Kelele zitasaidia, ukimya ni sawa na kuyaunga mkono matendo haya mabaya.

Wasalaam.

Tundu Lissu.
TunduLissu ni wapi Rais alisema UKWAJU asiachiwe?Alichofanya Rais ni kutembelea container zilizokamatwa,kama ni tatizo la kisheria au polisi usimuingize Rais kana kwamba kaamuru huyo UKWAJU asiachiwe.
Utakuwa mtu wa ajabu sana kuomba kuonana na Rais uliemwita dikteta uchwara,unaenda kuongea nini sasa na dikteta uchwara.
Akili za Tundu Lissu zinawakilisha akili za wafuasi wengi sana wa UKAWA,-Kutukana mamba kabla ya kuvuka mto
 
Labda ndiye aliyemkamata kwa sababu hata makontena ya mchanga wa dhahabu pamoja na magari ya kifahari yaliyofichwa ndani ya makontena tunaambiwa alikamata kwa mkono wake.
 
Tundu Lissu ni wapi Rais alisema UKWAJU asiachiwe?Alichofanya Rais ni kutembelea container zilizokamatwa,kama ni tatizo la kisheria au polisi usimuingize Rais kana kwamba kaamuru huyo UKWAJU asiachiwe.
Utakuwa mtu wa ajabu sana kuomba kuonana na Rais uliemwita dikteta uchwara,unaenda kuongea nini dikteta uchwara.
Akili za Tundu Lissu zinawakilisha akili za wafuasi wengi sana wa UKAWA,-Kutukana mamba kabla ya kuvuka mto

Wewe una uhakika gani kuwa rais hakutoa Hayo maelekezo? Na pia kama viongozi mmepishana kauli kwa hoja inatakiwa kusiwe na room for dialogue!!! Kweli!!!!
Vijana wa lumumba punguzeni ushabiki, fikirini kabla ya kuandika.
 
Tundu Lissu ni wapi Rais alisema UKWAJU asiachiwe?Alichofanya Rais ni kutembelea container zilizokamatwa,kama ni tatizo la kisheria au polisi usimuingize Rais kana kwamba kaamuru huyo UKWAJU asiachiwe.
Utakuwa mtu wa ajabu sana kuomba kuonana na Rais uliemwita dikteta uchwara,unaenda kuongea nini dikteta uchwara.
Akili za Tundu Lissu zinawakilisha akili za wafuasi wengi sana wa UKAWA,-Kutukana mamba kabla ya kuvuka mto
Kwa taarifa yako hata dictator kamili huwa anaongea tu na watu, inategea kaamkaje siku hiyo. Sema tu anafanya hivyo bila kufuata sheria taratibu au mpangilio Fulani, anakurupuka tu.
 
Back
Top Bottom