Atoa mfano wa ndege ya airbus kukamatwa Uholanzi baada ya baraza la usuluhishi la kimataifa kuona mwekezaji alipwe fidia kwa mkataba uliovunjwa na serikali.
Jopo la waamuzi huwa na watu watatu, mmoja huteuliwa na serikali/mdaiwa yaani Tanzania, mjumbe wa pili huteuliwa na mwekezaji na wa tatu huteuliwa kwa makubaliano baina ya serikali na mwekezaji na huyu huwa ndiyo mwenyekiti wa tribunal anabainisha Tundu Lissu.
Tundu Lissu anazidi kutuelimisha kuwa wawekezaji huweka sharti kuwa kukitokea mgogoro basi waende kwenye hii tribunal / baraza la kimataifa kupata suluhisho. Maana wawekezaji wanafahamu kuwa mahakama zetu na majaji wake hawapo huru.
Tanzania imesaini mikataba na nchi nyingi ambazo ni wadau wa maendeleo kuwa kukitokea kutoelewana baina ya wawekezaji toka Mataifa hayo na Tanzania basi utatuzi utatafutwa katika Baraza hilo la kimataifa la biashara / uwekezaji kupata suluhu au kulipwa fidia.
Hivyo kelele kuwa inakuwaje ndege zetu zinakamatwa kiholela siyo za kweli. Maana wakati wa kuingia mkataba na wawekezaji mambo yote huwekwa hadharani na pia Tanzania imesaini mikataba ya maridhiano ya kimataifa kuwa mchakato gani ufuatwe kukitokea kadhia kama hii ya mwekezaji wa shamba la miwa Bagamoyo kugeukwa dakika ya mwisho baada ya mkataba kuwekwa.
Tundu Lissu anaongeza kuwa maamuzi ya Tribunal hii ya usuluhishi yanatambulika kama maamuzi ya mahakama yoyote ulimwengu na Tanzania ikiridhia hivyo ili kukazia hukumu ya baraza hilo, basi Mali za mdaiwa zinaweza kukamatwa kokote kule kulipo nchi zilizoafikia mikataba hii ya kimataifa.
Tundu Lissu baada ya kuweka sawa nini kimepelekea ndege za serikali yaani airbus a220-300 kukamatwa anasema kuwa ....
icsid.worldbank.org
https://icsid.worldbank.org › about
About ICSID - World Bank
ICSID is the world's leading institution devoted to international investment dispute settlement. It has extensive experience in this field