Tundu Lissu, kwa hili, kachemka

Boko Haramu, tafsiri yake ni Western Education is Haram, yaani elimu ya Magharibi ni haramu, unaweza kupata hisia kwamba dini inawasukuma kusafisha kila kitu kilicho na ideals za kimagharibi ukiwemo Ukristo na ndio maana Makanisa hayatakiwi kuwepo kule kaskazini mwa Nigeria.

Mzee zimmerman, hivi huo uislamu ulikuwepo kabla ya waarabu hawajafika Afrika?! Yaani unataka kusema kwamba hao Boko Haramu wanaona uislamu ndiyo dini ya asili yao?! Kwa hiyo ideas za kimashariki ya kati na mbali ndizo sawa na ideas za ancient Africa?! Hawa jamaa hivi wanaelewa kwamba waafrika walikuwa na imani zao; kwamba uislamu na ukristo zote ni imani ngeni zilizoletwa na wavamizi - wawe wamisionari ama wafanya biashara (waarabu na waasia)?!
 
Last edited by a moderator:
lisu yupo sahihi 100%,tatizo ni muungano hapo hakuna lingino,zanzibar ni taifa la kislam na wakristo ni wakuja,hivyo wanachoma makanisa ili kuwaondoa wabara wabaki na zanzibar yao,zanzibar komaeni mpaka kieleweke,hakuna ugaidi ukiwa unadai haki yako
 
Nakubaliana na mheshimiwa Lissu kwa asilimia zote. Amejibu kitaalam, pengine ndio maana wengine wanapata ugumu kuelewa. Labda swali moja linaweza kusaidia katika kumuelewa. Je, mtu yeyeto anaweza kutaja mahali na wakati ambapo paliwahi kuwa na kitu kinachoitwa uislamu safi, katika maana ya kuwa dini pekee bila mchanganyiko wowote ule? Tena Lissu akisema frustration yuko sahihi kwasababu frustration haina mantiki. Ukiuliza mbona wanachoma makanisa tu, jibu ni kwamba ndiyo asili ya frustrations, mtu mwenye akili tulivu haelewi kirahisi anachofanya a frustrated person. Even the other groups that may be referred in this connection, basically they are not for doing proselytism, but they reflect a certain kind of political disillusionment. Hapa dini ni terminus operis(object) na si terminus operantis(intention). Ahsante mheshimiwa Lissu.
 
Sikubaliani na hoja yako hata kidogo. Ili watu waweze kuishi katika jamii moja jambo la msingi sio kufuata matakwa au imani ya mtu mwingine ili uweze kukaa naye kwa amani. ukishafanya hivyo tayari umekuwa "MTUMWA"
Jambo la kuzingatia ni kuheshimu uhuru wa mtu mwingine. Mwana falsafa mmoja alisema kuwa "katika msongamano wa watu mwisho wa uhuru wako ni pale linapoanzia bega la mwenzako" Tafsiri yake ni kuwa katika jamii inayoheshimu uhuru wa watu uhuru wako wa kufanya mambo ni kwa kiwango kile tu ambacho hutamuathiri jirani yako.
Kwa hiyo basi tukisema kuwa ili tuishi nao ni lazima tukubaliane na matakwa yao ni dhahiri kuwa tutakuwa watumwa wao. wewe unasema kuwa kwenu mmekubaliana kuku lazima achinjwe kiislamu ili kuwaridhisha, ni sawa ila ukumbuke halitaishia hapo.
- kesho watasema lazima mavazi uvae kwa mujibu wa dini ya kiislamu utakubali?
-Halafu mkikubali watakuja na hili; bar, guest house nk zivunjwe kwa kuwa haziendani na imani yao. tukikubali watasema sheria za nchi hazifai bali sharia za kiislam ndio zifuatwe na watu wote hili ni pamoja na kufanya mashauri yote (ya waislamu na wasio waislamu) kwenye mahakama ya kadhi ili tuweze kukaa nao kwa amani
Mwisho watasema hata raisi lazima awe shehe maana kwa mujibu imani yao hawawezi kutawaliwa na kafri.

Mimi nafikiri uhuru wa kiraia ni muhimu zaidi, kila mtu afanye mambo yake ili mradi asifunje sheria ya nchi ambayo inatuunganisha wote na sheria hii ilinde haki na uhuru wa kila mmoja bila kujali imani.

Twende Taratibu Kiongozi.
Usiongee kwa namna ambayo inamaanisha kwamba sheria zetu ni kamilifu bila chembe ya mapungufu, moja ya mapungufu makubwa ya sheria zetu ni poor penetration kwenye jamii zetu, jamii zetu nyingi zinajiendesha bila ufahamu wa kuwapo kwa sheria, na serikali yetu haijawahi kuchukumua maamuzi ya dhati ya kupropagate sheria za nchi yetu ili ziweze kuwa enforced nchi nzima, vyombo vyetu vya usimamizi wa sheria vinavyanya kazi kwa kuvizia, sheria inaonekana kuwapo baada ya kosa kutokea, hata washitakiwa wengi kwenye mahakama zetu wanashitakiwa kwa mujibu wa sheria wasizozifahamu, kwa hiyo unaposema watu waishi kwa mujibu wa sheria nashindwa kukuelewa unamaanisha nini exactly?

Ukweli ni kwamba Jamii zetu zinaongozwa na mila na desturi fulani fulani, na kwa bahati mbaya sana sheria nyingi zilizopo sasa hazireflect mira na desturi hizi,na ni mila na desturi hizi ndio zimeweza kuzihifadhi jamii zetu katika mazingira ya amani ya utulivu mpaka kufikia sasa, kumbuka kwamba, Mwalimu Nyerere aliona matatizo yanayoweza kujitokeza katika jamii yetu kwa uwapo wa vikabila vingi vingi, ndio maana alitumia nguvu na uwezo wake wote kuhakikisha kwamba elimu ya kuwawezesha watanzania kuishi bila kubaguana kwa misingi ya ukabila, rangi na dini inaingia akilini mwa kila mtanzania, hakuna sheria na maandishi hayo hayawezi kuitwa sheria kwa mtazamo wa kibinaadamu ambayo yanawaelekeza binaadamu kuishi kwa amani na utulivu. ndio maana nikalazimika kufanya reference kwenye maandiko ya kwenye biblia kwa namna yanayohimiza wakisristo kuishi na watu wa jamii zingine.

Hivyo hili sio swala la kisheria, ni swala la mila na desturi, na katika hili narudia tena, tunalazimika kujitune na matakwa ya jamii ya kiislamu,sasa wewe unakuza mambo, unadai kuheshimu mila na desturi za kiislamu ni sawa na kuwa mtumwa kwa uislamu au waislamu, unasisitiza kuheshimu uhuru wa mtu mwingine bila kuvunja sheria, sina nia ya kukushambulia, lakini sina namna ingine ya kuelezea kwamba hii ni hurka ya ushindani usio na maana yoyote ile, nimekueleza kwamba sisi mtaani kwetu ilikuwa na taratibu zetu kwa kuku kuchinjwa na muislamu, msingi ni kwamba if possible nao waje tujumuike nao kwenye chakula, kinyume cha hapo ni kufanya maandalizi ya chakula katika namna ambayo unajuwa jirani yako hawezi kukitumia, kwa nini uweke vikwazo kwenye chakula?
 
Huyo Lisu kuchemsha ni kawaida yake anafanya siasa kwa jazba anatafuta umaarufu kama wa Mh Zito au Mh Mbowe au Mh Dr Slaa kwa nguvu mara nyingi uropoka na kuteleza huyu jamaa hafai kuwa kiongozi mkubwa atatupeleka shimoni,wewe jiulize kuna mahusiano gani kutaka muungano ujadiliwe na kuchoma makanisa kwa nini wasichome misikiti au mali za serikali,hapo Tundu kachemsha sana tuongee ukweli tusiweke siasa manake kuna mijitu mingine itamtetea kwa sababu ni kiongozi wa chama chao ebu tuweke itikadi zetu kando tujadili ukweli wa jambo hili vinginevyo tukiwa tunajadili jambo kimtazamo wa kisiasa hatutafika ata kidogo,Mh Lisu katika hili kachemsha ata wachungaji na wananchi mbalimbali wamemshangaa!

Sawa mimi nitamtetea sababu ni wa chama changu, embu mlete huyo wa chama chako amung'unye tumsikie na wewe umtetee.

Tatizo lao ni kweli lahusu Muungano na wao wanaamini bila muungano wakristo wasingekuwepo na wao wanashambulia kiunganishi kimojawapo cha Muungano. ***** dot ukuda
 
mtoa hoja.. Thread n kilaza tuu.. Hukumuelewa komando lissu vizuri akakuacha njia panda.. Take care
 
%kubwa ya wazanzibar wazawa ni waislam, na wakristo wengi walioko zanzibar ni wahamiaji toka bara, kuwachomea makanisa, baa, nyumba ni ishara ya kuwafukuza warudi kwao bara, na yote hii inatokana na wazanzibari kutokuuhitaji muungano.

Hivi Enjo, kwa kumbukumbu zako ukristo na uislamu ni upi ulianza duniani? nia yangu ni kupima nani mvamizi, nani kati yao anajua maana ya IMANI!!!!
 
​@zimmerman
Ninachoamini ni kwamba Tundu yupo sahihi, na wanaochoma makanisa kule zanzibar siyo Kikundi cha Uamsho, bali vijana wa Dr. Shein ili wazanzibari na jamii iseme hawa jamaa wanachoma makanisa.
Hata mimi mwanzoni nilidhani kwamba waliochoma makanisa ni Uamsho, kumbe siyo!

[MENTION]Mungi [/MENTION]kwa mara ya kwanza nimeanza kukuamini kuwa wewe ni great thinker.
 
Mzee zimmerman, hivi huo uislamu ulikuwepo kabla ya waarabu hawajafika Afrika?! Yaani unataka kusema kwamba hao Boko Haramu wanaona uislamu ndiyo dini ya asili yao?! Kwa hiyo ideas za kimashariki ya kati na mbali ndizo sawa na ideas za ancient Africa?! Hawa jamaa hivi wanaelewa kwamba waafrika walikuwa na imani zao; kwamba uislamu na ukristo zote ni imani ngeni zilizoletwa na wavamizi - wawe wamisionari ama wafanya biashara (waarabu na waasia)?!

Kwa kumkumbusha ourstory not history, ni kuwa IN THE BEGINING AFRIKA WAS CALLED ALKEBULAN- MEANS THE LAND OF THE BLACKS, kwa hili kuna sababu ya kuwahusudu wapagani kwani hawakulazimishi uelewa wao uwe wako pia hasa kwa maswala ya imani.
 
Last edited by a moderator:
hata mimi nakuunga mkono kwa asilimia 100 kwani busara alizotumia mh lissu ndiyo hiyo na hakuna nyingine

namuunga mkono lissu mnataka aseme halafu mpotoshe kama mlivyopotosha kauli ya mzee mtei.shame on you magamba
 
hivi wewe na elimu yako ya kuunga unga unaweza kumzidi tundu lisu? walikolalia ccm ndiko cdm walikoamkia.kwa nini itv hawakuita vyama vingine
 
Lissu alikua sahihi, japo wenzetu dini na siasa vinakwenda sambamba lakini lengo lao kuu la vurugu ni siasa kwa maslai ya dini..!lakini kaa ukijua wazanzibar wakilala wakiamuaka wanawaza uarabuni.!
 
Lisu yuko saws, uchomaji wa makanisa kunaueezekano mkubwa ikawa ccm wamefanya hivyo ili kuizima hoja ya kupinga muungano inayoongozwa na uamsho.
 
kisiasa yuko sahihi kabisa amesema kuokoa cdm, hasa nyakati hizi mbaya

kihalisia wale jamaa hawaupendi ukristo
 
Kwenye keyboard ya computer kila button ina kazi yake, wacha kutetea ujinga, wewe ndio mvivu wa kufahamu. Binafsi siwezi hata kupoteza muda wangu na kujiumiza macho kusoma thread ya namna hii isiyokuwa na mpangilio.

Kama hujaisoma mbona unachangia? bwana ee kama unaweza unaruhusiwa kuedit sio issue kuaibishana hapa.mi napita tu.
 
Huyo Lisu kuchemsha ni kawaida yake anafanya siasa kwa jazba anatafuta umaarufu kama wa Mh Zito au Mh Mbowe au Mh Dr Slaa kwa nguvu mara nyingi uropoka na kuteleza huyu jamaa hafai kuwa kiongozi mkubwa atatupeleka shimoni,wewe jiulize kuna mahusiano gani kutaka muungano ujadiliwe na kuchoma makanisa kwa nini wasichome misikiti au mali za serikali,hapo Tundu kachemsha sana tuongee ukweli tusiweke siasa manake kuna mijitu mingine itamtetea kwa sababu ni kiongozi wa chama chao ebu tuweke itikadi zetu kando tujadili ukweli wa jambo hili vinginevyo tukiwa tunajadili jambo kimtazamo wa kisiasa hatutafika ata kidogo,Mh Lisu katika hili kachemsha ata wachungaji na wananchi mbalimbali wamemshangaa!
tuliza munkari bro na ondoa bias zako za u ccm utaelimika zaidi.
 
Zimmerman na Wana JF,
Ukweli siku zote Unauma, Kwa mimi sioni ubaya wa Tundu Lissu, alichoongea ni maoni na mawazo yake, tukubali tukatae kuna elements za ukweli, tukumbuke kwenye Hotuba yake kama Waziri Kivuli, wengi walimbeza kama sio kumpinga. Tatizo ninalilioona na naona Hasira za Wanzanzibar ni kunyimwa Haki ya kuhoji na kupiga kura ya Maoni kuhusu huu Muungano, walichopewa ni kutoa Maoni, na hawajui kama hayo Maoni yao yatafanyiwa kazi au la. Ikumbukwe Mkuu wa Kaya alishasema kwenye Katiba Mpya Muungano usiguswe, so naona kama kuna maswali mengi juu ya Muungano ambayo yanajificha nyuma ya Pazia. Kikubwa kinachonipa maswali ni kauli ya Serikali kukubali kulipa gharama zote za huaribifu wa mali huko ZNZ. Hata hotuba ya Rais ya mwisho wa mwezi ameongelea hilo.
My take: Kuna matatizo makubwa kufanya mambo nyuma ya Pazia, mambo yasiyofuata Sheria na Kanuni za Nchi na Katiba ya Nchi.
Nawakilisha




Jana usiku nimemsikiliza kwa makini mheshimiwa Tundu Lissu kwenye kipindi cha Kipima Joto cha ITV kuhusu mada iliyosema, Je kundi la Uamsho lipo juu ya sheria? Argument ya Lissu ilikuwa kwamba fujo zote za Uamsho kuchoma moto makanisa kule Zanzibar, zisitazamwe kidini bali ziaminike zaidi kuwa ni frustrations za kisiasa hasa hasa kuhusu Muungano kwamba serikali imewaminya watu kuzungumzia uwepo au kutokuwepo kwa Muungano, bali imewapa option ya kutoa maoni ya kuuboresha. Akakoleza chumvi zaidi bwana Lissu pale alipotoa mifano ya Kanisa la kwanza East Africa kujengwa Zanzibar, na kwamba kule Egypt Ukristo umekuwepo more than 2, 000 years (Coptic Church), na uko kote (Zanzibar na Egypt) Waislamu walio wengi wameishi pamoja kwa amani na Wakristo walio wachache. Kwa hiyo udini wa Waislamu kuwachukia Wakristo kutokana na imani yao hauwezi kuwa hoja halisi iliyosababisha mali za Wakristo kuharibiwa hivi karibuni na Waislamu huko Egypt na Zanzibar bali siasa ndo mshtakiwa wa kwanza. Kwa haraka haraka unaweza ukaaminishwa na hoja hii ya Lissu pamoja na ushawishi wake wa hoja hiyo. Pamoja na kwamba mimi binafsi namkubali Lissu lakini hapa kaonyesha udhaifu mkubwa. Ni kama vile bwana Lissu kapitiwa hivi na mambo yanayoendelea ulimwenguni kuhusiana na vikundi vya aina ya Uamsho kwenye nchi zingine. Kuanzia kwa baba lao Al Qaeda, Al Shabab ya Somalia, Boko Haramu ya Nigeria, Taleban ya Pakistan na Afghanstan, na kadhalika. Kwa maoni yangu Uamsho ni kikundi tu cha kigaidi kama vikundi vinginevyo vyote nilivyotaja hapo juu, tofauti yake ni kwamba kipo katika hatua za kwanza za kuelekea ugaidi original. Vikundi vyote vya kigaidi hasa vile vinavyotumia uislam huwa vina jambo moja linaloviunganisha. Vyote ni fundamentalist kwenye theolojia yake na vinasukumwa na nia (kwao ni nia njema) ya kutaka kutakasa dini yao kutokana na hatari wanayohihisi kwamba nguvu za kisecular na kikiristo zinaikaba na wanataka kurudisha enzi zile za Uislam safi (sharia itawale serikali, “uchafu” wote kama bar, guest houses, na kadhalika usafishwe ili kurudisha imani halisi na iliyo safi). Al Qaeda kiliundwa baada ya Wamarekani kuweka bases zake za kijeshi Saudi Arabia ili kuipiga Iraq miaka ya 90, maana Osama bin Laden aliona ni aibu kwa nchi yake yenye makazi mawili matakatifu ya Allah (Mecca na Medina) kuweka bases za kijeshi, ishara ya kutawaliwa na Kafir mkuu, Marekani. Na kumbuka katika Uislamu siasa na dini haviwezi kutenganishwa, Lissu yampasa ajielimishe vizuri na theology ya Kiislamu. Boko Haramu, tafsiri yake ni Western Education is Haram, yaani elimu ya Magharibi ni haramu, unaweza kupata hisia kwamba dini inawasukuma kusafisha kila kitu kilicho na ideals za kimagharibi ukiwemo Ukristo na ndio maana Makanisa hayatakiwi kuwepo kule kaskazini mwa Nigeria. Uamsho ya Zanzibar ina vichembe hivyo hivyo vya kuhisi Zanzibar inaanza kukengeuka kutoka kwenye Uislam sahihi. Muungano unachukuliwa kama culprit wa kwanza aliyesababisha Zanzibar kujaa baa, vijiwe vya kiti moto, Makanisa ya Kikristo kila shehia ya Zanzibar, watoto wa kike wa kizanzibari kuanza kuvaa kama wabara, na megineyo mengi. Wale wote wanaotumia hoja ya kanisa la kwanza EA kujengwa Zanzibar, wanasahau kwamba enzi zile kanisa lilelilionekana kama siyo threat kwa utamaduni wa kiislamu, after all waliosali mule ni wazungu wawili watatu pamoja na weusi wachache. Kanisa lenyewe moja. Zanzibar ya sasa imebadilika sana siku za hivi karibuni. Makanisa yameongezeka sana na hili linawatisha Wazanzibari. Maredio mengi ya FM yameanzishwa na muziki wa bongo fleva unapigwa sana ikiwemo chombeza chombeza sex stories kwenye hizo redio. Hili linawakera sana mafundamentalists na wanaona pa kuanzia ni Muungano kuuvunja ili wapate control kamili ya kuendesha serikali kwa kanuni zisizofungamana kwa namna yoyote na katiba ya kisecular ya serikali ya Tanganyika. Lissu anaweza akawa na nia nzuri ya kutofungamanisha mainstream Islam na vurugu zinazojithibisha kidini. Lakini ukweli upo pale pale kwamba Uamsho na vikundi vinginevyo vilivyopo huko Zanzibar vipo motivated zaidi na dini. Tafsiri yao ya fundamentalist Islam ya kutotenganisha dini na serikali inaweza isiwe muafaka kwa wakati huu lakini hilo ndilo linalowasukuma. Kwao Uislam Zanzibar umeingiliwa na yapaswa kuusafisha. Kuvunja Muungano ni hatua ya kwanza, na kama wakifanikiwa hatua zingine zitafata.
 
Back
Top Bottom