Tundu Lissu, kwa hili, kachemka

Tundu Lissu, kwa hili, kachemka

Kusema kweli hili swala la muungano ni kitendawili kikubwa sana kwa Watanzania.
Jinsi muungano ulivyoundwa si kawaida sana. Wakati mwingine huwa nawaza kuwa Baba wa Taifa angegundua hili akalishughulikia kabla hajafa akalirekebisha likakaa sawa ingekuwa salama zaidi.

Kwa sasa tulipofikia na viongozi hawa tulio nao nashindwa kuamini kama kuna busara za kutosha kulishughulikia jambo hili lipate ufumbuzi wa kudumu ila kitakachotumika tena ni ubabe ule ule. Matokeo yake haliishi bali tunazidi kuliahirisha tatizo.

Kusema ni marufuku kujadili muungano au hata kasoro za muungano ni kukiri kuwa kuna udhaifu.
 
Mkuu ni lazima tuishi maisha ya kuvumiliana na kujaliana kama tunadhamira ya kweli ya kuishi kwa amani na utulivu kwenye jamii zetu, wakirsto wanaelekezwa kwamba kama kula kwao nyama kuna mkwaza mtu mwingine basi na waache kuila hiyo nyama, wanaekekezwa kuwapenda jirani zao kama wanavyojipenda wao, na wanashauriwa kutokuwaudhi watu wengine, hii ni katika kuhakikisha kwamba jamii za kikirsto zinaishi kokote pale duniani bila kukorofishana na jamii zenye imani tofauti.

Nikiwa mdogo nyumbani, ilikuwa ni marufuku kula kuku ambaye hajachinjwa na muislamu, kwa sababu waislamu huchukulia kuku ambaye hajachinjwa na muislamu ni nyamafu na hastahiri kuliwa, sasa kama kweli mmeamua kuishi kidugu kumuachia muislamu achinje kuku kuna matatizo gani.

Nasisitiza kwamba dunia inawajibika kujifunza namna ya kuishi na waislamu na kuziheshimu taratibu hizo, hakuna haja ya ushindani kwenye hili, athari za kutofanya hivi zinaeleweka vizuri sana, hata wewe yaya unazitambua acha ubabe na ubinafsi.

Sangara!

Inakubidi uwe mstaarabu angalau kidogo, hapa JF wanachangia kutumia simu za mkononi na kashalika sio wote wanaweza kuandika na kupanga paragrafu zipendeze. Cha msingi ni kuangalia hoja. Makosa ya typesetting na Mengineyo achana nayo.

Watanzania huwa mnakuwa na kumbukumbu ndogo. Uamsho ni CUF na kuchoma makanisa Huko Zanzibar Ilianza mwaka 2001 na hayo matukio ya mwezi wa Mei ni maendelezo tu ya sera ya CUF ya ngangari ambayo awamu ya Mkapa alipuuzia na kuwatumia wakina Mahita kutumia ngunguri. Mifano ya ukandamizaji tumeona matokeo yake Huko Misri.

Dawa ya ugonjwa sio kuuficha. Ni ukweli kwamba Muungano wa Zanzibar na Tanganyika ulikosewa na Hilo halina mjadala. Hata walioasisi Muungano wa Soviet waliweka katika katiba yao haki ya nchi kujitenga (self determination) kwa Sharti la kufanya referendum (kura ya maoni) na ndicho kilichofanyika. Federation ingefaa ila upeo wa waliounganisha ulikuwa finyu na ndio kiini cha tatizo.

Njia muafaka hawa akina CCM waache ukichwa ngumu tutumie nafasi hii kuandika mkataba wa Muungano upya na watu wapige kura kuhusu Muungano Kabla ya kupoteza muda kuandika katiba mpya bila kuwauliza Watanzania . CUF Msimamo wao wa ngangari wamewachia Uamsho behind the scenes and the main Zanzibaris wa Mrengo aw Dr. Bilal. Ushahidi CCM haikuchukua hatua zozote kupinga kuchoma makanisa for ten years pamoja na Bar. Zanzibar ni nchi ya kiislamu tena siasa Kali almost like Iran ukitaka kuona Hilo tembelea Zanzibar Mfungo Ramadhani halafu uthubutu kula mchana hadharani kitakukuta kilichonyoa kanga manyoya!

Uamsho ni Al-qaeda , Al shabab au Boko Haram ya Nigeria . Of course Wazenj wanaipenda hiyo taasisi. Huku Bara Rais Mwislam na Makamu wa Rais but for sure huu ni moto! Wapeni nchi yao kwani si mwaka Juzi mliwaruhusu Wakavunja Muungano and you keep on laughing ! Once more simwamini Jakaya Kikwete and his Mtandao hata wafanye ni it's sexed Muslim fundamentalists in a goats skin!
 
Zimmerman na Wana JF,
Ukweli siku zote Unauma, Kwa mimi sioni ubaya wa Tundu Lissu, alichoongea ni maoni na mawazo yake, tukubali tukatae kuna elements za ukweli, tukumbuke kwenye Hotuba yake kama Waziri Kivuli, wengi walimbeza kama sio kumpinga. Tatizo ninalilioona na naona Hasira za Wanzanzibar ni kunyimwa Haki ya kuhoji na kupiga kura ya Maoni kuhusu huu Muungano, walichopewa ni kutoa Maoni, na hawajui kama hayo Maoni yao yatafanyiwa kazi au la. Ikumbukwe Mkuu wa Kaya alishasema kwenye Katiba Mpya Muungano usiguswe, so naona kama kuna maswali mengi juu ya Muungano ambayo yanajificha nyuma ya Pazia. Kikubwa kinachonipa maswali ni kauli ya Serikali kukubali kulipa gharama zote za huaribifu wa mali huko ZNZ. Hata hotuba ya Rais ya mwisho wa mwezi ameongelea hilo.
My take: Kuna matatizo makubwa kufanya mambo nyuma ya Pazia, mambo yasiyofuata Sheria na Kanuni za Nchi na Katiba ya Nchi.
Nawakilisha
Mimi nadhani Lissu alikuwa anaangalia maslahi ya cdm Zanzibar....kuchomwa moto makanisa/kukashifu ukristo/kutisha wakristo havikuanza baada ya kukatazwa kujadili kuuvunja muungano. Hivi vitu vimeanza kutokea miaka mingi Zanzibar...
 
​@zimmerman
Ninachoamini ni kwamba Tundu yupo sahihi, na wanaochoma makanisa kule zanzibar siyo Kikundi cha Uamsho, bali vijana wa Dr. Shein ili wazanzibari na jamii iseme hawa jamaa wanachoma makanisa.
Hata mimi mwanzoni nilidhani kwamba waliochoma makanisa ni Uamsho, kumbe siyo!

Hapo nakupa 100% za bure, na Bwana Tundu nadhani kaliona hili kwamba ukweli sio udini kama inavodhaniwa na baadhi ya MaCCM, tatizo ni muungano na Wazenji sasa hv huna cha kuwaeleza tena juu ya jambo hili.

Miaka mingi (48yrs now) kuna kero za muungano zisizo na mwisho na kila cku zinaongezeka, ikiwa suala moja tu la mafuta limeshindwa kupatiwa ufumbuzi, jeee hayo mengine 40 unataraji nini ? Inabidi hapo tusubiri miaka 50 mingine!!!
 
Sweke34 na Wana JF,
Maslahi gani ya CDM ZNZ unayoangelea ?? Hoja yako ni nini hapa ??
Nawakilisha

Mimi nadhani Lissu alikuwa anaangalia maslahi ya cdm Zanzibar....kuchomwa moto makanisa/kukashifu ukristo/kutisha wakristo havikuanza baada ya kukatazwa kujadili kuuvunja muungano. Hivi vitu vimeanza kutokea miaka mingi Zanzibar...
 
Weka habari yake kwenye paragraph mkuu, great thinker your suppose not to present your idea this way. It is difficult for us to read and to follow.
 
Huyo Lisu kuchemsha ni kawaida yake anafanya siasa kwa jazba anatafuta umaarufu kama wa Mh Zito au Mh Mbowe au Mh Dr Slaa kwa nguvu mara nyingi uropoka na kuteleza huyu jamaa hafai kuwa kiongozi mkubwa atatupeleka shimoni,wewe jiulize kuna mahusiano gani kutaka muungano ujadiliwe na kuchoma makanisa kwa nini wasichome misikiti au mali za serikali,hapo Tundu kachemsha sana tuongee ukweli tusiweke siasa manake kuna mijitu mingine itamtetea kwa sababu ni kiongozi wa chama chao ebu tuweke itikadi zetu kando tujadili ukweli wa jambo hili vinginevyo tukiwa tunajadili jambo kimtazamo wa kisiasa hatutafika ata kidogo,Mh Lisu katika hili kachemsha ata wachungaji na wananchi mbalimbali wamemshangaa!

wewe funga domo lako linanuka unaongea mambo ya kishabiki,lete pointi zenye mshiko
kwa taarifa yako lisu ni zaidi ya hao uliowataja hapo juu
 
Jana usiku nimemsikiliza kwa makini mheshimiwa Tundu Lissu kwenye kipindi cha Kipima Joto cha ITV kuhusu mada iliyosema, Je kundi la Uamsho lipo juu ya sheria? Argument ya Lissu ilikuwa kwamba fujo zote za Uamsho kuchoma moto makanisa kule Zanzibar, zisitazamwe kidini bali ziaminike zaidi kuwa ni frustrations za kisiasa hasa hasa kuhusu Muungano kwamba serikali imewaminya watu kuzungumzia uwepo au kutokuwepo kwa Muungano, bali imewapa option ya kutoa maoni ya kuuboresha. Akakoleza chumvi zaidi bwana Lissu pale alipotoa mifano ya Kanisa la kwanza East Africa kujengwa Zanzibar, na kwamba kule Egypt Ukristo umekuwepo more than 2, 000 years (Coptic Church), na uko kote (Zanzibar na Egypt) Waislamu walio wengi wameishi pamoja kwa amani na Wakristo walio wachache. Kwa hiyo udini wa Waislamu kuwachukia Wakristo kutokana na imani yao hauwezi kuwa hoja halisi iliyosababisha mali za Wakristo kuharibiwa hivi karibuni na Waislamu huko Egypt na Zanzibar bali siasa ndo mshtakiwa wa kwanza. Kwa haraka haraka unaweza ukaaminishwa na hoja hii ya Lissu pamoja na ushawishi wake wa hoja hiyo. Pamoja na kwamba mimi binafsi namkubali Lissu lakini hapa kaonyesha udhaifu mkubwa. Ni kama vile bwana Lissu kapitiwa hivi na mambo yanayoendelea ulimwenguni kuhusiana na vikundi vya aina ya Uamsho kwenye nchi zingine. Kuanzia kwa baba lao Al Qaeda, Al Shabab ya Somalia, Boko Haramu ya Nigeria, Taleban ya Pakistan na Afghanstan, na kadhalika. Kwa maoni yangu Uamsho ni kikundi tu cha kigaidi kama vikundi vinginevyo vyote nilivyotaja hapo juu, tofauti yake ni kwamba kipo katika hatua za kwanza za kuelekea ugaidi original. Vikundi vyote vya kigaidi hasa vile vinavyotumia uislam huwa vina jambo moja linaloviunganisha. Vyote ni fundamentalist kwenye theolojia yake na vinasukumwa na nia (kwao ni nia njema) ya kutaka kutakasa dini yao kutokana na hatari wanayohihisi kwamba nguvu za kisecular na kikiristo zinaikaba na wanataka kurudisha enzi zile za Uislam safi (sharia itawale serikali, “uchafu” wote kama bar, guest houses, na kadhalika usafishwe ili kurudisha imani halisi na iliyo safi). Al Qaeda kiliundwa baada ya Wamarekani kuweka bases zake za kijeshi Saudi Arabia ili kuipiga Iraq miaka ya 90, maana Osama bin Laden aliona ni aibu kwa nchi yake yenye makazi mawili matakatifu ya Allah (Mecca na Medina) kuweka bases za kijeshi, ishara ya kutawaliwa na Kafir mkuu, Marekani. Na kumbuka katika Uislamu siasa na dini haviwezi kutenganishwa, Lissu yampasa ajielimishe vizuri na theology ya Kiislamu. Boko Haramu, tafsiri yake ni Western Education is Haram, yaani elimu ya Magharibi ni haramu, unaweza kupata hisia kwamba dini inawasukuma kusafisha kila kitu kilicho na ideals za kimagharibi ukiwemo Ukristo na ndio maana Makanisa hayatakiwi kuwepo kule kaskazini mwa Nigeria. Uamsho ya Zanzibar ina vichembe hivyo hivyo vya kuhisi Zanzibar inaanza kukengeuka kutoka kwenye Uislam sahihi. Muungano unachukuliwa kama culprit wa kwanza aliyesababisha Zanzibar kujaa baa, vijiwe vya kiti moto, Makanisa ya Kikristo kila shehia ya Zanzibar, watoto wa kike wa kizanzibari kuanza kuvaa kama wabara, na megineyo mengi. Wale wote wanaotumia hoja ya kanisa la kwanza EA kujengwa Zanzibar, wanasahau kwamba enzi zile kanisa lilelilionekana kama siyo threat kwa utamaduni wa kiislamu, after all waliosali mule ni wazungu wawili watatu pamoja na weusi wachache. Kanisa lenyewe moja. Zanzibar ya sasa imebadilika sana siku za hivi karibuni. Makanisa yameongezeka sana na hili linawatisha Wazanzibari. Maredio mengi ya FM yameanzishwa na muziki wa bongo fleva unapigwa sana ikiwemo chombeza chombeza sex stories kwenye hizo redio. Hili linawakera sana mafundamentalists na wanaona pa kuanzia ni Muungano kuuvunja ili wapate control kamili ya kuendesha serikali kwa kanuni zisizofungamana kwa namna yoyote na katiba ya kisecular ya serikali ya Tanganyika. Lissu anaweza akawa na nia nzuri ya kutofungamanisha mainstream Islam na vurugu zinazojithibisha kidini. Lakini ukweli upo pale pale kwamba Uamsho na vikundi vinginevyo vilivyopo huko Zanzibar vipo motivated zaidi na dini. Tafsiri yao ya fundamentalist Islam ya kutotenganisha dini na serikali inaweza isiwe muafaka kwa wakati huu lakini hilo ndilo linalowasukuma. Kwao Uislam Zanzibar umeingiliwa na yapaswa kuusafisha. Kuvunja Muungano ni hatua ya kwanza, na kama wakifanikiwa hatua zingine zitafata.

Naungana na wewe Zimmerman, Lissu alikuwa anaongea kisiasa ili kulinda maslahi ya CDM ambayo imetuhumiwa kuwa chama cha kikiristo mara kadhaa lakini ukweli unabaki pale pale kuwa uamsho ni kikundi cha kigaidi chenye mtazamo wa kiislamu kama vilivyo vikundi vingine vya BOKO HARAM ,AL QUEIDA, TALIBAN n.k Lengo la vikundi hivyo huwa ni Jihad ya kutetea imani ya kiislamu. Kama uchomaji wa makanisa ni frustrations kwa nini isichomwe misikiti? ina maana makanisa yamekuwa mengi sana kiasi cha kuwa spotted kirahisi kuliko misikiti? wangechoma na misikiti kadhaa tungekubali maelezo ya bwana Lissu.
Serikali na vyama vya siasa wanapiga siasa kuhusiana na yaliyotokea Zanzibar lakini amini usiamini 'usipoziba ufa utajenga ukua"
Napita tu!!!!
 
Nawashukuru wote mliojitokeza kuchangia thread yangu. Ninaomba samahani sikuwa online kwa siku mbili tatu hivi kufatilia thread yangu kwa wakati na ninasikitika sana kwamba iliwapa wakati mgumu sana kuisoma kutokana na kutopangika vizuri.

Niliandika hii post nikiwa na flu kali na kichwa kikiniuma hivyo nilishindwa kuconcetrate sana katika kuipanga vizuri. Flu hhiyo ndo iliniweka kitandani hivyo sikuweza kufatilia.

Kimsingi ndo hivyo kama baadhi yenu mlivyonisupport. Ukweli ni kwamba Uamsho ni udini mtupu.

Na kuna wale ambao wananishangaza sana kwa kuwa clueless na theologia ya kiislam. Wanaaminishwa kirahisi rahisi hivi na uongo wa Uamsho kwamba hawausiki na uchomaji wa mali za watu huko Zanzibar (maana wao ni waislam na uislam haufundishi kuharibu mali za watu).

Uongo. Tusipoelewa vizuri doctrines za Kiislam tutapelekeshwa sana na hawa wahuni wa kiislam. Hawa Uamsho ni kikundi kinachoongozwa na mashehe mafundamentalists wa Quran na Hadith za Mtume. Lengo lao kuu ni kuitawala Zanzibar kwa Sharia. Hili kufikia lengo lao ni lazima wapambane na nguvu za katiba iliyopo. Waliitumia CUF mwanzoni, sasa wanatumia fursa ya katiba mpya.

Lakini ni wajanja sana maana wanafata doctrine ya Kiislam inayoitwa "Stealthy War" au Vita ya Kificho. Hii ni doctrine inayowafundisha waislam kupambana kisiri bila adui kujua anapambana na jeshi la namna gani kimalengo na kimbinu. Na Uamsho walifanikiwa katika hili mpaka juzi juzi tu tulipowafahamu rangi zao halisi.

Kwanza walisajili kundi lao kama jumuia ya kidini yenye lengo la dini tu. Wakavuka mtego wa kwanza wa adui wakisubiri fursa nyingine. Pili, kwa kutumia mashehe charismatic wakaanza kuhubiri jinsi ya kuushamirisha Uislam. Kwa jinsi hii wakapata wafuasi wazanzibari vijana (jeshi) la kutosha. Tatu, mara fursa ikajitokeza ya kubadili katiba. Hapa ndipo nadhani walikosea step. Mahubiri yao yakabadilika sana yakawa ya kutukana Ukristo na kuukashifu Muungano. Chui mwenye mavazi ya kondoo akaanza kubweka kama chui. Na walipochoma makanisa hakukuwapo la kufichika tena.

Hata hivyo nakubaliana na Waberoya hapo juu kwamba kwa faida za kisiasa Lissu ilimpasa aseme hivyo (Waislam wana prejudices na Chadema na huu si wakati wa kuzidi kuwatenganisha na chama), kosa la Lissu pale ilikuwa ni kulegitimize kisiasa uhuni wa wana Uamsho.

Hayo ndo yangu.
 
Last edited by a moderator:
Tundu Lisu is right, kwanza una uhakika waliochoma hayo makanisa ni hao jamaa. Inawezekana yakawa yamechomwa na wachonganishi fulani hivi.
 
Jana usiku nimemsikiliza kwa makini mheshimiwa Tundu Lissu kwenye kipindi cha Kipima Joto cha ITV kuhusu mada iliyosema, Je kundi la Uamsho lipo juu ya sheria? Argument ya Lissu ilikuwa kwamba fujo zote za Uamsho kuchoma moto makanisa kule Zanzibar, zisitazamwe kidini bali ziaminike zaidi kuwa ni frustrations za kisiasa hasa hasa kuhusu Muungano kwamba serikali imewaminya watu kuzungumzia uwepo au kutokuwepo kwa Muungano, bali imewapa option ya kutoa maoni ya kuuboresha.

Akakoleza chumvi zaidi bwana Lissu pale alipotoa mifano ya Kanisa la kwanza East Africa kujengwa Zanzibar, na kwamba kule Egypt Ukristo umekuwepo more than 2, 000 years (Coptic Church), na uko kote (Zanzibar na Egypt) Waislamu walio wengi wameishi pamoja kwa amani na Wakristo walio wachache. Kwa hiyo udini wa Waislamu kuwachukia Wakristo kutokana na imani yao hauwezi kuwa hoja halisi iliyosababisha mali za Wakristo kuharibiwa hivi karibuni na Waislamu huko Egypt na Zanzibar bali siasa ndo mshtakiwa wa kwanza.

Kwa haraka haraka unaweza ukaaminishwa na hoja hii ya Lissu pamoja na ushawishi wake wa hoja hiyo. Pamoja na kwamba mimi binafsi namkubali Lissu lakini hapa kaonyesha udhaifu mkubwa. Ni kama vile bwana Lissu kapitiwa hivi na mambo yanayoendelea ulimwenguni kuhusiana na vikundi vya aina ya Uamsho kwenye nchi zingine. Kuanzia kwa baba lao Al Qaeda, Al Shabab ya Somalia, Boko Haramu ya Nigeria, Taleban ya Pakistan na Afghanstan, na kadhalika.

Kwa maoni yangu Uamsho ni kikundi tu cha kigaidi kama vikundi vinginevyo vyote nilivyotaja hapo juu, tofauti yake ni kwamba kipo katika hatua za kwanza za kuelekea ugaidi original. Vikundi vyote vya kigaidi hasa vile vinavyotumia uislam huwa vina jambo moja linaloviunganisha. Vyote ni fundamentalist kwenye theolojia yake na vinasukumwa na nia (kwao ni nia njema) ya kutaka kutakasa dini yao kutokana na hatari wanayohihisi kwamba nguvu za kisecular na kikiristo zinaikaba na wanataka kurudisha enzi zile za Uislam safi (sharia itawale serikali, “uchafu” wote kama bar, guest houses, na kadhalika usafishwe ili kurudisha imani halisi na iliyo safi).

Al Qaeda kiliundwa baada ya Wamarekani kuweka bases zake za kijeshi Saudi Arabia ili kuipiga Iraq miaka ya 90, maana Osama bin Laden aliona ni aibu kwa nchi yake yenye makazi mawili matakatifu ya Allah (Mecca na Medina) kuweka bases za kijeshi, ishara ya kutawaliwa na Kafir mkuu, Marekani.Na kumbuka katika Uislamu siasa na dini haviwezi kutenganishwa, Lissu yampasa ajielimishe vizuri na theology ya Kiislamu.

Boko Haramu, tafsiri yake ni Western Education is Haram, yaani elimu ya Magharibi ni haramu, unaweza kupata hisia kwamba dini inawasukuma kusafisha kila kitu kilicho na ideals za kimagharibi ukiwemo Ukristo na ndio maana Makanisa hayatakiwi kuwepo kule kaskazini mwa Nigeria.

Uamsho ya Zanzibar ina vichembe hivyo hivyo vya kuhisi Zanzibar inaanza kukengeuka kutoka kwenye Uislam sahihi. Muungano unachukuliwa kama culprit wa kwanza aliyesababisha Zanzibar kujaa baa, vijiwe vya kiti moto, Makanisa ya Kikristo kila shehia ya Zanzibar, watoto wa kike wa kizanzibari kuanza kuvaa kama wabara, na megineyo mengi.

Wale wote wanaotumia hoja ya kanisa la kwanza EA kujengwa Zanzibar, wanasahau kwamba enzi zile kanisa lilelilionekana kama siyo threat kwa utamaduni wa kiislamu, after all waliosali mule ni wazungu wawili watatu pamoja na weusi wachache. Kanisa lenyewe moja. Zanzibar ya sasa imebadilika sana siku za hivi karibuni. Makanisa yameongezeka sana na hili linawatisha Wazanzibari. Maredio mengi ya FM yameanzishwa na muziki wa bongo fleva unapigwa sana ikiwemo chombeza chombeza sex stories kwenye hizo redio.

Hili linawakera sana mafundamentalists na wanaona pa kuanzia ni Muungano kuuvunja ili wapate control kamili ya kuendesha serikali kwa kanuni zisizofungamana kwa namna yoyote na katiba ya kisecular ya serikali ya Tanganyika.

Lissu anaweza akawa na nia nzuri ya kutofungamanisha mainstream Islam na vurugu zinazojithibisha kidini. Lakini ukweli upo pale pale kwamba Uamsho na vikundi vinginevyo vilivyopo huko Zanzibar vipo motivated zaidi na dini. Tafsiri yao ya fundamentalist Islam ya kutotenganisha dini na serikali inaweza isiwe muafaka kwa wakati huu lakini hilo ndilo linalowasukuma. Kwao Uislam Zanzibar umeingiliwa na yapaswa kuusafisha.

Kuvunja Muungano ni hatua ya kwanza, na kama wakifanikiwa hatua zingine zitafata.



Hata wewe unatakiwa kuangalia source ya al qaida ni nini? sababu kuu ni siasa na dominations, ukiangalia al shabab pia ni siasa, maana somalia asilimia kubwa ni waisilam kuna udini wa namna gani wakati wanauana wote waisilam? Afghastan wote ni waisilam, Boko haramu imesababishwa na siasa si dini. Ndg yangu nenda tena library ukapashe. Nikipata muda wa kutosha nitakuelekeza hiki nilichokiandika hapa kwa mapana na marefu yake.
 
Naungana na wewe Zimmerman, Lissu alikuwa anaongea kisiasa ili kulinda maslahi ya CDM ambayo imetuhumiwa kuwa chama cha kikiristo mara kadhaa lakini ukweli unabaki pale pale kuwa uamsho ni kikundi cha kigaidi chenye mtazamo wa kiislamu kama vilivyo vikundi vingine vya BOKO HARAM ,AL QUEIDA, TALIBAN n.k Lengo la vikundi hivyo huwa ni Jihad ya kutetea imani ya kiislamu. Kama uchomaji wa makanisa ni frustrations kwa nini isichomwe misikiti? ina maana makanisa yamekuwa mengi sana kiasi cha kuwa spotted kirahisi kuliko misikiti? wangechoma na misikiti kadhaa tungekubali maelezo ya bwana Lissu.
Serikali na vyama vya siasa wanapiga siasa kuhusiana na yaliyotokea Zanzibar lakini amini usiamini 'usipoziba ufa utajenga ukua"
Napita tu!!!!

Ni vyema tukaangalia kwa undani masuala haya, tuache siasa, TALIBAN, AL QAIDA, AL SHABAAB, BOKO HARAMU, haya yote ni matokeo ya siasa, makundi haya yameanzia maeneo ambayo asilimia kubwa ya wakazi wake ni waisilam, kama ingekuwa tatizo ni dini nafikiri wasingeuana waisilamu kwa waisilam. Si vyema kufikia pahala tuseme kuwa dini fulani imechoma kanisa la dini fulani, nafikiri ni makundi ya wahuni waojiingiza katika harakati ambazo hawazijui, wanauamusho ni sawa na wakristo wanaojiita wameokoka, watu wa namna hiyo ni watu wenye hofu ya mungu, hawawezi kufanya kinyume na mapenzi ya mungu.

Kikubwa hapa ifahamike kuwa waisilamu wa zanzibar hawawezi uchoma makanisa, waliofanya hivyo ni wahuni na si wana uamusho. Ukiangalia kwa undani, watu wa Zanzibar wako tayari sahihi kuhusu mjadala wa muungano, na ni vyema wakapewa nafasi kuujadili, kwa karne hii huwezi kumuswaga binadamu mwenzako kama punda, anahitaji ajue unampeleka wapi na kwa nn? hivyo mfumo wetu wa siasa lazima uruhusu wananchi wake kuamua mambo yao kwa kufuata utashi wao na si utashi wa viongozi.
 
Hata wewe unatakiwa kuangalia source ya al qaida ni nini? sababu kuu ni siasa na dominations, ukiangalia al shabab pia ni siasa, maana somalia asilimia kubwa ni waisilam kuna udini wa namna gani wakati wanauana wote waisilam? Afghastan wote ni waisilam, Boko haramu imesababishwa na siasa si dini. Ndg yangu nenda tena library ukapashe. Nikipata muda wa kutosha nitakuelekeza hiki nilichokiandika hapa kwa mapana na marefu yake.

Ndugu nimenda library vya kutosha kuwasoma hawa jamaa. Ndiyo, they are power mongers lakini ni kwa sababu fulani. Sababu hiyo ni dini tu, pure and simple. Ngoja nifunguke zaidi.

Uislam unasimama chini ya Allah na mtume wake Mohammed (SAW). Mohammed anayechukuliwa kuwa mfano halisi wa waislam wote kuiga kwa kila nukta ya maisha yake kuanzia alivyovaa, alivyosema mpaka alivyokuwa anakula, alikuwa nabii wa dini ya Kiislam wakati huo huo akiwa kiongozi wa kisiasa/kiserikali. Kwa kipindi kirefu baada ya Mohammed kufa Uislam ulishamiri sana kutokana na conquest za majeshi ya Kiislam chini ya utawala wa makalifa wakiiteka Mashariki ya kati yote, Mashariki ya mbali, Ulaya Mashariki, pamoja na Afrika ya Kaskazini. Nusra tu waiingie Western Europe kupitia Spain kabla ya pope wa wakati ule kuamua kuwapinga na kuwakuzia mbali.

Kwa namna ya tofauti, nguvu za Ulaya na Marekani zimekua sana kisiasa, kijeshi na kitamaduni kwa kiwango kwamba zinawakaba au kuwagusa watu wote wa dunia, Waislam wakiwemo, popote pale walipo. Kwa ndugu zetu Waislamu mafundementalist hawataki kucope na hali halisi, wanataka kurudi kwenye enzi zile za Ukalifa. Kwa hiyo mara nyingi wanaamini kwamba serikali za nchi zenye Waislam wengi hazipaswi kuongozwa na viongozi masecular kama Hosni Mubarak wa Eygpt, Bashar Al Assad wa Syria au hata Mohammed Shein wa Zanzibar. Wanataka awepo mtu pale juu ambaye ni muislam aliyejaa Uislam tu na anayeota sharia mchana na usiku.

Al Shabab wa Somalia wanataka hilo. Huyu rais aliyepo Somalia alishawahi kuwa member wa Al Shabab. Alipofika Ikulu akatekeleza matakwa ya Sharia fulani fulani lakini wenzake hawakutafsiri kwamba aliyoyatekeleza ni Sharia in its purest form. Of course Sharia in its purest form tunaifahamu kwa jinsi Taleban walivyokuwa wanaongoza huko Afghanistan kabla ya kufumuliwa. Wanawake hawapaswi kumwona daktari wa kiume, wanawake hawapaswi kwenda shule na wavulana, mwanamke anaweza kuolewa hata kabla ya miaka 18, etc. Hivyo ndivyo wanavyotaka wenzako.

Kwa hiyo ndugu, kama unahisi Uamsho ni sawa na Walokole umekosea.
 
Back
Top Bottom