zimmerman
JF-Expert Member
- Feb 17, 2011
- 1,628
- 3,155
Jana usiku nimemsikiliza kwa makini mheshimiwa Tundu Lissu kwenye kipindi cha Kipima Joto cha ITV kuhusu mada iliyosema, Je kundi la Uamsho lipo juu ya sheria? Argument ya Lissu ilikuwa kwamba fujo zote za Uamsho kuchoma moto makanisa kule Zanzibar, zisitazamwe kidini bali ziaminike zaidi kuwa ni frustrations za kisiasa hasa hasa kuhusu Muungano kwamba serikali imewaminya watu kuzungumzia uwepo au kutokuwepo kwa Muungano, bali imewapa option ya kutoa maoni ya kuuboresha.
Akakoleza chumvi zaidi bwana Lissu pale alipotoa mifano ya Kanisa la kwanza East Africa kujengwa Zanzibar, na kwamba kule Egypt Ukristo umekuwepo more than 2, 000 years (Coptic Church), na uko kote (Zanzibar na Egypt) Waislamu walio wengi wameishi pamoja kwa amani na Wakristo walio wachache. Kwa hiyo udini wa Waislamu kuwachukia Wakristo kutokana na imani yao hauwezi kuwa hoja halisi iliyosababisha mali za Wakristo kuharibiwa hivi karibuni na Waislamu huko Egypt na Zanzibar bali siasa ndo mshtakiwa wa kwanza.
Kwa haraka haraka unaweza ukaaminishwa na hoja hii ya Lissu pamoja na ushawishi wake wa hoja hiyo. Pamoja na kwamba mimi binafsi namkubali Lissu lakini hapa kaonyesha udhaifu mkubwa. Ni kama vile bwana Lissu kapitiwa hivi na mambo yanayoendelea ulimwenguni kuhusiana na vikundi vya aina ya Uamsho kwenye nchi zingine. Kuanzia kwa baba lao Al Qaeda, Al Shabab ya Somalia, Boko Haramu ya Nigeria, Taleban ya Pakistan na Afghanstan, na kadhalika.
Kwa maoni yangu Uamsho ni kikundi tu cha kigaidi kama vikundi vinginevyo vyote nilivyotaja hapo juu, tofauti yake ni kwamba kipo katika hatua za kwanza za kuelekea ugaidi original. Vikundi vyote vya kigaidi hasa vile vinavyotumia uislam huwa vina jambo moja linaloviunganisha. Vyote ni fundamentalist kwenye theolojia yake na vinasukumwa na nia (kwao ni nia njema) ya kutaka kutakasa dini yao kutokana na hatari wanayohihisi kwamba nguvu za kisecular na kikiristo zinaikaba na wanataka kurudisha enzi zile za Uislam safi (sharia itawale serikali, uchafu wote kama bar, guest houses, na kadhalika usafishwe ili kurudisha imani halisi na iliyo safi).
Al Qaeda kiliundwa baada ya Wamarekani kuweka bases zake za kijeshi Saudi Arabia ili kuipiga Iraq miaka ya 90, maana Osama bin Laden aliona ni aibu kwa nchi yake yenye makazi mawili matakatifu ya Allah (Mecca na Medina) kuweka bases za kijeshi, ishara ya kutawaliwa na Kafir mkuu, Marekani.Na kumbuka katika Uislamu siasa na dini haviwezi kutenganishwa, Lissu yampasa ajielimishe vizuri na theology ya Kiislamu.
Boko Haramu, tafsiri yake ni Western Education is Haram, yaani elimu ya Magharibi ni haramu, unaweza kupata hisia kwamba dini inawasukuma kusafisha kila kitu kilicho na ideals za kimagharibi ukiwemo Ukristo na ndio maana Makanisa hayatakiwi kuwepo kule kaskazini mwa Nigeria.
Uamsho ya Zanzibar ina vichembe hivyo hivyo vya kuhisi Zanzibar inaanza kukengeuka kutoka kwenye Uislam sahihi. Muungano unachukuliwa kama culprit wa kwanza aliyesababisha Zanzibar kujaa baa, vijiwe vya kiti moto, Makanisa ya Kikristo kila shehia ya Zanzibar, watoto wa kike wa kizanzibari kuanza kuvaa kama wabara, na megineyo mengi.
Wale wote wanaotumia hoja ya kanisa la kwanza EA kujengwa Zanzibar, wanasahau kwamba enzi zile kanisa lilelilionekana kama siyo threat kwa utamaduni wa kiislamu, after all waliosali mule ni wazungu wawili watatu pamoja na weusi wachache. Kanisa lenyewe moja. Zanzibar ya sasa imebadilika sana siku za hivi karibuni. Makanisa yameongezeka sana na hili linawatisha Wazanzibari. Maredio mengi ya FM yameanzishwa na muziki wa bongo fleva unapigwa sana ikiwemo chombeza chombeza sex stories kwenye hizo redio.
Hili linawakera sana mafundamentalists na wanaona pa kuanzia ni Muungano kuuvunja ili wapate control kamili ya kuendesha serikali kwa kanuni zisizofungamana kwa namna yoyote na katiba ya kisecular ya serikali ya Tanganyika.
Lissu anaweza akawa na nia nzuri ya kutofungamanisha mainstream Islam na vurugu zinazojithibisha kidini. Lakini ukweli upo pale pale kwamba Uamsho na vikundi vinginevyo vilivyopo huko Zanzibar vipo motivated zaidi na dini. Tafsiri yao ya fundamentalist Islam ya kutotenganisha dini na serikali inaweza isiwe muafaka kwa wakati huu lakini hilo ndilo linalowasukuma. Kwao Uislam Zanzibar umeingiliwa na yapaswa kuusafisha.
Kuvunja Muungano ni hatua ya kwanza, na kama wakifanikiwa hatua zingine zitafata.