Tundu Lissu kumtetea Wema Sepetu

Tundu Lissu kumtetea Wema Sepetu

Jamaa anapiga kazi sana huyu,
mara yuko lokapu,mara katoka anamtetea fulani,mara yuko mahakama,hujakaa sawa press conference,huyu mtu anapumzikaga saa ngapi huyu?
 
Napata wasiwasi sana na watu wanaosema Lissu ni Mwanasheria bora sasa najiuliza kitu bora kina machaguo? ni sawa useme jembe langu ni bora then hapo hapo unalichagulia shamba la kulima

Sidhani kama wema anathamani kama Lema ndani ya Chadema ukizingatia Lissu ni mwanasheria wa Chama lakini sijawai kumsikia Lissu hata kuongelea kesi ya Lema

Lissu hana tofauti na zile shule zinazochagua wanafunzi wenye akili tu ktk interview zao then wanajiita shule bora kwa kuwa wanafunzi wote wamepata daraja la kwanza na la pili katika mitihani ya kitaifa lakini wameshindwa kujua tayali wanafunzi wale walikuwa na 50% kichwani so walichoongezea wao ni kama 20-24% tu

Unajua mtu aliyezoea kusifiwa akili yake inakuwa imejenga picha ya kujiona ni bora zaidi ya wenzie sasa siku wanaomsifia wakianza kupunguza kumsifia anajikuta anatafuta kitu chochote tu hata cha ajabu tu ili bado aendelee kuwa kwenye macho au masikio ya watu

Lissu alikuwa anasifiwa sana kwa weledi wake wa kujua sheria na vifungu Bungeni sasa nadhani watu wameshazoea anavyovifanya sasa inabidi atafute kitu kingine nje ya weledi wake Bungeni mpaka mitaani sasa na kudeal na vitu vidogo sidhani wajihi au heshima ya Lissu anaweza kujiingiza kwenye kesi ya kumtetea wema kesi ambayo hata vijana waliotoka chuo juzi wanaweza kushinda

Kazi anayotaka kufanya Lissu , Albert Msando anaiweza kwa kiwango kikubwa kuliko hata Lissu sema Lissu anatafuta political stunt
 
Inaonekana siku ile wamepelekwa wote mahakamani na kupanda gari moja Lissu akiwa mbele wema nyuma watakuwa waliongea mengi
 
Source Mwananchi

pic+lissu+kumtetea+wema.jpg

Msanii maarufu wa fani ya uigizaji wa filamu, Wema Sepetu

Kwa ufupi
  • Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), alijitokeza mahakamani jana kuwa wakili wa Wema na wenzake wawili akiwamo mfanyakazi wa ndani.

Dar es Salaam. Wakati Wakili Tundu Lissu akijitokeza kumtetea msanii maarufu wa fani ya uigizaji wa filamu, Wema Sepetu katika kesi ya kukutwa na bangi, mrembo anayepamba video za wasanii nchini, Agnes Gerald maarufu Masogange (28) amepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kutumia dawa za kulevya.

Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), alijitokeza mahakamani jana kuwa wakili wa Wema na wenzake wawili akiwamo mfanyakazi wa ndani.

Hata hivyo, Wakili wa Serikali, Constantine Kakula aliieleza mahakama jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika. Baada ya maelezo hayo, kesi iliahirishwa hadi Machi 15.

Katika tukio jingine, Masogange alipandishwa kizimbani mahakamani hapo akikabiliwa na mashtaka mawili ya kutumia dawa za kulevya aina ya heroini na oxazepam.

Akimsomea mashtaka jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbroad Mashauri, Wakili wa Serikali, Constantine Kakula alidai Masogange alitenda makosa hayo kati ya Februari 7 na 14, chini ya kifungu cha 18 (a) cha Sheria ya Kupambana na Dawa za Kulevya namba 5 ya mwaka 2015.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Masogange alikana na Hakimu Mashauri alimtaka mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili; kila mmoja alisaini bondi ya Sh10 milioni na anatakiwa asitoke nje ya Jiji la Dar es Salaam bila kibali cha Mahakama.



Hivi vita hii ni kuwa tafuta ma drug dealers au petty addicts? Hayo ndo makusudi kweli au ni janja ya kutaka kutusahaulisha benny?
 
Huyu wema si ndio alikuwa anajaribu kucheza "rafu" kwenye uchaguzi dhidi ya Tundu Lissu kule singida mashariki!!!!
Huenda Lissu ameamua kumfunga mdomo kiaina na usije shangaa uchaguzi mkuu ujao akajiunga kumpigia kampeni Lissu.
 
Hapa ukawa wamebugi!
Lisu siyo UKAWA,uwe na uwezo wa kutofautisha mambo.Pia Wema ni raia wa Tanzania anastahili kupata huduma za kisheria bila kuangalia yuko chama gani bali haki itendeke
 
Lissu kesi zitakuua...!! Huyu wemasepetu si alikuwa anatetewa na Albert Msando..imekuwaje tena?
 
Back
Top Bottom