Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,885
Msanii maarufu wa fani ya uigizaji wa filamu, Wema Sepetu
Kwa ufupi
- Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), alijitokeza mahakamani jana kuwa wakili wa Wema na wenzake wawili akiwamo mfanyakazi wa ndani.
Dar es Salaam. Wakati Wakili Tundu Lissu akijitokeza kumtetea msanii maarufu wa fani ya uigizaji wa filamu, Wema Sepetu katika kesi ya kukutwa na bangi, mrembo anayepamba video za wasanii nchini, Agnes Gerald maarufu Masogange (28) amepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kutumia dawa za kulevya.
Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), alijitokeza mahakamani jana kuwa wakili wa Wema na wenzake wawili akiwamo mfanyakazi wa ndani.
Hata hivyo, Wakili wa Serikali, Constantine Kakula aliieleza mahakama jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika. Baada ya maelezo hayo, kesi iliahirishwa hadi Machi 15.
Katika tukio jingine, Masogange alipandishwa kizimbani mahakamani hapo akikabiliwa na mashtaka mawili ya kutumia dawa za kulevya aina ya heroini na oxazepam.
Akimsomea mashtaka jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbroad Mashauri, Wakili wa Serikali, Constantine Kakula alidai Masogange alitenda makosa hayo kati ya Februari 7 na 14, chini ya kifungu cha 18 (a) cha Sheria ya Kupambana na Dawa za Kulevya namba 5 ya mwaka 2015.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Masogange alikana na Hakimu Mashauri alimtaka mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili; kila mmoja alisaini bondi ya Sh10 milioni na anatakiwa asitoke nje ya Jiji la Dar es Salaam bila kibali cha Mahakama.
Chanzo: Mwananchi
=======
Wema Sepetu kukamatwa na kuhukumiwa kwa kukutwa na madawa ya kulevya
- Wema Sepetu, Mr. Blue, TID, Recho wahusishwa na Dawa za Kulevya. Watakiwa kuripoti kituo cha Polisi
- Kamanda Siro: Wema Sepetu, TID na Nyandu Tozi bado wanashikiliwa na jeshi la polisi
- Sakata la Madawa ya Kulevya: Wema Sepetu afikishwa Mahakamani, apata dhamana
- Wema Sepetu kapatikana na bangi
- Tundu Lissu kumtetea Wema Sepetu
- Maajabu: Serikali haiwajui Vigogo wa Dawa za Kulevya hadi inataka Wema awatajie?
- Makonda kumfuata Wema mahabusu nyakati za usiku, hii imekaaje?
- Sauti ya Wema Sepetu iliyosambaa akiwatoa hofu Mashabiki
- Kesi ya Wema Sepetu hadi mwakani
- Wema Sepetu amefiwa, kesi yake yapigwa kalenda
- Dawa za Kulevya: Wema adai Makonda anatembea na Agnes Masogange ndio maana hakamatwi
- Wema Sepetu Apandishwa Tena Kizimbani Kisutu leo
- Vita ya Dawa za Kulevya: Steve Nyerere alivyopiga kambi Bungeni Kumuokoa Wema Sepetu
- Kesi ya Wema Sepetu yaahirishwa, uchunguzi haujakamilika
- Kutoka mahakamani: Wema Sepetu hakufanyiwa upekuzi kwenye maungo ya mwili wake, asema Hakimu
- Mkemia Mkuu: Mkojo wa Wema Sepetu ulikuwa na bangi
- Kibatala aandika barua ya kujitoa kesi ya Wema Sepetu, Alberto Msando aandika barua ya kuwa wakili mpya
- KISUTU: Wema Sepetu afika na Wakili wake Msando kwenye kesi. Diamond na Hamisa nao wafika Mahakama ya watoto
- Shahidi kesi ya Wema asema bangi ilikutwa jikoni
- Kisutu: Korti yakataa vielelezo vya ushahidi kesi ya Wema Sepetu. Masogange akutwa na kesi ya kujibu
Kuhukumiwa na kuachiwa huru baada ya kulipa faini