Uchaguzi 2020 Tundu Lissu hawezi kushinda Uchaguzi wa 2020, Dkt. Magufuli ana nafasi kubwa ya kushinda

Umesahau viongozi wako wa chama walivyotimka bungeni ila chadema matapeli sana, eti wakasubiri hadi posho ikaingia ndio wakakumbuka kuna corona

John Pombe Magufuli unayedai hajui kizungu ndio rais wako hutaki hama Nchi au kuwa rais wewe teheteheee

Kizungu kimekuingizia sh ngapi leo
Kumpa kura yako jiwe ni kujidhalilisha utu wako

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Ningekuwa mimi ni wewe ningetaka Lissu ashinde kwani sera zake za elimu zitakusaidia kupata ujuzi wa lugha ya malikia. Your English is terribly terrible!!

Na kujibu swali lako, kuna uwezekano mkubwa CCM wakatawala maisha yako yote, just be prepared
 
Kila kichwa kura 1 tu, omba namba ya wakala mwaminifu, akusimulie alichoona, na kwamba hakuna wizi wa kura kwenye kituo chenye wakala wa vyama mbalimbali.
Endeleeni kujifariji tu. Hakuna mwenye akili timamu atakayemchagua magufuli iwe kesho na keshokutwa Zanzibar na hata Keshokutwa Tanzania bara
 
Pale unapoandaa mechi marefa unawatafuta wewe na kuwalipa wewe ! Unamfuga mbwa miaka nenda rudi ataweza kukuuma? CCM mko kwenye comfort zone, ipo siku mtaingia uwanja huru Tafakari hayo!
 
Umeandika hisia zako, kama anaweza kushindwa, hata kushinda aweza.
JPM ameweka misingi ya nchi hii kupaa kimaendeleo kwenye akili wanajua, wanaotaka siasa na ufisadi hawapendi kabisa na wewe ni miongoni wao.
 
Pale unapoandaa mechi marefa unawatafuta wewe na kuwalipa wewe ! Unamfuga mbwa miaka nenda rudi ataweza kukuuma? Ccm mko kwenye comfort zone ipo siku mtaingia uwanja huru Tafakari hayo !
Uwanja uko huru siku zote
 
Ndiomana nami nikamuuliza?


Una uwakika gani watz wameridhika na yaliyofanyika? Una utafiti wowote uliofanyika nchi nzima ukang'amua hilo?
Amani na haki kipi humzaa mwenzake (hutangulia)?
Elezea hayo maneno yenye ushari mbele ya haki na uhuru unaoujua wewe..
Majibu ya swali lako utayapata baada ya 28 October 2020
 
Baki na CCM lako sisi tumeshastuka

Mungu ibariki chadema

Mungu ibariki Tanzania

Mungu mbariki Tundu Lisu
Screenshot_20201026-071802.jpg
 
JPM ameweka misingi ya nchi hii kupaa kimaendeleo kwenye akili wanajua....wanaotaka siasa na ufisadi hawapendi kabisa na wewe no miongoni wao
Bado ni hisia tu.
Lakini pia tunataka kiongozi atakaye tupaisha kiuchumi, bila kututeka, kutupoteza, wala ku temper na uhuru wetu.
 
Kwa wizi sawa ila tumeshuhudia watanzania maelfu kwa maelfu wakiikataa CCM kwa vitendo. Tumeshuhudia mgombea wa urais wa CCM kila aendapo anakwenda na konvoi la wasanii ili kujaribu kuwashawishi watu waende kwenye mikutano yake, tumeshuhudia mgombea huyo wa CCM akifunga shule na kuagiza watumishi wa umma na wanafunzi kuvaa sare za CCM ili wajaribu kuongeza umati.

Ni ukweli usiopingika kwamba CCM imekataliwa na wananchi wa Tanzania kwa sababu kuu ya kuminya UHURU wa kujieleza, Usalama wa wananchi hasa wakosoaji wa Serikali kuwa na wakati mgumu, kupotea, kubabikiziwa kesi zisizo na dhamana na hata kuuawa, Hali ngumu ya maisha waliyonayo watu, Ajira kwa vijana ni ndoto, vyeti feki vimeancha madonda makubwa mioyoni wa watanzania wengi, kuvunjiwa nyumba bila fidia nako, kutosaidia wananchi kwenye majanga ya kitaifa kama mafuriko na matetemeko kwa sababu kwamba serikali huwa haiyaagizi haya majanga kuwafuata wao.

Kifupi CCM haiwezi kushinda hiyo kesho kutwa !!! labda wafanye hujuma ya kupindua matokeo kitu ambacho kitakuwa hatari sana kwa usalama wa nchi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom